0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Nov 22, 2008

KUFIKIRI VIZURI NA NAMNA YA KUJENGA TASWIRA

Niliahidi kuelezea namna ya kufikiri vizuri katika mfulilizo wa makala zangu hizi za maarifa ya utambuzi.
Leo nimeona ni vyema kama nitaimalizia mada hii, ili niweze kuanza mada nyingine.

Njia ya kwanza:

Fikiri vizuri (jenga mfumo wa kufikiri vizuri); mfumo huu uwe endelevu; siyo usubiri upate tatizo ndiyo uanze kufikiri vizuri (usiwe kama zima moto).Hii itakusaidia kuanza kupanda mbegu njema kwenye mawazo yako ya kina ili maisha yako ya baadaye yawe mazuri; yatoe mbegu nzuri/ njema.

Njia ya pili:

Rudisha mawazo yako nyuma, jenga picha yako ya utotoni.Chagua taswira moja wakati ulipokuwa mtoto, jione kimwili, kimavazi na mazingira ulipokuwa (nyumbani /shuleni au popote). Kisha rudi kwako sasa hivi ukiwa mtu mzima; Jione kama ulivyo sasa hivi ukiwa unamtazama huyo mtoto ambaye umemjengea taswira; mtoto ambaye pia ni wewe. Mtazame na zungumza naye, mwambie ulidanganywa kwamba ni mbaya; huna akili, huna thamani, huwezi, hufai n. k; na wewe uliamini kwa sababu ulikuwa mtoto. Lakini sasa umekua; fahamu ukweli halisi kwamba wewe ni mzuri; una akili, una thamani sawa na wengine; unaweza na unafaa. Rudia zoezi hili mara kwa mara; kila wakati hakikisha unachagua eneo ambalo uliambiwa huwezi: Futa imani zote mbaya kwenye mawazo yako ya kina.

Nji ya tatu

Ni ile ya kufanya affirmation (kurudia rudia maneno) pamoja na kujenga taswira (visualization). Mfano: kila wakati jiambie naweza; ninafaa; nina thamani; najiamini. Imani ni muhimu sana wakati unajiambia maneno hayo (amini).

Njia ya nne:

Ni ile ya kutumia mshumaa. Washa mshumaa; uweke mbele yako juu ya meza au stuli au sehemu yoyote. Angalia ile sehemu ya mshumaa inayowaka moto (siyo mshumaa wote) kwa muda wa dakika 10, 30 au zaidi. Baada ya hapo fumba macho, uone ule moto wa mshumaa kwa kutumia macho yako ya akili (jicho la tatu). Utaona moto huo ukiwa wa kijani, bluu, njano au mweupe. Baada ya kuuona, anza kuchoma zile tabia au mambo yanayokukera au kuwakera wengine mfano: choyo, wivu, uzinzi, dharau, zichome moja baada ya nyingine. Wakati unazichoma utaona moto wa mshumaa ukiongezeka ukubwa, au utaona moshi. Fanya zoezi hili mara kwa mara, baada ya muda utashangaa kuona tabia au mambo hayo yamekwisha (umeacha tabia hizo).

Njia ya tano:

Ni ile ya kutumia kioo. Jitazame kwenye kioo ikiwezekana kila siku asubuhi na jioni. Tafuta zile kasoro ambazo uliambiwa na jiambie kwamba huna. Kama uliambiwa wewe ni mbaya; jiambie wewe ni mzuri, huku ukijiangalia bila kujiogopa kwenye kioo. Lakini kama uliambiwa huwezi, jiambie unaweza sana. Pia jikubali kama ulivyo na jiambie umekamilika, unathamani na unastahili.

Njia ya sita:

Ni ile ya kufanya Haipnosia / hypnosis. (Hatutajifunza inafanywa vipi, ni mada inayojitegemea) zile njia tano za mwanzo; tumeona ni njia ambazo unayapa mawazo yako ya kawaida mambo ambayo baada ya kupewa nafasi na muda hatimaye yatachukuliwa na mawazo yako ya kina, mambo haya mapya yataua au kukausha ile miche /miti iliyoota kwenye mawazo yako ya kina; miti hii ni ile ya mambo ambayo yanakukera au kuwakera wengine. Kwa ile ambayo imeshazaa matunda haiwezi kukauka kwani umeshaanza kuvuna (ndiyo maisha unayoishi sasa hivi). Njia hizi zote 5 ni za mzunguko. Hii njia ya sita ya Hypnosis ni ya mkato kwani yenyewe unaenda moja kwa moja kwenye mawazo ya kina na kuyaambia yale unayohitaji - ambayo ni kinyume na yanayokukera.

Nguvu ya uumbaji kitaswira (creative visualization):
kujipa nguvu.

(i ) Kumbuka: imani – hisia – matokeo.

( ii) Programu za zamani kwenye mawazo ya kina ndiyo sababu ya msingi ya kukwama.

( iii )Kuna aina tatu ya uumbaji kitaswira: sauti, kuona na hisia.

( iv )Kila mmoja ana aina yenye kutawala kwake awe anajua au la. Kuna wengine wanatawaliwa na aina mbili. Katika matumizi ya uumbaji kitaswira, tunaanza na aina yetu, baadaye tunajifunza nyingine.

( v )Ili kujua aina yako, jaribu kufikiria unachohitaji sasa hivi ili uone. Mwanzoni unaweza kusikia sauti inayokuambia hutaweza au ni mzaha ufanyao. Unatakiwa ufanye mazoezi mengi ili uweze kujenga uwezo.

( vi ) Mawazo yako ndiyo yenye kukufanya/kukuwezesha ujenge uumbaji kitaswira. Unachokiona kila siku ni matokeo ya kilicho mawazoni kila siku. Hivyo, bila kujua huwa tunaumba yale tusiyoyataka maishani. Uumbaji kitaswira unawakilisha utunzaji wa mbegu (mawazo) kutegemea ni mbegu gani tumepanda.

( vii ) Makosa yajitokezayo sana: usiweke nguvu kwenye kukosa, kwenye usichokitaka na kwenye usichonacho. Mfano: kama umepanga kwenye chumba kimoja na unataka kujenga nyumba yako, usijiambie nimechoka kukaa kwenye haka kakibanda au maisha ya kupanga yamenichosha.

( viii ) Unapokuwa kwenye uumbaji kitaswira, hisi au ona kama vile jambo limeshakuwa tayari.

( x ) Jinsi ya kufanya (hatua):
i.Tafuta mahali tulivu.
ii.Tuliza mawazo yako.
iii.Weka nguvu zako za mawazo katika jambo unalolitaka.

Ni muhimu kufahamu kuhusu makuzi yako kwani yana mchango mkubwa sana kuhusu maisha yako ukubwani.

1 comment:
Andika Maoni Maoni
  1. Hii mara zote ni hatua ya kwanza ya mtu kuelekea aelekeako. Yaani wafanikiwao, wajiuao, wajikwamishao na kotekote yategemea na maamuzi yatokanayo na kujitambua. Lakini pia kuitambua sasa kwa kuwa kama ulikosea ama kukoseshwa katika maisha yaliyopita, bado una nafasi ya kutambua kuwa ulikuwa ukitenda ama kuamua visivyo na sasa unajitambua na kuanza upya.
    Unajua tuna usukani wa maisha yetu na pasina kujitambua hatutajua tuendako hata kidogo.`Wale wasiojitambua na wenye kuwatambua ama niseme kutambua baadhi ya wengine na wao kutamani kuwa kama wao, huishia kuiga maisha ya kina fulani katika harakati za kujitambua na matokeo yao hujipoteza wao. Kama ambavyo tunaona watu wakifanya ukatili kutaka kudhihirisha kuwa wao ni wababe. Watu wanafanya ubakaji na kuua kutafuta mafanikio ndani mwao. Ndio hayahaya aliyouliza Ziggy Marley kwenye wimbo wake Into the Groove kuwa "why wo loose ourselves just to find who we are?" Ni utambuzi mwema na kila asomaye na ajitambue, atambue aendako kisha kwa pamoja tutaitambua na kuikomboa jamii. Hii ni CHANGAMOTO YETU sote

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi