0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Nov 25, 2009

BINTI ALIYESHANGAZA FAMILIA KWA VISA!

Kalikuwa ni kabinti kazuri
Inaniumiza sana kuikumbuka, hasa kuisimulia, lakini nimeambiwa kuwa, kwa kusema jambo hili wazi, naweza kupata nafuu. Hata hivyo naamini nitapata thawabu kwa kuwasaidia wengine kujua tatizo na kuweza kuliepuka wakimudu.

Mimi na mke wangu tulioana mwaka 1974 jijini Dar es salaam, mimi nikiwa na miaka 32 na yeye akiwa na miaka 24 wkati huo. Mke wangu ni mwenyeji wa Iringa na mimi ni mwenyeji wa Lushoto , mkoani Tanga. Tulikutana hapa dar es salaam, mimi nikiwa mfanyabiashara naye akiwa amemaliza kozi ya ualimu daraja A akisubiri kwenda kufundisha.

Tulianza uhusiano na alipopangiwa kituo cha kazi Kyela, nilimwambia asiende. Alisema ni lazima aende akaonje ualimu ambao aliusomea kwa miaka miwili. Alikwenda, lakini baada ya miezi sita alirudi akidai hawezi. Nilimwomba aache ualimu na kufanya biashara. Tulikubaliana.

Tulioana wakati huohuo na kuanza maisha ya mke na mume. Tulikuwa tukiishi Mburahati wakati huo, ambapo baadae hata hivyo tulihamia Sinza. Tulikaa kwa miaka mitatu bila mke wangu kupata ujauzito. Ndugu walianza maneno na mke wangu alianza kubabaika. Nilimtuliza na kumewambia, angekuja tu kupata ujauzito.

Hadi mwaka 1980 yaani miaka sita baadae, mke wangu alikuwa bado hajapata ujauzito. Ndugu zangu walianza kelele na vurugu za kila aina, wakidai nioe mke mwingine. Nilipuuzia maneno yao, ingawa yalianza kuniingia kidogokidogo.

Mwaka 1981 niliwaza njia ambayo niliona ingesaidia kuondoa kero zote. Nilimwambia mke wangu afunge maguo tumboni na kuonekana kama ana ujauzito. Aliponiuliza sababu , nilimwambia afanye tu hivyo. Alibishabisha awali, lakini nilipomuuliza kama haniamini , aliamua kunikubalia ombi langu.

Alipovaa maguo hayo na kuonekana kama mwenye ujauzito nilianza kutangaza kwamba mke wangu ni mjamzito. Nilitangaza kwa ndugu, jirani na hata kwa jamaa zanguwa karibu. Ilipofika miezi saba baada ya kutangaza hivyo nilimwambia mke wangu ni muda mzuri sasa wa kuaga kwamba anaenda kwao .

Nilikuwa wakati wote huo nahangaika kutafuta namna ya nitakavyoweza kuwezesha kile nilichokuwa nimekibuni. Ni kweli aliondoka kwenda kwao. Wiki ile ile aliyoondoka, nilifanikiwa kupata nilichokuwa nataka.

Nilikuwa nimezungumza na wahusika wengi sana wa maeneo mbalimbali ambao wangeweza kunipatia mtoto mchanga. Mama mmoja ambaye naomba nisimtaje jina alipata mtoto mchanga.

Mtoto huyo alikuwa amezaliwa hospitalini {naomba nisiitaje} na mama yake akafariki. Hakutokea mtu kumdai mtoto, wala maiti ya mama yake na huyo mama alijifanya ni ndugu wa marehemu, mara tu alipofariki. Kwa kutumia fedha kidogo nilizokuwa nimempa aliruhusiwa kuchukuwa mtoto yule akamlee. Ukweli ni kwamba hakuna ndugu wa yule msichana aliyejitokeza hapo hospitalini………….


Kwa kusindikizana na mama huyu, tulisafiri kwenda Iringa kwa mke wangu. Mke wangu hakuwa ameenda kuishi kijijini bali alikuwa akikaa hotelini, pale Iringa mjini. Tulipofika pale hotelini, nilimkabidhi mke wangu kachanga kale nakusema ni kake kuanzia wakati ule. Kalikuwa ni katoto ka kike kazuri.

Kwa mara ya kwanza mke wangu alijua mpango wangu. Ilibidi niondoke na mke wangu kwenda naye kijijini kwao, ambapo tulipofika tuliwaambia alikuwa amejifungua njiani. Nilimwacha kule na kurudi Dar es salaam, kutangaza kwamba mke wangu amejifungua mtoto wa kike. Siwezi kusema furaha iliyokuwepo kwa ndugu zanguna wa mke wangu. Tukawa wanandoa wenye mtoto mmoja kwa njia hiyo.

Mwaka 1987 ndipo tulipoanza kushangazwa na binti huyu, akiwa na miaka sita wakati huo. Kwanza, alikuwa ni binti mkatili sana, tangu akiwa mdogo tu wa miaka mitatu. Alikuwa anapenda sana kukwangua wengine tukiwemo sisi. alipoanza kuzungumza, alikuwa akizungumza maneno ya ajabu, lakini ya kutisha pia.

Mara nyingi alikuwa akipenda sana kutaja kufa, kuumwa na nyoka, kupanda mlimani, kufukiwa gizani na mengine ya aina hiyo. Alikuwa akipenda sana kusikiliza kwa makini watu wanapokuwa wakizungumzia mambo ya uasi kuliko mambo mazuri. Hii tabia tuliigundua alipokuwa na miaka mitano.

Akiwa na miaka sita, tukio la kwanza lililotushtua ni lile la kumwambia mama yake, hana adabu, alimwambia hivyo kufuatia kumwambia , akinywa chai awe anaondoa kikombe chake mezani na kukipeleka jikoni. Mama yake alimchapa. Kwa kawaida mtoto wa miaka sita akichapwa, mtu anategema akiona akilia. Huyu hakulia, bali alimwangalia tu mama yake vibaya na kuondoka.

Siyo siri, niliogopa sana. Mwaka 1994 alipokuwa darasa la saba alifanya vituko vingi sana na tulihangaika sana kutafuta suluhu. Ili kupunuza maumivu, tuliamua kumpeleka shule ya sekondari ya bweni mikoani. Tulimpeleka. Lakini hata mwezi haukuisha alikuwa amerudishwa kutokana na kushindikana.

Alikuwa na kila aina ya visa. Alikuwa akitukana waalimu,kupiga wanafunzi wenziena kuanzisha vurugu za aina mbalimbali. Ajabu ni kwamba, ukiwa umekaa naye na kuzungumza naye, anakuwa mtoto mzuri na msikivu sana. Anaweza hata kulia, kujutia makosa yake. Lakini baada ya hapo ndio anakuwa ametiwa moto.
FUATILIA KISA HIKI KESHO...............

6 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. Kisa kinasisimua na kusikitisha. Kwa kifupi naweza kusema mume labda alifanya kosa kuwasikiliza ndugu zake. ngoja nisubiri kesho nisome mwendelezo kwanza isije nikaharibu hapa.

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. Mmm!mbona inatisha,mtoto wa miujiza hasa!ngoja tusubiri part 2.

    ReplyDelete
  4. Kama hamku adapt jini sijui, poleni sana lakini

    ReplyDelete
  5. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!Friday, November 27, 2009

    yasinta, wewe unawasikiliza akina nani?

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi