0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Dec 3, 2008

MCHANGO WA BWAYA JUU YA MADA HII YA MUDA, NAOMBA KUWASILISHA........


Huu ni mchango wa mwanablog mkongwe Bwaya, juu ya mada niliyoiandika kuhusu watu kujali muda. Nimeona niiweke hapa barazani ili wasomaji wengine watoe changamoto, kwani naona mada hii imeamsha hisia za wasomaji wengi.
Nikinikuu mojawapo ya makala alizoandika mwanzuoni huyu Bwaya, kwamba hakuna kujifunza bila kutofautiana, nami nakubaliana naye, juu ya kauli yake hiyo.
Jamani kutofautiana sio dhambi nakaribisha maoni zaidi.......


**********************************************

Nadhani kuna haja ya kuangalia kwa mapana zaidi maana hasa ya muda. Muda ni nini? Mimi nautazama muda kama kielelezo cha badiliko. Kama hakuna badiliko maana yake hakuna muda.

Kwa sababu muda maana yake ni hesabu ya tofauti ya badiliko moja na lingine.Penye badiliko la haraka maana yake muda kwa mukhtadha huo, utakuwa mfupi kuliko penye badiliko la taratibu.

Kwa hiyo muda unatokana na badiliko. Milele, ni dhana ya kutokuwapo badiliko. Yaani yalivyo leo, ndivyo yatakavyokuwa kesho na kesho kutwa. Kwa hivyo, muda hapo unakuwa sifuri.Mtu anapokufa, kwake muda ni sifuri hata kama saa yake inakuwa bado inatembea. Sababu ni kwmaba mwili wake hauna badiliko lolote la kibaolojia.

Na tumekwisha kutangulia kusema kwamba muda haupo bila badiliko.Kwa hivyo, tunaweza kusema, wazo kwamba muda uligunduliwa si sahihi. Muda haukugunduliwa. Muda ulikuwapo tangu badiliko la kwanza lilipoanza.

Kidini, uumbaji ulipofanyika.KInachoonekana kugunduliwa (kwa maana ya juu juu) ni namna ya kuhutathimini muda. Kwmaba sayansi imetuwezesha kuwa na njia za kimakenika kuutathimini muda haimaanishi kwamba muda umegunduliwa.

Vile vile wazo kwamba tufanye mambo yetu bila kutilia maanani muda nadhani linahitaji kutazamwa kwa tahadhari hata kama linaonekana kuwa na mantiki kisaikolojia. Sababu ni kwamba kutathimini muda, iwe kwa kutumia njia za kimakenika ama za asili, hutusaidia kuyatekeleza majambo hayo kwa kuzingatia kuwa na sisi kama viumbe tuna badilika na kuna siku tutakoma kubadilika.

Kama ingekuwa kwmaba hatubadikili, wazo la kutokuzingatia muda lingekuwa na nguvu. Lakini ni bahati mbaya kuwa sivyo ilivyo.Tofauti ya mawazo ni msingi wa mjadala. Asante kwa kazi nzuri ya kupangilia mjadala.


Wednesday, December 03,

Dec 1, 2008

KWA NINI MUDA UKUENDESHE?

Kwao hakuna kitu kinachoitwa muda.
Nilipoandika kuhusu mwili wa hisia, bwana Kitururu alikuja na hoja kwamba, ni vigumu sana kwetu kuuratibu mwili wa hisia kwa sababu ya ubize wa shuguli zetu za kila siku. Ukweli ni kwamba nilipinga hoja yake. Kwa nini?.
Kwa sababu wanaadamu wamejilundikia majukumu mengi kutokana na ushindani, kila mtu siku hizi anataka kushindana, katika kutafuta kuuridhisha mwili, ambao nao kamwe hauridhiki. Watu wanaishi kwa utashi na si kwa uhitaji, na ndio sababu ya tunashuhudia watu wakisingizia kuwa bize au kukimbizana na muda kutokana na mikanganyiko ya majukumu waliyojiwekea.

Kuna wakati niliwahi kusoma habari za watu wa imani ya Kihindu na wale wa imani ya Buddha, ambao kwao suala la muda au kuwa bize haliko, yaani hakuna kitu kinachoitwa muda kwenye maisha yao. Nami nakubaliana nao. Kuna wanaoamini kuwa muda ni pesa, au wanoamini kwamba muda una nguvu na unahitaji kutumiwa kwa njia ambayo inaonyesha kwamba unapewa heshima yake, ambayo ni lazima iwe kubwa kuliko binadamu mwenyewe.

Mtu asipokuwa makini anaweza kukubaliana kabisa na kauli au dhana hizi ambazo kwa nje zinaonekana zina uzito, wakati kwa ndani hazina kitu, ni tupu. Ni kauli au dhana ambazo zinaashiria kwamba, muda ulivumbuliwa na sio kwamba uliumbwa na binadamu.
Naamini unafahamu tofauti kati ya kuvumbua na kuumba. Kwa kawaida tunavumbua kitu ambacho ni cha kimaumbile na kilikuwepo siku zote, isipokuwa hakuna aliyekuwa amebaini kuwepo kwake. Kuumba ina maana ya kutengeneza kitu ambapo hapo awali hakikuwepo au kilikuwepo na kinatengenezwa tena na tena.
Binadamu alivumbua muda, kwani haukuwepo hapo awali. Mungu hakutengeneza kitu kinachoitwa sekunde, dakika, saa, siku, wiki, mwezi, mwaka, muongo, karne na vyote unavyovijua vyenye kupima muda. Mungu alitengeneza vile vitu ambavyo binadamu anadhani vilitengenezwa kwa sababu ya kupima muda. Wanatumia mzunguko wa dunia kwenye mhimili wake wa kulizunguka jua kama kipimo cha muda.

Lengo la mungu kufanya mizunguko hiyo haikuwa kupata muda, bali kitu kingine kabisa. Ndio maana suala la muda limeanza juzi tu, binadamu akiwa tayari ni mjanja. Kuna kuishi na kutenda yale ambayo mtu anaamini ndio yaliyomleta hapa duniani, lakini hakuna muda. Binadamu amevumbua muda kwa lengo la kujipa maradhi ya moyo, hofu na mashaka. Amevumbua muda katika hofu zake za kukabili kutokujua kwake amekuja hapa duniani kufanya nini. Kwa sababu ya muda anakwambia, “maisha ni mafupi sana”, au “ponda mali kufa kwaja”

Kama ukiweza kuishi bila kujali muda, unaweza kuanza kuhisi tofauti. Nikisema kuishi bila kujali muda, sina maana kwamba ukiambiwa umalize kazi uliopewa leo ukatae, hapana. Sisemi kwamba ukiambiwa mradi uliopewa ukamilike mwezi ujao, useme, “nitakamilisha siku yoyote’, hapana. Unapaswa kukumbuka kwamba ni wajibu wako kufanya kwa juhudi, kufanya kwa dhamira na kujitolea zaidi na zaidi, na sio juu yako kuendeshwa na muda wa mwisho uliopewa kukamilisha mradi huo (deadline)

Kama umefanya na imefikia mahali huwezi kukamilisha kwa kadiri ya muda uliojiwekea, au uliopewa, basi huna haja ya kujiuwa. Kama ni kazi yako, unajua namna ya kujiambia , na kama ni kazi ya mtu, ni suala la kujieleza na kujionesha ni kwa nini umeshindwa kwenda kwa mujibu wa ulivyotaka wewe. Kumbuka kwamba dunia hii imekuwepo na ilibeba watu, wanyama na mimea ya kila aina, lakini imepita yote. Hata kama utafanya usiku na mchana na asubuhi na jioni ili kuwahi muda usiishe, utaondoka nawe pia, ukiwa hujamaliza unayotaka kumaliza.


Nov 29, 2008

HOFU ZA MAISHA, SAWA, LAKINI........


Kuwa na hofu hutuwezesha kuchukuwa tahadhari, iwapo tutatafsiri matukio yanayotutokea bila kuongeza chumvi.



Nilipozungumzia kuhusu hofu na kuwataka watu wasihofie matukio ya kimaisha na kujitahidi kuyapokea kama yanavyokuja na kutulia kabla hawajiuliza wafanye nini, sikuwa na maana kwamba binadamu hatakiwi kuwa na hofu.

Ukweli ni kwamba hofu ni kama kitu cha kimaumbile ambacho humfanya Binadamu aweze kuishi.
Bila kuwa na hofu kabisa , kuna uwezekano hapo kuna tatizo la kiakili. Hii ni kwa sababu hofu kama hofu humsaidia binadamu kuweza kukwepa maafa na kusonga mbele.

Kuna zile hofu ,ambazo hizo tunaweza kusema ni kama lazima ziwepo, Kwa maisha haya na maumbile yetu binadamu, hizi hatuwezi kuzikwepa. Lakini hofu ambazo tunasema ni tatizo, ni zile zinazotokana na kuongeza chumvi mambo au kutafsiri mambo ndivyo sivyo. Kwa nini nasema hofu ni lazima kwa binadamu?

Hebu jaribu kuzunguka ukiwauliza watu kama wako tayari kuondolewa hisia za maumivu. Iwapo atatokea mtu na kukwambia kwamba angependa aondolewe hisia za maumivu kwenye mwili wake , yaani asihisi maumivu. Bila shaka jibu hilo litakuwa limetokana na ujinga, kwa nini?

Kwa sababu bila kuwa na hisia za maumivu ni vigumu kwako na kwangu kuishi. Maumivu ni muhimu kwa binadamu ili tuishi. Hofu ni kama hisia za maumivu, pia nayo ni muhimu. Kwa kuhofia jambo halisi tunaweza kujilinda na madhara au uharibufu wake.

Mtu anaweza kutamani kuingia baa na kunywa pombe na kula kuku, lakini akipata hofu kuwa atapunguza fedha za ada za watoto, itamfanya aachane na wazo hilo.
Mtu anaweza kumtamani sana mwanamke, lakini hofu kuwa anaweza kuwa mke wa mtu, (Je watu wanajali kuhusu hilo kweli?) au hofu kwamba ameathirika kwa ukimwi, huweza kumzuia kufanya jambo hilo ambalo matokeo yake ingekuwa ni maumivu.

Hali inapotafsiriwa vibaya huleta hofu isiyo na maana. Kwa mfano mtu anaweza kuwa na kijipu usoni, lakini kwa hofu zake kuhusu kansa akadhani amepata kansa, anaweza kuingia kwenye hofu na kuwatisha wengine walio karibu yake na kusababisha madhara mengi na makubwa..

Kuna watu ambao wakifukzwa kazi hufanya familia ione kama vile dunia imesimama na kila kitu kimepoteza maana. Ukweli ni kwamba mtu akipoteza kazi anaweza kuingia kwenye hofu ili aweze kurekebisha hali hiyo. Hii ni hali ya kawaida, lakini anapoanza kuwafanya wengine waamini kwamba, huo ni mwisho wa maisha , hapa tunasema hofu hiyo ni ya ujinga.

Tunapoingia kwenye hofu kimaumbile tunajiandaa kupambaana na kile kinachotuhofisha au tunajiandaa kukikimbia. Wakati mwingine tunatulia na kukusanya nguvu zetu zote ili kukikabili kile kinachotutisha.

Haiwezekeni hata hivyo katika hali halisi ya maisha kukimbia vile vitu vinavyotutisha. inabidi tupambane navyo, kama ni kufuzwa kazi inabidi tupambane na kufukuzwa huko kwa kukubali halafu tuamue kukusanya nguvu na kuanza kutafuta kazi mahali pengine au kufanya kitu kingine kitachotuwezesha kujikimu, badala ya kukaa na kujilaumu, ni kupoteza muda bure.

Kujaribu kukimbia ukweli huo ni kujidanganya bure. Kuna watu ambao hukimbia hali halisi kwa kunywa pombe, kuwa malaya, kugombana na kila mtu, na pengine hata kuamua kuachana na miili yao ( kufa). Bila shaka hawa ndio ambao ni dhaifu zaidi. Kujiuwa ni kutafuta suluhu ya kudumu kwa tatizo la muda mfupi.

Kumbuka jambo moja. Hata kama jambo litakuwa kubwa kiasi kwa gani, hatimaye ni lazima litafikia tamati. Kulikubali na kulikabili bila hofu ndio njia pekee ya kulifikisha kwenye tamati kimafanikio.

Kwa hiyo usiogope kuonekana kuwa una hofu, kwa sababu hofu ni suala la kimaumbile. Unachotakiwa ni kujichunga nacho ni kutafsiri vibaya matukio kwa kuongeza chumvi matukio na kujaribu kukimbia hali halisi.

Bado nasisitiza kuwa hofu zetu zisiwe ni dubwana la kutisha, kwa sababu ya kutafsiri kwetu vibaya matukio yanayotutokea katika maisha yetu, tukiweza kuratibu hisia zetu, basi tutaweza kukabiliana na hofu zetu kwa njia bora zaidi.


Nov 26, 2008

JE MWILI WA HISIA NI UPI?


Sema hisia zako, katika njia ambayo haitakuumiza au kuwaumiza wengine kihisia.


Mwili wa hisia:

Mwili wa hisia ni jumla ya hisia na mihemko yote. Hiyo ni kama, hasira, furaha, huzuni, sononeko, kero, kijicho, wivu n.k. Kila binadamu ana hisia kwani humsaidia kuishi. Mfano: bila hasira, utakufa baada ya muda mfupi kwani hutaweza kujilinda. Tunapaswa kutumia vizuri hisia zetu ili ziwe msaada kwetu na kwa wengine badala ya kuwa maumivu kwetu na kwa wengine.

Maumivu mengi ya kimaisha yanatokana na kushindwa kwetu kuzipeleka mahali bora hisia zetu ili zisitupe maumivu na badala yake ziwe na msaada kwetu. Kwa mfano: upande wa pili wa kijicho ni wa kujenga. Badala ya kuwa na hasira na kulaani na kumshusha aliyefanikiwa, mtu anaweza kujiambia kumbe inawezekana, na mimi nitajitahidi. Hapa ni kijicho kilekile ila kimegeuzwa kuwa wivu wa maendeleo (kutoa nafasi na muda kwenye kijicho katika mkabala wenye kujenga).

Watu ambao wanaweza kuitumia miili yao ya hisia vizuri, ni wale ambao wana utambuzi kuhusu mawazo yao, hisia zao na tabia zao. Wamejifunza namna ya kukabiliana na vema na matatizo ya kila siku ya kimaisha, ambayo hakuna anayeweza kuyazuia. Watu hawa hujihisi vizuri kuhusu wao wenyewe na hivyo wana uhusiano mzuri na watu wengine.

Kuna mambo mengi ambayo huwafanya watu kushindwa kuwa na afya njema kwenye miili yao ya hisia. Hebu fikiria kuhusu kupoteza kazi, kuanguka mtihani, kufiwa na mtu wa karibu, kuachwa na mpenzi, kuugua kwa muda mrefu au kuugua magonjwa hatari, kuwa na matatizo ya kifedha na mengine. Unaweza vipi kuyakabili haya, bila kuwa mwerevu kihisia? Ni vigumu.

Ukumbuke kwamba, mabadiliko mabaya au mazuri kwenye maisha yanaweza kuwa na athari mbaya kwenye miili yetu ya hisia. Mfano: kuhama, kupanda cheo, kuoa au kuolewa vinaweza kuvuruga miili yetu ya hisia. Tutaona ni kwa vipi kupanda cheo kunaweza kutuathiri vibaya wakati tutakapofika kwenye kipengele cha hasira na msongo. Hivyo bila kujali tuko katika hali gani, tunapaswa kujua namna ya kuratibu hisia zetu. Miili yetu hujibu mambo au kuwa katika hali fulani kutegemea na jinsi au namna tunavyofikiri, kuhisi na kutenda.

Uhusiano huu hufahamika kama uhusiano wa akili na mwili ( mind/body connection). Hivyo, unapoingia kwenye mashaka, wasiwasi na hofu, mwili wako hujaribu kukuambia kwamba, kuna jambo ambalo siyo sahihi (haliko sawa). Unapopata tukio au unapofikiria jambo ambalo litakuweka kwenye huzuni, kusongeka na kusononeka kwa muda mfupi au mrefu, unaweza kupata maradhi au matatizo ya kimwili kama vile: maumivu ya mgongo, kuumwa/ kubanwa kifua, kukosa choo, kuharisha, kinywa kukauka, kuchoka kupita kiasi, maumivu ya jumla ya mwili, kuumwa kichwa kisicho na maelezo rahisi, shinikizo la juu la damu, kukosa usingizi, kuhisi aina ya kizunguzungu kwa mbali, moyo kwenda mbio, matatizo ya tendo la ndoa, kukosa pumzi, shingo kukakamaa, kutoka jasho hovyo, usumbufu wa tumbo usioeleweka, kupungua uzito na vidonda vya tumbo.

Unaposhindwa kuuratibu vyema mwili wako wa hisia, huwa na afya duni na hivyo huuathiri mwili unaoonekana kwa kuuondolea kinga yake, ambapo maradhi hupata mahali pa kukimbilia. Maradhi yanapotupata, kama pia hatuwezi kuratibu mwili wetu wa akili, athari huja kwenye mwili huu unaoonekana na hivyo kuathiri mwili wa hisia tena, halafu huathiri mwili unaoonekana. Huu ni mzunguko thakili (vicious cycle). Mfano, mtu akifiwa na mkewe na akajaribu kushindana na hali hiyo (kuikataa) kwa kufikiri vibaya, na kuamua kutoa nafasi na muda kwa matatizo yaliyotokana au yatakayotokana na kifo cha mkewe kwa kujiuliza, kwa nini mkewe amekufa au amekufa kwa utata. Hali hii itasababisha hisia zake kukereka na hivyo zitaathiri kinga ya mwili. Mwili ukiathirika, ataanza kufikiri vibaya kuhusu mwili wake ( yaani ndiyo mimi kweli?). kwa kufanya hivyo, atachokoza hisia tena na hivyo kuumiza zaidi mwili huu unaoonekana. Ni mduara usio na mwanzo wala mwisho. Tunaposhindwa kufikiri vizuri, tunaishi kwenye mduara wa aina hiyo.

Jinsi ya kuwa na afya bora ya mwili wa hisia:

( i ) Kila wakati, tambua au fahamu upo kwenye hisia gani kwa kujenga urazini ( kujua kila wakati uko kwenye hisia gani na kwa nini?).
mfano, ukiwa na huzuni, jiulize ni kwa nini uwe na huzuni. Ukiwa na simanzi hivyohivyo. Usikubali kubeba hisia usizozipenda bila kufahamu ni kwa nini umezibeba.

( ii ) Sema hisia zako wazi na kwa njia nzuri. Usifiche hisia zinazoumiza kwani zitasababisha maumivu zaidi. Ni vyema mtu unayemwambia akawa mtu wa nje ya familia, inaonekana watu wa familia wameshindwa kumudu kuwasaidia jamaa zao kutoka kwenye maumivu ya kihisia. Kama unajisikia kulia, lia sana, kama ni kucheka, cheka sana. Usijaribu kukandamiza hisia kwani utaumia. Wanaume waliambiwa kulia ni tabia ya kike. Huu ni ujinga mwingine wa ukweli wa kimapokeo, ukatae.

( iii ) Ishi maisha yenye uwiano bora. Usiwaze sana kuhusu matatizo ya kazini, nyumbani au popote ambayo yatakufanya usifikiri vizuri. Hii haina maana ujifanye kwamba umefurahi, wakati umejaa mashaka na hofu tele. Fahamu kwamba, kufikiri vizuri ndiko kunakoweza kukusaidia kukabiliana na matatizo na siyo kufikiri vibaya. Weka nguvu kwenye mambo au vitu ambavyo vitakupa nguvu na ahueni. Kumbuka, hisia kama hisia hazina tatizo, kama ambavyo hakuna kitu au jambo lenye tatizo, bali wewe. Kama ukishindwa kuzipeleka hisia zako namna na mahali panapostahili, zitakuumiza.

Werevu wa kihisia (emotional intelligence):

Ukweli ni kwamba, kila siku huwa tunakabiliwa na hisia nzuri au mbaya.
Je, tuwazuri kiasi gani katika kuzisimamia? Huwa unakabiliana vipi na hasira? Hofu? Kuvunjika moyo? N.k. Je, ni nani alikufundisha kuchukulia hisia kama ufanyavyo? Je, unaweza vipi kupokea, kuonesha, kuelewa na kuratibu hisia zako na za wengine kwa njia isiyoumiza.

Werevu wa kihisia ni ule uwezo wa kudhibiti hisia zako na za wengine ili zisikuumize wewe au wengine. Kila binadamu anaweza kuratibu hisia zake akitaka. Hisia hizi ni kama kucheka, kukasirika, kuhisi kijicho, hofu, kuvunjika nguvu, wivu, huzuni, furaha n.k. karibu hisia zote ni miito ya kibaologia. Hakuna binadamu anayeweza kupinga kutokewa nazo. Lakini pale zinapozidi au zinaposhindwa kupatikana kwa mazingira muafaka huweza kusababisha matatizo.

Kwa sehemu kubwa tumejifunza kuhusu hisia kutoka kwa watu wa karibu yetu tangu tukiwa wadogo kwa kuona na kusikia. Hatufundishwi shuleni namna ya kuratibu hisia zetu, bali wazazi na walezi wetu walitufundisha. Lakini tukiwa wakubwa (ukubwani) ni muhimu sana kujifunza namna ya kuratibu hisia zetu ili zisituumize au kuwaumiza wengine. Watu ambao wanamudu kuratibu hisia zao na kuwawezesha kutowaumiza huwa na uhusiano mzuri na watu. Tunasema, watu hawa ‘wana werevu wa kihisia’

Vyanzo vya migogoro ya hisia:

i. kuchukulia mambo kibinafsi (personal).

ii. kutosikiliza.

iii. kutojua lugha nzuri katika kujieleza.

iv. kutozingatia hali ya hisia ya mzungumzaji.

v. hisia za watu wengine ni zao, usichukulie kuwa ni wewe umewakera.

vi. usijali matokeo, jieleze au wasikilize watu wengine kwa kadri ya uwezo wako wa utulivu, waache waamue.

Sifa zinazobainisha werevu wa kihisia:

(i) Mtu mwenye werevu wa kihisia anajua hisia zake na kuweza kutambua ni nini anafikiri katika muda mwingi. Kumbuka, baada ya kufikiri hufuata hisia. Ukijua unachokifikiri, utajua kirahisi ni kwa nini unahisi kwa namna unavyohisi.

(ii) Mtu mwenye werevu wa kihisia ana uwezo wa kuzidhibiti hisia zake na kujua namna ya kuzifanyia kazi. Kama ni hasira anajua kuzidhibiti na kujua zitamfaidisha vipi badala ya kumpa hasara. Kama amekasirika kwa sababu amedharauliwa, badala ya kutukana na kutaka vita, ataamua kurekebisha au kuboresha eneo lililomfanya achekwe, bila kinyongo kwa aliye mcheka.

(iii) Mwenye werevu wa hisia ni mtu ambaye hakati tama hata pale panapoonekana kwamba kuna vikwazo vikubwa. Kumbuka jambo moja, kukata tama hutokea akilini, ambapo huzifanya hisia za mtu kuingia kwenye kukasirika, kukosa matumaini au chochote.

(iv) Mtu mwenye werevu wa kihisia ana uwezo wa kusoma mawazo ya wengine na kuyaelewa. Kusoma mawazo yaw engine maana yake ni kumudu kujua wengine watajihisi au wanajihisi vipi kwenye mazingira fulani. Kuna watu ambao hawajui nikisema au kufanya nini kwa mtu au watu gani watajihisi vipi. Huongozwa na hisia tu. Wakifurahi au kukasirika wanaweza kusema au kufanya kwa njia yenye kuwaumiza sana wengine. Huu ni udhaifu.

(v) Mwenye werevu wa kihisia ana uwezo wa kujenga na kudumisha uhusiano bora kazini, na marafiki, wapenzi, na watu walio katika familia yake. Hii inatokana na ukweli kwamba, kwa kumudu kuziratibu hisia zake vizuri, hawakeri watu kirahisi.


Njia zitakazokuwezesha kuratibu hisia zako:

(i) Unatakiwa kujua kwamba unazo hisia na huwa zinajitokeza kwako. Mfano_ jua kwamba, sasa umekasirika, sasa umefurahi au sasa umehuzunika. Watu wengi huwa hawajui kwamba wako kwenye hisia fulani, hivyo wanapokuwa kwenye hisia hizo, wanafanya mambo kimazoea (wanarudia makosa).

(ii) Ukishagundua kwamba upo kwenye hisia fulani unatakiwa ‘utulie’ usifanye kitu chochote. Hii inakupa nafasi nzuri zaidi ya kudhibiti hisia zako, siyo hisia zikudhibiti wewe.

(iii) Kubali kwamba upo kwenye hisia fulani. Kuna wakati mtu anakasirika lakini anapingana na ukweli huo. Kuna wakati mtu anahisi kijicho dhidi ya mafanikio ya mtu mwingine, lakini anajitahidi kupingana nayo kwa kujiambia “simwonei kijicho” bali anaringa ndiyo maana namchukia. Jaribu kukiri, kukubali kwamba uko kwenye hisia fulani kwani hisia siyo dhambi.

(iv) Unapokuwa kwenye hisia fulani usijaribu kufikiri au kufanya jambo lolote kwani hutamudu. Hisia zinapokuwa juu mantiki haifanyi kazi. Matumizi ya akili na hisia za juu au kuhemkwa haviwiani. Kama umekasirika sana usifanye jambo kwani utakachokifanya kitakuwa ni upuuzi. Ndani ya hisia kali hakuna matumizi ya akili, subiri hisia au furaha yako iwe katika hali ya kawaida ndiyo ufikiri na kutenda.
Kumbuka kwamba si vyema kujaribu kuwasiliana na mtu mwingine kwa kufuata hisia zake. Usivutwe na ndoano ya mtu mwingine. mfano: uko na rafiki yako ghafla akakasirika, wewe usikubali kukasirika, ukikubali ina maana umekubali kunaswa kwenye ndoano au mtego wake.

Hivyo mtu anapokasirika, unachotakiwa kufanya ni wewe kutulia, badala ya kuambukizwa na hasira zake. Unachotakiwa kufanya, ni kumwambia kwamba, ‘naona umekasirika, basi tutajadili au tutaongea baadaye’. Ukivutwa na hasira zake na ukajikuta na wewe
umekasirika hujitendei haki na hivyo umeshindwa kuwa na werevu wa hisia. Lakini pia, kubali hisia za mwingine. Aliyehemkwa hajui asemacho wala atendacho.

(v) Usimeze hisia zako, badala yake ziseme. Kama umekasirika mwambie mtu kwa upole, lakini kwa dhati kuwa umekasirika.
Ukimeza hisia, zitakuja kulipuliwa na jambo dogo sana. Lakini pia, ukimeza hisia zako watu hawatajua kwamba jambo fulani hulitaki, hivyo watakukera bila kujua. Waambie watu kama wanakukera jambo fulani au kama wanapaswa kukufanyia au kutokukufanyia jambo fulani. Weka mipaka ili usiingiliwe hovyo. Hupaswi kuogopa kusema hisia zako, bali ziseme kwa njia ambayo haitakuumiza au kuwaumiza wengine. Ukitulia, yaani ukiwa haupo kwenye mhemko, ndipo unapopaswa kusema hisia zako.

(vi) kwa kadri jinsi unavyokuwa na werevu wa kihisia zaidi, ndivyo unavyoweza kuwa na uhusiano mzuri na watu wengine na kuweka mipaka. Kwa kwawaida, sisi wote tuna mipaka ya kimwili (hii inayoonekana). Mipaka ya kihisia, ya kiakili na ya kiroho. Hii huwa hatuioni (haionekani). Hivyo, tunapaswa kuheshimu mipaka yetu.


Kwa Makala hii naamini sasa wasomaji wataelewa ni kwa jinsi gani maarifa haya ya utambuzi yamelenga kuwasaidia watu kwa kiasi gani, kwani kimsingi ukifahamu miili hii mitatu jinsi inavyofanya kazi na ukaweza kuidhibiti na kuiendesha na sio ikuendeshe wewe, basi maisha kwako yatakuwa ni rahisi sana.
Bado nitakuwa najadili mada tofauti tofauti kulingana na jinsi nitakavyoona, na kama kutakuwa na hoja mbalimbali kutoka kwa wasomaji wa blog hii, nitaziweka hapa barazani ili tusaidiane kujadili na kupata mawazo tofauti tofauti kutoka kwa wasomaji wengine.

Naomba kuwasilisha.









MTOTO WA MIEZI MINNE AZUNGUMZA MAZITO

Habari hii nimeidesa kutoka kwenye mtandao wa Jamii Forums.


Na Mashaka Mhando, Tanga


MTOTO wa miezi minne aliyezaliwa kwenye hospitali teule wilayani Muheza, amekuwa gumzo na kustaajabisha wakazi wa mji huo, wakiwamo wazazi wake, kutokana na kuzungumza akiwa na umri huo. Mtoto huyo pichani aliyezaliwa Julai 16 mwaka huu, licha ya kuzungumza, pia amekuwa kituko kutokana na kutaka aitwe majina matatu ya Glory, Halima na Upendo, pindi anapoitwa na mtu yeyote akitaka kumsalimia.

Akizungumza juzi kwenye ofisi za gazeti hili barabara ya 15 Jijini hapa, mama wa mtoto huyo Bi Rosemary Mhina, mkazi wa mtaa wa Bin Seif, wilayani Muheza, alidai kuwa mtoto wake huyo ni wa ajabu kwani tangu akiwa mjamzito wa miezi saba, alikuwa akilia tumboni. "Kwanza nilipokuwa na mimba, tumbo lilikuwa linaniuma sana, nilipofikisha miezi saba tumbo likiniuma, utamsikia mtoto analia tumboni, nikaenda hospitali, nilianzia Teule, nikaja huku Bombo na

Tumaini, nilipopigwa 'ultra-sound' madaktari wakanieleza kuwa nitajifungua mtoto wa kiume, waliyemwona tumboni kwa kifaa hicho," alisema Bi Rosemary. Akielezea zaidi kuhusu namna alivyobaini mtoto wake kuwa na mawasiliano na watu, mama huyo alidai kuwa mara baada ya kuzaliwa, alipofikisha miezi miwili, siku moja alilia sana wakati akimbembeleza "Nyamaza mwanangu usilie ngoja nikupewa maziwa".

Alisema baada ya kumweleza hivyo, mtoto huyo alitamka maneno yaliyomtisha mama yake huyo: "Mama usione nalia, nalizwa na mengi, kwanza baba alitaka uniue nikiwa tumboni, halafu maisha yako si mazuri mama nakuonea huruma." Bi Rosemary alikiri kwamba baada ya kupata ujauzito kutoka kwa mwanaume (jina tunalihifadhi) ambaye amedai kwamba anafanya kazi katika hospitali ya Mount Meru, Arusha, alimpa sh. 30,000 ili akaitoe hospitalini wakati mimba hiyo ilipofikisha miezi sita. "Yule baba alitaka nikatoe mimba ya mtoto huyu nikakataa, hata hivyo wazazi wangu hawakutaka mimi nizae baada ya kuwa na watoto wawili, niliogopa pengine ningefanya hivyo ungekuwa mwisho wangu," alidai Bi Rosemary.

Aliendelea kudai kuwa tangu mwanawe huyo awe naye amekuwa akitokewa na miujiza mingi na kipindi alichoanza kuzungumza, alimpeleka kwa wachungaji mbalimbali ili kumwombea, lakini kila anapokwenda huko akirudi anatokewa na vituko. "Kipindi kimoja nilimpeleka kuombewa, usiku niliona paka wengi ndani nilimolala wakaniparura huku mwanangu Upendo akinicheka," alidai. Mama huyo ameomba watu wamsaidie ili mtoto huyo asiwe na vituko hivyo kwani hivi sasa baba wa mtoto amemkimbia na hana mawasiliano naye tena.

HAKIKA DUNIANI KUNA MAMBO

KITUO CHA FAJI KIMARA ROMBO


Kuna mdau kanitumia sms, kuwa picha ya ofisi za FAJI niliyoeweka hapa, maandishi yake hayaonekani vizuri. haya nimeamua kubandika hii, Je nayo maandishi hayaonekani vizuri?

Nov 25, 2008

MWILI WA AKILI UNAFANYAJE KAZI?



Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa mwezeshaji wa utambuzi katika kituo cha FAJI, Dr. John Simbila.

Mwili wa akili:

Akili ni uwezo wa kuelewa na kujifunza mambo au uwezo
wa kufikiri na kuamua kwa busara. Ubongo ni bonge laini la
nyamanyama lenye mishipa ya fahamu lililomo kichwani. Jiulize, je, akili inazalishwa kwenye ubongo au inapitia tu kwenye ubongo ikitokea mahali fulani?

ubongo – ubongo umegawanyika katika sehemu tano:
( I ) Ubongo wa thalamus.
(II ) Ubongo wa hypothalamus.
( iii) Ubongo wa cerebellum.
( iv ) Ubongo wa shina (brain stem )- huu umegawanyika sehemu tatu:
i. Ubongo wa kati ( mid brain ).
ii. Ubongo wa pons valorii.
iii. Ubongo wa medulla oblongata.

(v ) ubongo wa cerebrum.

Huu ni mkubwa kuliko sehemu nyingine za ubongo.
Hutafsiri na kusimamia matendo yaliyo chini ya uamuzi wa mwili kama vile, kutoa sababu, kupanga mipango, kuhifadhi kumbukumbu, kutatua matatizo. Pia ni kitovu cha akili na haiba.

Ubongo huu umegawanyika sehemu 2:

i. Ubongo wa kushoto- husimamia upande wa kulia wa mwili. Hupokea na kutafsiri taarifa pamoja na kuratibu utendekaji kazi wa misuli upande wa kulia wa mwili.

ii. Ubongo wa kulia – husimamia upande wa kushoto wa mwili. Hupokea na kutafsiri taarifa pamoja na kuratibu utendekaji kazi wa misuli upande wa kushoto wa mwili.
Hali hii ( hapo juu ) inatokana na mishipa ya fahamu inapopita kati ya ubongo wa medulla oblongata na uti wa mgongo kupashana kwenda upande wa pili.

Karibu asilimia 90 ya watu wote duniani, ubongo wao wa kushoto unahusika na mantiki – orodha, maneno, tarakimu, mfuatano na uchambuzi. Wakati ubongo wao wa kulia unahusika na ubunifu, mapigo, rangi, kujenga taswira, ndoto za mchana, utambuzi maalumu, muziki na usanii. Lakini kwa baadhi ya watu, utendaji kazi huu wa ubongo huwa ni kinyume, na kwa watu wachache huwa hakuna tofauti.

Uchunguzi wa kitaalamu unaonyesha kwamba:

( I )Ubongo wa kushoto – unafanya kazi zaidi ya asilimia 90 kwa wale wanaotumia mkono wa kulia na asilimia 64 kwa wale wanaotumia mkono wa kushoto.

( ii ) Ubongo wa kulia – unafanya kazi kwa asilimia 10 kwa wale wanaotumia mkono wa kulia ni asilimia 20 kwa wale wanaotumia mkono wa kushoto.

(iii) Asilimia 16 iliyobaki ya watu wanaotumia mkono wa kushoto, ubongo wao wa kushoto na wa kulia unafanya kazi sawa.

Kumbuka kwamba, ubongo wa thalamus, hypothalamus kwa kushirikiana na sehemu za ubongo wa cerebrum kwa pamoja huunda mfumo unaoitwa mfumo wa limbiki (limbic system). Mfumo huu huhusika na kuhifadhi kumbukumbu pamoja na hisia kama vile huzuni, furaha, hasira, hofun.k. Hufanya kazi ya kurekebisha hisia zinazoimarisha uhai ( bila hisia, hakuna uhai).

Milango ya fahamu – hutujulisha kinachoendelea katika mazingira ya nje (mazingira yanayotuzunguka) ili mwili uweze kuchukua hatua zilizo chini ya uamuzi wa mwili au ambazo haziko chini ya uamuzi wa mwili na hivyo kuimarisha mazingira ya ndani ya mwili ( homeostasis) .
Lakini, mbona kuna wengine milango yao ya fahamu haifanyi kazi? Ina maana wao hawafahamu kuhusu mazingira yanayowazunguka? Je, hizi taarifa zinazotolewa na milango ya fahamu zina ukweli kiasi gani? Hebu jiulize kama kweli taarifa zote kuhusu mazingira yanayokuzunguka zinatolewa na milango ya fahamu.

Ulishawahi kusikia kuhusu machale? Ni kitu gani hiki? Ni mlango upi wa fahamu? Wataalamu wanasema kwamba kwenye ubongo wa kulia kuna eneo linaloitwa intuitive area (eneo la machale ) ambalo ndiyo linaloto taarifa za kweli kuhusu mazingira yanayotuzunguka. ( Machale ni mada inayojitegemea nitaijadili baadae katka makala zangu)

Kuna aina kuu mbili ya milango ya fahamu:

1. Milango ya fahamu mjumuisho – iko mitatu

i.Mlango wa joto – huhisi baridi na moto.
ii. Mlango wa mgandamizo na mguso – hihisi mgandamizo na mguso.
iii.Mlango wa maumivu – huhisi maumivu. Maumivu ni
muhimu sana kwa uhai. Hutufahamisha hatari inayotokea kwenye miili yetu ili tuweze kuondoa kihatarishi au tuhitaji matibabu.

2. Milango maalumu ya fahamu – hii ipo minne.
( i ).Mlango wa kunusa ( pua )- husaidia kunusa harufu mbalimbali. Husaidia kuchagua chakula kwa kusaidiana na mlango wa kuonja (ulimi). Tunanusa chakula na wakati huohuo tunaonja chakula. Ukiwa na mafua ladha ya kitu au chakula huwa ikoje?

( ii ) Mlango wa kuonja (ulimi) – husaidia kuonja ladha ya kitu au chakula kusaidiana na mlango wa kunusa(pua). Kuna aina nne za vionjo vilivyopo kwenye ulimi, navyo ni: vionjo vya utamu (mbele ya ulimi) – kuonja vyakula vitamu. Vionjo vya ukakasi (pembeni ya ulimi) - kuonja vyakula vyenye ukakasi. Vionjo vya chumvi (sehemu yote ya ulimi) – kuonja vyakula vya chumvi. Vionjo vya uchungu (nyuma ya ulimi) – kuonja vyakula vichungu.

( iii ) Mlango wa kusikia (sikio) – hufanya kazi mbili: kusikia pamoja na kuweka mwili sawa (kuubalansi) . Mawimbi ya sauti hupimwa kwa kutumia kipimo kinachoitwa decibels scale(Db). Mtu akikaa kwa muda mrefu kwenye eneo au sauti inayozidi 90dB huweza
kusababisha tatizo la kudumu la kutokusikia, mfano: sauti
inayotolewa kwenye amplifaya 120dB, sauti inayotolewa na ndege wakati wa kupaa 140dB. Taarifa ya kusikia kutafsiriwa na pande zote mbili za ubongo wa kulia na ule wa kushoto. Sikio pia hutumika kuimarisha wima wa mwili kwa kusaidia na misuli, viungo ( jointi) pamoja na macho.

( iv )Mlango wa kuona (jicho) – kwenye macho, kuna vipokea taarifa vya mwanga vinavyoitwa rods na cones.
Rods hutumika kuona kwenye mwanga hafifu. Vitamini A husaidia rods kufanya kazi vizuri. Hivyo, upungufu wa vitamini A husababisha upofu wa usiku (night blindness).
Cones hutumika kuona kwenye mwanga wa kawaida/ mkali.

Huonyesha rangi ya kitu. Kuna aina tatu za cones: zile zinazoona vizuri zaidi rangi nyekundu, zile zinazoona vizuri zaidi rangi ya bluu na zile zinazoona vizuri zaidi rangi ya kijani. Kuna aina mbalimbali za upofu wa rangi, inayojulikana zaidi ni ile ya upofu wa rangi nyekundu na kijani. Mtu mwenye tatizo hili hawezi kutofautisha kati ya rangi ya kijani na nyekundu. Tatizo hili huruthiwa, huwapata zaidi wanaume kuliko wanawake.


Kuchanganyika kwa milango ya fahamu (mixed-up senses): hali hii kwa kitaalamu huitwa synesthesia. Tafsiri na taarifa za milango ya fahamu huwa zimegawanyika. Usishangae kusikia mtu akisema, rangi inanuka bluu, jioni ya leo ni chumvi, ladha ya mandazi ni pembe tatu, tatu ni ya njano, ijumaa ni ya kahawia. Yamkini hata ule msemo wa blue Monday uliotolewa na watu wenye hali hii. Mara nyingi, herufi, namba, au muda huwa wanaziona kwa rangi maalumu. Haijafahamika vizuri hali hii husababishwa na nini.

Ingawa inawezekana husababishwa na kutokukomaa kwa mfumo wa fahamu au umeme wa ubongo kupelekea taarifa mahali ambapo ni tofauti kwenye ubongo wa cerebrum. Hali hii huwa inaridhiwa na huwapata zaidi wanawake.

Kutokana na maelezo hayo hapo juu, yametuonyesha kwamba, mwili wa akili ndiyo kitovu, hivyo ni mwili muhimu zaidi. Kama ni lazima tuwe chochote, basi tulipaswa tuwe mwili huu. Lakini hatuwezi kuwa mwili huu kutokana na sababu tutakazoziona baadaye. Mwili huu ndiyo injini ya maisha yetu ( controlling power) – mind (right thoughts), mouth (right speech) na deed (right actions).

Mwili huu unaunganisha mwili wa hisia na mwili unaoonekana. Unaundwa na mfumo wa fahamu (ubongo na milango ya fahamu) pamoja na urazini wa binadamu. Urazini ni sababu za msingi za kufanya jambo, ni maelezo ya kanuni, misingi au sababu.

Ni utambuzi wa ndani yako na nje yako, fahamu upo, nini kinaenda ndani na nje yako. Unapofanya jambo, jitahidi usiwaze kitu kingine ila zingatia tu unachofanya. Jitahidi akili yako ikae mahali ulipo tu. Usipuuze chochote, usimhukumu mtu yoyote ila kuwa na uadilifu (uwezo wa kujibainisha na mtu).

Usiwe na urazini wa viraka, toa fujo zote zilizomo ndani mwako. Kila siku iambie akili yako kwamba, kila kitu kinawezekana, kila kitu ni ok. Futa neno haiwezekani, siwezi, sitaki, sipendi kwenye akili yako.

Mwili huu hutafsiri maisha kwa kwa kadri ya maarifa uliyopewa na vyanzo mbalimbali. Vyanzo hivyo ni wazazi, walimu, mazingira na uzoefu mbalimbali tuliopitia. Maarifa haya ndiyo ambayo leo hii tunayaita akili, fikra au mawazo yetu. Ukweli ni kwamba sisi tunazo akili. Ukweli wenye kuuma zaidi ni kwamba akili hizo ni za kupewa, hivyo hatuna akili kwa sababu siyo za kwetu, ni za kupewa. Sisi ni maroboti/kasuku wa jamii, wazazi, walezi, walimu, marafiki n.k. Yamkini, maarifa hayo yanaweza kuwa siyo ya kweli na mengine yakawa ya kweli ( jiulize, kila unachokiona ni halisi au kwa sababu uliambiwa?).

Ili mwili huu tuweze kuutumia kwa faida yetu, ni muhimu kuufahamu vizuri. Lakini kuufahamu peke yake haitoshi, bali ni muhimu sana kufahamu umebeba taarifa zipi na za vyanzo gani. Mwili wa akili ndipo mahali palipowekwa sauti na taswira ambazo zinatuambia maisha ni kitu gani, sisi ni nani, kipi kifanyike, wakati gani, wapi au kwenye mazingira gani.

Tulipokuwa wadogo, tuliwekewa maarifa na watu tuliowaamini. Kuna mambo mengi ambayo tuliambiwa lakini siyo ya kweli. Ni ukweli wa kimapokeo, mfano: tusi ni kitu kibaya, kuoa au kuolewa ni kuzuri, kuachwa ni kubaya, thamani zetu zinategemea tuna kitu gani au hatuna nini?

Tukaambiwa pia kwamba - mwanamme hatakiwi kulia, fedha haipatikani mpaka uhenyeke sana, biashara ni za wahindi, wapemba na wachaga, ukoo wetu tumelaaniwa, utajiri ni kwa wale waliozaliwa na matajiri tu, maisha ni uwanja wa vita, ndoa ndoano, kumsaidia mkeo kazi za nyumbani ni utumwa au umepewa limbwata, mafanikio ni kwa wasomi tu. Kwa kuwa tunaamini ukweli huu wa mapokeo, matokeo yake tunashindwa kupata tunachohitaji.

Huna budi kuubadili, siyo wa kweli. Na badala yake, tafuta ukweli halisi. Utaupata wapi? Ukweli halisi inabidi tuutengeneze wenyewe kwani tayari tunao ndani yetu. Hii inawezekana tu kama utabadili mfumo wako wa kufikiri, unavyofikiri ndivyo unavyokuwa. Amini kila kitu kinawezekana, ondoa hofu, kubaliana na hali, kuwa mbunifu, usijali muda, usiogope kuhatarisha n.k.

Mwili huu unasimamiwa na fikra na mawazo. mawazo yetu ndiyo yanayofanya mambo yatokee. Mawazo hayataki kuratibiwa (kuwa displined), yanataka yafanye yanavyotaka yenyewe. Yanakuja yenyewe, huwezi kuyazuia wala kushindana nayo ila unaweza kuyaratibu kwa namna unavyotaka.

Tukutane wakati mwingine kwenye mada ya mwili wa hisia.
Kama kawaida nakaribisha maswali na maoni.


MAJIBU KWA KAMALA!!!!!!!!!!!!!!

Elimu ya utambuzi inapatikana hapa.


Kama nilivyoahidi kumjibu Bwana Kamala, nimeona si vyema kumuacha hewani.
Labda nikumbushe tu kwamba, kwenye makala yangu niliweka wazi kwamba ni vyema kama unataka kuelewa mada ya sisi ni nani, basi utoke kwenye dini kwanza au kwenye kile unachokiamini, hapo ndipo utakapoelewa mada hii vizuri.

Sisi tumefungwa sana na imani za dini, kiasi kwamba hatuwezi kuona kile kilichoko nje ya imani hizo, na kwa kawaida kama unataka kujifunza jambo fulani jipya ni lazima utoke kwanza nje ya hilo jambo au kwenye imani nyingine zinazokufunga ili uweze kujifunza vizuri.

Nikisema hivyo nina maana kwamba, wakati unapojifunza maarifa haya huenda kuna mambo ambayo yatakuwa yanakinzana na imani yako, hivyo utakuwa na wakati mgumu sana wakati unapojifunza kwa sababu utakuwa na mtazamo hasi juu ya maarifa haya, na hiyo haitakusaidia sana.

Sio lazima kujifunza haya maarifa kama unaona hayana maana kwako, lakini kama unaona kuna umuhimu wa kujifunza kitu kipya ili uyaone mambo kwa mkabala tofauti, basi inabidi ukubaliane na mimi kwamba ni vyema ukatoka nje ya kile unachokiamini.

Katika makala zangu zilizotangulia nilieleza vizuri sana, faida ya kujifunza haya maarifa, kwa hiyo sioni sababu ya kurudia tena.Ukweli ni kwamba nisingependa kuzungumzia imani ya wakiristo juu ya Yesu kupaa mbinguni akiwa na mwili, hiyo inahitaji makala inayojitegemea, na ni mada ya baadae sana.

Nilisema nitazungumzia Miili mitatu tuliyonayo sisi wanaadamu na kama ikibidi nitazungumzia mwili wa nne.

Miili niliyoitaja ni hii ifuatayo:

(i) Mwili huu tunao uona, yaani wa mwili wa nyama (Ambao nimeshauzungumzia)

(ii) Mwili wa akili

(iii) Mwili wa hisia

Kama ukijifunza kuhusu hii miili mitatu, na kutenda yale unayofundishwa naamini itakusaidia sana kujifunza mwili wa Roho na na kuuelewa kirahisi zaidi.
Hata hivyo ni vyema nikaweka wazi kwamba mwili wa roho ninaouzungumzia hauhusiani na dini kabisa.

Kuhusu kula nyama, hili nadhani imeelemea zaidi kwenye mambo ya kiafya, mara nyingi tanashauriwa kutokula nyama kutokana na madhara yanayotokana na nyama.
Hata hivyo lazima nitahadharishe kwamba kuna virutubisho muhimu vinavyotokana na nyama, kwa hiyo kama unaamua kutokula nyama basi ni lazime upate virutubisho hivyo kutoka kwenye vyakula vingine mbadala, na kama ikishindikana basi ule nyama kwa kiwango kidogo sana, lakini lazima ufahamu kuwa madhara yako pale pale.


Ikiwa una nia ya kutaka kujifunza maarifa haya kwa undani zaidi, basi unakaribishwa kwenye madarasa yetu.

Maarifa haya yanapatikana pale Kimara Rombo katika jengo moja lililoandikwa “FAJI, ELIMU YA UTAMBUZI INAPATIKANA HAPA”
Ukifika pale utapata majibu yote ya maswali yanayokutatiza.

HOJA ZA MWANBLOG KAMALA!!!!!!!!!

Haya ni maswali ya mwanablog mwenzangu na mtambuzi wa maarifa haya ya utambuzi, ambaye amejitambua na pia kuitambua blog hii kama kitivo cha maarifa haya ya utambuzi.
Nafurahishwa sana na michango yake mbalimbali anayonipa katika kuiboresha blog hii.
Na mimi namuahaidi kuwa mswali yake yote yamepata majibu.

KAMALA...........
asante kwa makala nzuri sisi ni nini? lakini nina swali moja kwako. wakristo wanasema kwamba Yesu kristo alipaa mbinguni akiwa na mwili, je wewe unasemaje? kwa sababu umetuonyesha ni kwa kiasi gani mwili hutegemea vitu vya mavumbini au ardhini yaani mimea nafaka na maji.je tule nyama? mbona inaonekana sisi hatupaswi kula wanyama wenzetu?

Monday, November 24, 2008

Nov 23, 2008

HIVI SISI NI NANI?

Sisi hatutakufa bali miili yetu ndiyo itakayokufa na kuzikwa mavumbini.
Nimekuwa na wakati mgumu kuweka mada zangu za namna ya kufikiri vizuri kwa sababu zimekuwa zikiacha maswali mengi kwa wasomaji wa blog hii ya Utambuzi.
Nadhani nilifanya makosa, kwa sababu tangu mwanzo sikuwahi kuweka msingi wa maarifa haya ya utambuzi kwa kuzungumzia kuwa sisi ni nani.
Kimsingi tukijua sisi ni nani nadhani mada zinazofuata hazitawapa shida wasomaji wablog hii.

Hivi sisi ni nani?

Ni kweli sisi ni hii miili inayoonekana (miili ya nyama)?, au ni majina yetu? Sura zetu? Makabila yetu? Akili zetu? Jinsia zetu? Hasira zetu?
Kwa kutaja hivi vyote, bado swali halijajibiwa.
Sisi tuna miili (inayoonekana), ambayo inatuwezesha kuishi kwenye maisha haya ya duniani, tuna mwili wa hisia, mwili wa akili na mwili wa roho (siyo dini). Kuna wakati mwingine, huwa tunajibainisha na miili minne. Lakini swali bado halijajibiwa.

Mwili unaoonekana:

hivi umeshawahi kujiuliza hata siku moja, ni kwa nini unavaa vizuri, unakula vizuri, unataka kujenga nyumba nzuri, kumiliki mali, kufanya starehe ili kuupa mwili raha au kuwa maarufu. Jibu ni kwamba unataka kuridhika. Ni kweli ukipata vitu hivyo vyote utaridhika? Jibu ni hapana. Je huoni kwamba, hii ni taarifa rasmi kwamba sisi siyo huu mwili?

Hebu tuangalie kwamba sisi tulitokana na nini?
Ulitoka kwa wazazi. Baba alitoa mbegu, ambazo kwa sehemu kubwa ni protini (chakula alacho). Kwa kufanya tendo la ndoa mara moja mwanamme hutoa cc 5 za manii (ujazo wa kijiko kimoja cha chai). Kila cc moja ina mbegu zipatazo milioni 120. Hivyo, cc 5 za manii, zina mbegu zipatazo milioni 600. Kati ya hizi, ni mbegu moja tu inayotakiwa kurutubisha yai ili azaliwe mtoto, ni ajabu eee!

Mbegu moja kati ya mbegu milioni 600. Ni uwiano mbaya sana kama siyo kituko. Kama wewe ni huu mwili, basi una bahati sana, kati ya watu milioni 600 aliowatoa baba ukabahatika wewe peke yako. Mama naye alitoa yai. Kila mwezi hutoa yai moja ambalo likirutubishwa anazaliwa mtoto.

Halafu mama naye hutoa yai moja kila mwezi, kwa mwaka mmoja hutoa mayai 12. kati ya haya ni mangapi hurutubishwa? Kumbuka, mbegu na yai vilitokana na vyakula ambavyo vilioteshwa au kupandwa kwenye udongo wenye rutuba (mbolea) na maji. Maji na mbolea vilitoka wapi? Ni mzunguko usio na mwisho wala mwanzo.

Binadamu hajui hata huo mwanzo halisi wa mwili wake, achilia mbali hisia zake, akili/mawazo yake na roho yake. Ngumu zaidi ni yeye mwenyewe ambaye ndiye mwenye kuitumia miili hiyo.

Dini zote zinasema baada ya kufa watakatifu watakaa milele peponi/mbinguni. Watenda dhambi/waovu watachomwa moto milele au watapelekwa jehanamu. Watu hawa wote (watakatifu na waovu) hawatatumia miili hii tuliyonayo. Watakuwa katika hali nyingine, pengine ni hali ile ile waliyokuwa nayo kabla hawajapata hii miili inayoonekana.

Milele maana yake hakuna mwisho. Kitu chochote kisicho na mwisho hakina mwanzo. Hivyo, binadamu hana mwanzo wala mwisho. Hebu jiulize, mwanzo wa kitu ni kizalisha au kizaliwa? Wewe siyo mwili kama unavyofikiri. Kama unaamini wewe ni mwili, basi una mwanzo na mwisho.

Na kama una mwanzo na mwisho, maisha hayana maana yoyote. Hii ni kwa sababu, dunia ina mamilioni ya miaka, wewe unaishi miaka 70 au 80 kama umejilinda sana. Huu pia ni uwiano mbaya sana- mamilioni ya miaka kwa miaka yako 70. Ni kweli MUNGU aumbe mtu kwa mfano wake, halafu aishi miaka 70, 10, au siku moja ndani ya miaka mamilioni ya dunia? Bila shaka angekuwa kituko.

Lakini pia, dini zinasema, mungu alimuumba binadamu kwa udongo kisha akampulizia pumzi akawa hai. Kuna dini zingine zinasema, sina uhakika kama zote zinasema hivi, wakati wa kuuzika mwili, yule anayeongoza mazishi utamsikia akisema, ulikuwa mavumbi na mavumbini utarudi. Je, wewe ni haya mavumbi (udongo) au ile pumzi aliyoipulizia mungu baada ya kuuumba huu mwili kwa kutumia udongo? Ni swali letu sote. Ili upate jibu, toka nje ya dini kwanza kwani ukiwa ndani hutaweza kupata jibu sahihi, jiulize haya maswali kana kwamba huna dini yoyote. Sisemi uache dini yako, la hasha!!!
Magonjwa: ukiumwa huwa unasemaje? Mwili wangu unauma, mkono wangu unauma, kichwa changu kinauma (changu nani?)
Lakini hata ukifa watu watasema: mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Arusha (mwenye huo mwili ni nani? Yuko wapi?). Kama mtu ni mwembamba, anakula mapochopocho lakini hanenepi, utamsikia akisema, mwili wangu hauna shukrani (wangu nani?).
Kuharibika kwa mimba: hebu jiulize, kwa nini mimba huwa zinaharibika? Unaweza kukadiria, kwa siku moja ni mimba ngapi huwa zinaharibika? Ukienda kumuuliza mtaalamu yoyote wa tiba, atakutajia sababu nyingi sana zinazopelekea mimba kuharibika, ikiwemo ile ya mimba kuharibika yenyewe au kuharibiwa kwa makusudi.

Lakini bado jibu halijajibiwa, kwa nini iharibike yenyewe au iharibiwe? Je kuharibu (kutoa) mimba kuna ubaya gani? Huo ubaya unaouona wewe, unafikiri huyo anayetoa hiyo
mimba anauona pia? Kama hauoni kwa nini?. Ni kweli kilicho kibaya/kizuri kwako na kwa wengine kiko hivyo? Kwa nini?. Jiulize tena.

Hivi kama kusingekuwa na kuharibika au kuharibiwa kwa
mimba dunia ingekuwaje? Bila shaka ingekuwa imemalizika kutokana na wingi wa watu. Nasema hivyo kwa sababu, ukiangalia idadi ya mimba zinazoharibika na zinazoharibiwa kwa siku moja zinaweza kuwa sawa au ni nyingi kuliko idadi ya watoto wanaozaliwa kwa siku moja. Lakini si mimba zote zinaweza kuharibika au kuharibiwa, kuna zingine huharibika kirahisi sana hata kama mwenye nayo ataitunza kama yai, kuna zingine huharibiwa kirahisi sana hata kwa kunywa dose ya kawaida ya dawa au kwa kufanya kazi nzito kidogo, unafikiri ni kwa nini?.

Mfano; mama anaweza akawa anafanya kazi nzito kila siku,
akanywa dawa za kila aina au akatumia kila njia kuharibu mimba aliyonayo ikiwemo ile ya kwenda kwa madaktari lakini mimba isiharibike, unafikiri ni kwa nini? Je, nikikuambia kwamba zile zinazoharibika hazijapata mtu wa kuutumia huo mwili utakubaliana na mimi? Pia nikikuambia kwamba zile zinazokataa kutoka tayari zimeshapata mwenyewe ambaye atautumia huo mwili, utakubaliana na mimi? Kama hukubaliani na mimi, una sababu za msingi za kutokukubali? Ukijiuliza kwa kina, hatimaye utapata jibu.

Jamii inasemaje kuhusu wewe/sisi ni nani?

Mwili ni nini? Je mwili una thamani gani kwetu? Hivi kama mwili ungekuwa na maana sana, ungekimbizwa mochuari na kuhifadhiwa ili usiharibike baada ya mtu kufa? Au ungepakwa asali au kuchomwa sindano ili usiharibike na kuleta usumbufu wa harufu na maradhi?

Mwili siyo mimi wala wewe. Mwili haujawahi kuwa mwenye mwili na hautakuja kuwa. Mwili ni kama tochi tu, ambayo umeiazima tu ili iweze kukusaidia kufika kijiji cha pili, kutokana na giza na njia ya uchochoro ambayo unatakiwa kuipita ili kufika kijiji hicho cha pili.

Mwili ni kifaa na siyo wewe, bali wewe unakitumia kifaa hicho. Binadamu anajibainisha kwenye maisha haya ya hapa duniani kupitia mwili wake, lakini yeye siyo mwili. Mwili ni ubainisho, ni chombo cha kutumika kwa kusudi la kidunia tu.

Baada ya muda mwili hukoma kuwepo, hujimaliza wenyewe au kumalizwa, ili binadamu amudu kuingia hatua nyingine ya maisha ambayo haitumii au haihitaji mwili. Tangu ulipozaliwa umeoneshwa na kufundishwa kwamba, wewe ni mwili kama njia zote.

Akili yako imeshika kutu kwa kuamini kwamba, mwili ni wewe na wewe ni mwili. Huna uwezo tena wa kuuona ukweli, kwa sababu vipimo vyako vyote kuhusu maisha vinaishia kwenye akili, ambayo nayo pia haikuhusu, siyo yako, umepachikwa tu.
Kwa ujinga huu wa kutojua mwili ni nini na sisi ni nani, ndipo ambapo tunaingia kwenye ujinga wa kuendeshwa na miili yetu, hisia zetu na akili. Kila mmoja anaamini kwamba, mwili wake ukipotea, ukishindwa kutumika, yaani akifa, basi huo ndiyo mwisho wake. Kama hiyo ni kweli, ina maana binadamu hana maana kabisa, ni upuuzi usofaa kuelezewa.

Yaani binadamu amekuwepo ili awepo kwa mwezi mmoja, miaka kumi, hamsini, sabini, tisini, au mia tu. Halafu baada ya hapo basi. Huu ni uongo mkubwa sana, unaoweza kukubaliwa na akili makapi ya kulishwa tu;Anayetafakari zaidi kidogo, atabaini kwamba, mwili ni mwili tu ni kasha tu.
Mwili ni kasha ambalo muda wake wa kutumika ukiisha mtumiaji au(wewe) analiacha kwa sababu haliwezi kukidhi kile anachokihitaji hapa duniani. Mtumiaji anachukua kingine ambacho kinakidhi wakati huo(baada ya kifo).

Kwa hiyo, binadamu hafi bali mwili ndiyo unaofikia ukomo wa muda wake wa matumizi kwa sababu mbalimbali. Anapokufa John au Hamisi, haina tofauti. Anapokufa mkulima hohehahe au tajiri kuliko wote duniani, pia haina tofauti. Wote wanapita kwenye hatua muhimu ya mabadiliko, ambapo wanaacha matumizi ya kifaa kilicho kuwa ndicho pekee kinachoweza kuwabainisha na wengine hapa duniani na kuchukua kingine ambacho hakiwezi kuwabainisha tena na wale wenye miili bado.

Anapokufa John au Hamisi, haijalishi kama amezikwa kwa dini jeneza la dhahabu na mizinga 100 au kwa masululu butu na kaniki. Kuzikwa ni utaratibu wa kimazoea wa kuhifadhi mwili ambao sasa ni mzoga tu,ili usisumbue watu wengine kwa harufu na maradhi. Kuzikwa haina maana kwamba, kunambadili aliyekuwa akitumia mwili huo(marehemu), la hasha.

Kama unadhani kwamba Mungu anahesabu umezikwa na dini gani, umezikwa na shehe au padri gani, ndiyo afanye uamuzi wa kukupokea mbinguni hapana, ujue unahitaji msaada wa haraka, kama siyo kupelekwa milembe.Ujue hujui chochote ingawa umekuwa ukijidanganya kwamba unajua. Mungu wa kweli hahangaiki na mzoga, bali sisi kwa ufinyu wetu ndiyo tunaodhani kwamba, mizoga au(maiti) hii ina maana.

Mungu Hayatazami mambo kama Abdallah Juma au John Maiko; Kwani kuzika hasa ni kitu gani. Hatuziki watu ili waende mbinguni. Kama ni hivyo, wanaoliwa na wanyama, kuungua na kuteketea kabisa, wao mbinguni hawatafika? Kama hawafika, watahukumiwa vipi siku ya mwisho? Mwili hautakiwi mbinguni, hauna kazi huko, kwani huko siyo makazi ya miili.

Mwili unafaa tu duniani. Kuna zile jamii ambapo mtu akifa mwili wake huchomwa moto na kuteketezwa kabisa unadhani hizi jamii hazimjui Mungu kama wewe unavyomjua? Zinamjua, tena vizuri zaidi yako. Lakini zimeng’amua kwamba, mwili ni kasha tu, likishindwa kufanya kazi, ni sawa na taka nyingine, hutupwa dampo na kuteketezwa kwa moto.

Mtu akishauacha mwili wake(kufa)hana tena uhusiano na mwili huo. Mtu huyo anakuwa ameingia kwenye awamu nyingine ya maisha ambayo haihitaji mwili na ambayo haihitaji kujua huo mwili.

Naona kwa leo niishie hapa nisije nikawachosha, kwani mada hii ni ndefu kidogo.
Bado nakaribisha maoni na maswali kwa wasomaji.

MAONI YA MUBELWA BANDIO.

Haya ni maoni ya msomaji na mwanablog Mubelwa Bandio.
Hebu soma maoni yake hapa chini.

Hii mara zote ni hatua ya kwanza ya mtu kuelekea aelekeako. Yaani wafanikiwao, wajiuao, wajikwamishao na kotekote yategemea na maamuzi yatokanayo na kujitambua. Lakini pia kuitambua sasa kwa kuwa kama ulikosea ama kukoseshwa katika maisha yaliyopita, bado una nafasi ya kutambua kuwa ulikuwa ukitenda ama kuamua visivyo na sasa unajitambua na kuanza upya.Unajua tuna usukani wa maisha yetu na pasina kujitambua hatutajua tuendako hata kidogo.`Wale wasiojitambua na wenye kuwatambua ama niseme kutambua baadhi ya wengine na wao kutamani kuwa kama wao, huishia kuiga maisha ya kina fulani katika harakati za kujitambua na matokeo yao hujipoteza wao. Kama ambavyo tunaona watu wakifanya ukatili kutaka kudhihirisha kuwa wao ni wababe. Watu wanafanya ubakaji na kuua kutafuta mafanikio ndani mwao. Ndio hayahaya aliyouliza Ziggy Marley kwenye wimbo wake Into the Groove kuwa "why wo loose ourselves just to find who we are?" Ni utambuzi mwema na kila asomaye na ajitambue, atambue aendako kisha kwa pamoja tutaitambua na kuikomboa jamii. Hii ni CHANGAMOTO YETU sote

Nov 22, 2008

KUFIKIRI VIZURI NA NAMNA YA KUJENGA TASWIRA

Niliahidi kuelezea namna ya kufikiri vizuri katika mfulilizo wa makala zangu hizi za maarifa ya utambuzi.
Leo nimeona ni vyema kama nitaimalizia mada hii, ili niweze kuanza mada nyingine.

Njia ya kwanza:

Fikiri vizuri (jenga mfumo wa kufikiri vizuri); mfumo huu uwe endelevu; siyo usubiri upate tatizo ndiyo uanze kufikiri vizuri (usiwe kama zima moto).Hii itakusaidia kuanza kupanda mbegu njema kwenye mawazo yako ya kina ili maisha yako ya baadaye yawe mazuri; yatoe mbegu nzuri/ njema.

Njia ya pili:

Rudisha mawazo yako nyuma, jenga picha yako ya utotoni.Chagua taswira moja wakati ulipokuwa mtoto, jione kimwili, kimavazi na mazingira ulipokuwa (nyumbani /shuleni au popote). Kisha rudi kwako sasa hivi ukiwa mtu mzima; Jione kama ulivyo sasa hivi ukiwa unamtazama huyo mtoto ambaye umemjengea taswira; mtoto ambaye pia ni wewe. Mtazame na zungumza naye, mwambie ulidanganywa kwamba ni mbaya; huna akili, huna thamani, huwezi, hufai n. k; na wewe uliamini kwa sababu ulikuwa mtoto. Lakini sasa umekua; fahamu ukweli halisi kwamba wewe ni mzuri; una akili, una thamani sawa na wengine; unaweza na unafaa. Rudia zoezi hili mara kwa mara; kila wakati hakikisha unachagua eneo ambalo uliambiwa huwezi: Futa imani zote mbaya kwenye mawazo yako ya kina.

Nji ya tatu

Ni ile ya kufanya affirmation (kurudia rudia maneno) pamoja na kujenga taswira (visualization). Mfano: kila wakati jiambie naweza; ninafaa; nina thamani; najiamini. Imani ni muhimu sana wakati unajiambia maneno hayo (amini).

Njia ya nne:

Ni ile ya kutumia mshumaa. Washa mshumaa; uweke mbele yako juu ya meza au stuli au sehemu yoyote. Angalia ile sehemu ya mshumaa inayowaka moto (siyo mshumaa wote) kwa muda wa dakika 10, 30 au zaidi. Baada ya hapo fumba macho, uone ule moto wa mshumaa kwa kutumia macho yako ya akili (jicho la tatu). Utaona moto huo ukiwa wa kijani, bluu, njano au mweupe. Baada ya kuuona, anza kuchoma zile tabia au mambo yanayokukera au kuwakera wengine mfano: choyo, wivu, uzinzi, dharau, zichome moja baada ya nyingine. Wakati unazichoma utaona moto wa mshumaa ukiongezeka ukubwa, au utaona moshi. Fanya zoezi hili mara kwa mara, baada ya muda utashangaa kuona tabia au mambo hayo yamekwisha (umeacha tabia hizo).

Njia ya tano:

Ni ile ya kutumia kioo. Jitazame kwenye kioo ikiwezekana kila siku asubuhi na jioni. Tafuta zile kasoro ambazo uliambiwa na jiambie kwamba huna. Kama uliambiwa wewe ni mbaya; jiambie wewe ni mzuri, huku ukijiangalia bila kujiogopa kwenye kioo. Lakini kama uliambiwa huwezi, jiambie unaweza sana. Pia jikubali kama ulivyo na jiambie umekamilika, unathamani na unastahili.

Njia ya sita:

Ni ile ya kufanya Haipnosia / hypnosis. (Hatutajifunza inafanywa vipi, ni mada inayojitegemea) zile njia tano za mwanzo; tumeona ni njia ambazo unayapa mawazo yako ya kawaida mambo ambayo baada ya kupewa nafasi na muda hatimaye yatachukuliwa na mawazo yako ya kina, mambo haya mapya yataua au kukausha ile miche /miti iliyoota kwenye mawazo yako ya kina; miti hii ni ile ya mambo ambayo yanakukera au kuwakera wengine. Kwa ile ambayo imeshazaa matunda haiwezi kukauka kwani umeshaanza kuvuna (ndiyo maisha unayoishi sasa hivi). Njia hizi zote 5 ni za mzunguko. Hii njia ya sita ya Hypnosis ni ya mkato kwani yenyewe unaenda moja kwa moja kwenye mawazo ya kina na kuyaambia yale unayohitaji - ambayo ni kinyume na yanayokukera.

Nguvu ya uumbaji kitaswira (creative visualization):
kujipa nguvu.

(i ) Kumbuka: imani – hisia – matokeo.

( ii) Programu za zamani kwenye mawazo ya kina ndiyo sababu ya msingi ya kukwama.

( iii )Kuna aina tatu ya uumbaji kitaswira: sauti, kuona na hisia.

( iv )Kila mmoja ana aina yenye kutawala kwake awe anajua au la. Kuna wengine wanatawaliwa na aina mbili. Katika matumizi ya uumbaji kitaswira, tunaanza na aina yetu, baadaye tunajifunza nyingine.

( v )Ili kujua aina yako, jaribu kufikiria unachohitaji sasa hivi ili uone. Mwanzoni unaweza kusikia sauti inayokuambia hutaweza au ni mzaha ufanyao. Unatakiwa ufanye mazoezi mengi ili uweze kujenga uwezo.

( vi ) Mawazo yako ndiyo yenye kukufanya/kukuwezesha ujenge uumbaji kitaswira. Unachokiona kila siku ni matokeo ya kilicho mawazoni kila siku. Hivyo, bila kujua huwa tunaumba yale tusiyoyataka maishani. Uumbaji kitaswira unawakilisha utunzaji wa mbegu (mawazo) kutegemea ni mbegu gani tumepanda.

( vii ) Makosa yajitokezayo sana: usiweke nguvu kwenye kukosa, kwenye usichokitaka na kwenye usichonacho. Mfano: kama umepanga kwenye chumba kimoja na unataka kujenga nyumba yako, usijiambie nimechoka kukaa kwenye haka kakibanda au maisha ya kupanga yamenichosha.

( viii ) Unapokuwa kwenye uumbaji kitaswira, hisi au ona kama vile jambo limeshakuwa tayari.

( x ) Jinsi ya kufanya (hatua):
i.Tafuta mahali tulivu.
ii.Tuliza mawazo yako.
iii.Weka nguvu zako za mawazo katika jambo unalolitaka.

Ni muhimu kufahamu kuhusu makuzi yako kwani yana mchango mkubwa sana kuhusu maisha yako ukubwani.

Nov 20, 2008

ZIJUE CHANGAMOTO ZA KUFIKIRI VIZURI


Kama ulikuwa umepanda mbegu hasi, kufikiri kwako vizuri kutatawaliwa na changamoto, zisikutishe na usishindane nazo,ziache zipite.

Jana usiku nimepokea ujumbe kwenye simu yangu ya mkononi kutoka kwa msomaji wa blog hii.
Msomaji huyo alisema kwamba amefurahishwa sana na ujio wa blog hii ya utambuzi, hapo kabla alikuwa anasoma Gazeti la jitambue ambalo kwake lilikuwa ni kama dawa, kwani kila akikumbana na changamoto za maisha, basi akisoma gazeti la jitambue anapata majibu ya matatizo yake.

Baada ya gazeti hilo kusimama kuchapishwa, amekuwa na wakati mgumu sana, Lakini ujio wa blog hii ya utambuzi umemrejeshea matumaini makubwa, na sasa anaweza kumudu kupambana na changamoto, zozote za maisha zitakazomkabili.

Hata hivyo msomaji huyo alikuja na hoja, anasema kwa muda mrefu amekuwa akijibidisha kufikiri vizuri na pia amekuwa, akivuta anachokitaka akitumia mbinu alizojifunza kupitia katika gazeti la jitambue.
Amekiri kwamba yapo baadhi ya mabadiliko ameyashuhudia kwa kiasi fulani katika maisha yake, ingawa kwa upande wa kufikiri vizuri, zoezi hilo limekuwa gumu sana kwake, kwa sababu ameathirika sana na malezi yake ya utotoni.

Anadai kila akijaribu kufikiri vizuri zinatokea changamoto ambazo zinamtoa kwenye uzingativu hivyo, kuyumba kihisia, kiasi kwamba anatilia mashaka fikra zake, kitu ambacho ni kosa kubwa, katika kanuni hii ya kufikiri vizuri.
Baada ya kumaliza kusoma ujumbe wake niliamua kumpigia simu na kuzungumza nae.

Kufikiri vizuri kuna kanuni zake na kama hukuzifuata kufikiri kwako kutakuwa na walakini. Iwapo maisha yako yatakuwa yamejaa maumivu makubwa kihisia, au hisia zako zilikuwa zimekandamizwa kwa muda mrefu, ni lazima utakuwa unachokozeka kirahisi, kiasi cha kukufanya uwe na hasira za ziada.
Kwa kawaida mtu mwenye hasira za ziada si rahisi kumvumilia mtu au kuvumilia changamoto za maisha.

Ukweli ni kwamba tumechaguliwa kila kitu tulicho nacho katika maisha tunayoishi leo, tumechaguliwa dini za kuabudu, tumechaguliwa taaluma za kusomea, tumechaguliwa aina ya maisha tuanayoishi, tumekuwa sio sisi bali tumekuwa wazazi wetu ndugu zetu au jamii. Utakuta baba anataka uwe yeye, mama nae anataka uwe yeye, shangazi, mjomba, shekh, mchungaji, jirani, rafiki na kila mtu aliyekuzunguka anataka uwe yeye. Sasa wewe ukiwa wao utakuwa na miili mingapi?

Sisemi tusiheshimu maoni ya wazazi wetu, la hasha, bali namaanisha kwamba yapo baadhi ya maamuzi tunapaswa kuamua wenyewe aina ya maisha tunayotaka kuishi. Kwa sababu kila mtu yupo hapa duniani kwa lengo maalum. Tembea dunia yote hii hutakuta mtu yeyote anayefanana na wewe kwa kila kitu, labda sana sana, utasikia “Huyu anafanana na fulani” kwa maana ya kwamba kuna baadhi ya maeneo ameshabihiana na mtu fulani lakini huyo mtu sio yeye.
Kwa hiyo ile kuwa wewe, ni jambo la kujivunia, wewe ni mtu kamili na una umaalum wako, huhitaji kukamilishwa na mtu mwingine

Kimsingi kanuni ya kufikiri vizuri inahitaji mazoezi ya kutosha kwa sababu tumelelewa na kufundishwa kufikiri vibaya, kwa hiyo mawazo yetu yamekandamizwa sana kiasi kwamba hatukuwa na uhuru wa kufikiri tofauti na wazazi wetu.
Kama maisha yako yalitawaliwa na nguvu hasi nyingi, na labda umeshawahi kuwafanyia watu ubaya, kudhulumu au kuwaumiza watu wengine kihisia huko nyuma kutokana na kufikiri kwako vibaya, basi utakuwa umepanda nguvu hasi nyingi ambazo zitakuwa zimekuzunguka.
Kwa kawaida ukipanda nguvu hasi unavuna nguvu hasi, kwani huwezi kupanda mahindi ukavuna mtama, tunavuna kile tulichopanda.

Kwa kuwa ile nguvu hasi inakuwa inakuzunguka, ndio sababu maisha yetu yanakuwa, magumu. Kama mtu umeishi na nguvu hasi kwa muda mrefu, ukiamua kuanza kufikiri vizuri usidhani kuwa ile nguvu hasi uliyopanda kabla hujajitambua itakuacha, ni lazima itaendelea kukuzunguka, kwa hiyo wakati mwingine ukiwa unafikiri vizuri na kujenga uzingativu, nguvu hiyo inaweza ikaja ghafla na kukusomba na hivyo kukutoa kwenye kufikiri kwako vizuri.

Usipokuwa makini, wa kuzipokea changamoto hizo basi hutapata matokeo mazuri, kwa sababu kufikiri kwako vizuri kunategemea na imani uliyonayo juu ya kile unachofikiri na kuamini, kama imani yako ina mashaka, basi na kufikiri kwako kutakuwa hakuna maana.
Kinachotakiwa ni kupokea hizo changamoto, kwa sababu tulizipanda wenyewe kutokana kwamba tulikuwa hatujajitambua.

HE KUMBE HATA WAZUNGU WANAPIGA RAMLI!!!!!!!!!!!


Mimi nilijua mambo haya ni kwa Waafrika tu kumbe hata Wazungu nao huwa wanaenda kwa Sangoma kupiga Ramli!!
Nadhani haya maarifa ya Utambuzi inabidi yasambae mpaka kwa Wazungu!

Nov 19, 2008

JE HAYATI MUNGA TEHENAN ALIWAHI KUSEMAJE KUHUSU FIKRA ZETU? SOMA MOJAWAPO YA MAKALA ZAKE HAPA CHINI.


Kufikiri vizuri kumenifikisha hapa


Makala hii ni miongoni mwa makala za hayati Munga Tehenan, zilizowahi kutoka katika Gazeti la Jitambue. (Gazeti hilo limesimama kuchapishwa kutokana na sababu za kiufundi)

Nimeamua kuirejea makala hii kwa sababu inaelezea mada hii hii ya namna ya kufikiri vizuri, ambayo inaonekana kuwagusa wasomaji wengi.

Kwa kuwa Hayati munga alikuwa ni mwalimu wangu, nitakuwa narejea baadhi ya makala zake pale ambapo nitaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo, nadhani pia itakuwa ni njia moja wapo ya kumuenzi.

Sasa unaweza kuendelea kusoma makala hii:

Ili kufanikiwa kwenye lengo lolote katika maisha, ni lazima uamini kwamba utafanikiwa. Kama usipofanya hivyo, una nafasi kubwa ya kushindwa.
Unaweza kuwa na malengo mapya uliyoyapanga na ambayo unaanza kujaribu kuyatekeleza. Lakini ni lazima ufanye hivyo ukiwa na imani kubwa kwamba utafanikiwa.
Waweza kuona kazi uliyo nayo hivi sasa haikusaidii sana na hivyo kuamua ghafla kuiacha.
Waweza kufanya hivyo huku ukiwa hujaamua kitu gani cha kufanya, na hivyo kulazimika kutumia kipindi cha pengine miezi sita ama hata zaidi inayofuata kujaribu kufikiria nini cha kufanya.

Huwezi kufanikiwa katika kile unachokitaka kufanya ikiwa hutaamua kuyafanya mawazo yako hayo uliyonayo kuwa vitendo. Hata ukiwa na kiu na hamu kubwa kiasi gani ya kufanikiwa, bila kuhamasisha nafsi yako na kuanza kufuatilia lile unalotaka kulifanya, kufanikiwa itakuwa ndoto kwako. Hilo litashusha ari yako na kujikuta unarudi kulekule ulikotoka, kwenye kazi ya kuajiriwa.
Lakini wakati wote huu, vyanzo vya mafanikio huwepo karibu nawe tayari kutumiwa nawe kwa ajili ya kukuletea mafanikio unayoyataka. Lakini bila kuiamini nafsi yako kwamba unaweza kufanikiwa, huwezi kufanikiwa.

Hivyo ni lazima ujifikirie katika mambo unayoyafanya, unafanya mambo yako yanayokuelekeza kwenye malengo yako ukiwa na imani kwamba utafanikiwa. Je, unayo picha ya mafanikio yako akilini mwako na hisia kwamba hivi ndivyo inavyotakiwa kuwa?
Hebu kaa chini na ufikirie kuhusu mambo uliyowahi kuyafanya na ukashindwa katika kipindi cha miaka michache iliyopita. Jiulize ikiwa kweli ulijiamini kwa dhati kwamba utafanikiwa.

Mara nyingi utakuta katika matukio hayo ulikuwa na mashaka ndani yako kuhusiana na uwezo wako wa kufanikiwa na hivyo iko haja ya kujihamasisha kabla ya kuanza kupiga hatua kuelekea kwenye lengo lako. Unatakiwa kuamini kwamba utafanikiwa.
Ni kwa nini imani hiyo ni muhimu kiasi hicho? Kwa kawaida huwa tunaanza kujenga imani tangu tukiwa wadogo. Mara baada ya kuzaliwa kwetu, huanza kujenga au kujengewa imani.
Na baadaye tunaendelea kujijengea imani wakati tukiendelea kukua na huwa tunabadili imani kutoka za zamani na kujenga mpya, kutegemea vitu vingi. Tunahitaji kufanya haya ili kuyafanya maisha yetu hapa duniani yawe rahisi na ya kweli.

Siku zote tunaamini kwamba tunapoamka vitandani mwetu asubuhi, tunahitajika kuweka miguu yetu chini ili kuweza kusimama ardhini kabla ya kuendelea na shughuli zetu nyingine na si kuruka hewani hadi kwenye dari ili kuweza kutoka vyumbani mwetu kwa shughuli zetu za kawaida.
Tumejifunza hili tangu tukiwa wadogo kabisa na sasa hatuna haja hata ya kufikiria kila siku kwamba hivyo ndivyo tunavyotakiwa kufanya. Vivyo hivyo, pia hatuna haja ya kufikiria ni kwa kiasi gani nguvu ya uvutano ina mchango gani katika kusimama kwetu kila asubuhi tangu tunapoamka vitandani mwetu.
Wakati unapofungua mlango wa nyumba yako, unageuza ufunguo wako kuelekea upande uliko ubao wa kufungia mlango ama upande wa tofauti na mwenendo wa mikono ya saa.
Hiyo ni imani tunayojijengea tangu tukiwa watoto wadogo kabisa, tunapoanza kujifunza kufungua na kufunga milango.

Kila unapokutana na mlango mpya hatuwi na wasiwasi kwamba tunajua vile mlango unavyofunguka kwani tunakuwa na hakika (akilini mwetu) na namna mlango huo utakavyofunguka. Tunazunguusha funguo kuelekea upande uliko mlango tu! Ni rahisi. Hiyo ndiyo imani tuliyonayo.
Huoni sababu ya kufikiria uwezekano wa kukutana na mlango unaofunguka vinginevyo. Lakini hakuna atakayekataa kwamba wengi tumewahi kukutana na milango inayofunguka kwa mwelekeo tofauti na ule tunaoamini ndio utaratibu ‘unaokubalika.’ Inaudhi sana unapokutana nao kwa mara ya kwanza.

Hata baada ya mwaka mzima wa kufungua mlango kwa mwelekeo huo, bado imani uliyojijengea kutokana na uzoefu wako kwamba mlango haufunguki kwa mwelekeo huo, utakuwa nayo, na hivyo utakuwa ukikasirika kila mara utakapofungua mlango huo. Imani unayojijengea moja kwa moja huathiri tabia yako, hata kama imani hiyo si sahihi kama unavyofikiria.
Hebu tufikirie kitu kingine! Dunia ni duara ama si duara? Umelijuaje hili? Si kwamba umeambiwa na watu tu? Una uhakika gani? Wapo wanaoamini kwamba dunia ni ya ubapa kutokana na wanavyoiona kila wanapochungulia madirishani.
Kama ungeamini kwamba dunia ni ya ubapa, ni wazi ungepatwa na wasiwasi mkubwa wakati unaposafiri kwenye mashua kwamba huenda mngefika mwisho na kuangukia nje ya dunia.


Lakini hivi ndivyo watu walivyokuwa wakifikiria. Kilikuwa ni kikwazo kikubwa kwa ugunduzi kwa miaka mingi ya mwanzoni. Imani waliyokuwa nayo watu moja kwa moja iliathiri vitendo vyao, na hilo lilikwaza matokeo yao.
Fahamu tena kwamba imani si lazima zioneshe ukweli uliopo duniani. Si kila siku milango hufunguliwa kuelekea mwelekeo uliko mlango.
Imani kuhusu dunia kuwa ubapa ilibadilishwa mara wagunduzi walipoanza kuzunguuka dunia. Imani huathiri moja kwa moja matendo yetu hata hivyo. Wakati mwingine, tunachukua hatua hata imani zetu zinapokuwa si sahihi, na hii yaweza kutukwaza. Hii ni kweli kuhusiana na imani tulizonazo kuhusu nafsi zetu na uwezo wetu.

Vipi kuhusu nafsi zetu? Kama tufanyavyo mambo tuliyoyazoea bila kufikiria kutokana na imani tunazojijengea kama vile kufungua mlango, tunafanya hivyo hivyo kutokana na imani tunazojijengea kuhusu nafsi zetu.
Ikiwa tutajenga imani za kutukwaza kuhusiana na nini kinawezekana kufanikisha, jibu letu litakuwa kukwamisha matokeo ya vitendo vyetu tunavyochukua. Matokeo yake tunakwaza pia matokeo tunayoyapata.

Ikiwa tunaamini kwamba kuna kila uwezekano wa kushindwa katika kile tunachofanyamawazo yetu ya kina (subconscious mind), itafanya kazi ya kujenga mazingira yatakayounga mkono imani yetu hii. Wakati mambo yanapokuwa magumu, hatutakuwa na haja ya kufanya jitihada zaidi iliyo muhimu katika kufanikiwa; kushindwa kwa mara ya kwanza kutaunga mkono imani yetu hiyo na hivyo kutufanya tukate tamaa na kuachana na kile tunachofanya.

Kwa upande mwingine, ikiwa tutaamini kwamba tutafaulu, ni lazima tutafaulu. Mohamed Ali aliyekuwa akifahamika kama mwanamichezo aliyefanikiwa kushinda wote waliowahi kutokea duniani, mbali ya ari aliyokuwa nayo, kipaji na nguvu zake, moja ya sababu kuu zilizomsadia kufanikiwa na kuwa maarufu kiasi alichokuwa ni kwamba alikuwa na imani nzito kuhusiana na kila alichotaka kufanya.

Wengi tumewahi kuona picha zake za televisheni wakati akiwa ulingoni, alipokuwa akidai kwamba yeye ndiye bondia bora kushinda wote waliowahi kutokea duniani. Wakati alipokuwa akiieleza dunia hivi, ni kweli alikuwa bondia bora kushinda wote duniani? Wakati ule hakuwa hivyo, kwani alikuwa bado ana mambo ya kuionesha dunia ili kuthibitisha hilo. Alichokuwa nacho hata hivyo ni kujiamini moja kwa moja katika uwezo wake. Imani hiyo ilithibitishwa na matokeo aliyoyapata licha ya kuvuliwa mkanda wake wa dunia mwaka 1967, baada ya kukataa kwenda kupigana vita Vietnam akiwa askari wa jeshi la Marekani, hakukata tamaa.

Alirudi tena miaka saba baadaye na kushinda ubingwa huo alioendelea kukaa nao kwa miaka minne zaidi. Imani yake kwamba yeye ndiye bora kuliko wote waliowahi kutokea duniani, si kwamba ilimsaidia kufikia kiwango cha juu cha masumbwi, bali kiwango cha juu cha michezo kwa ujumla
This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi