Alikuwa ni mama!
Ø Amtazama mtoto na kusema bila mabadiliko atakufa mtu
Ø Awabadilikia mume na binamu zake dakika chache baada ya ndoa
Ø Atangaza kwa mtoto kwamba yeye ni mama aliyekufa zamani amerudi
Nina uhakika kuhusu watoto wanaoteswa na wazazi wao, wanavyojisikia. Nina uhakika kwa sababu, niliwahi kutokea kuwa mmoja kati ya hao. Lakini pia najua kuhusu watoto wanaoteswa na hata kudhuriwa na kimaisha na mama zao wa kambo. Hapa kwenye hili sitaki kusema chochote kwa sasa.
Kwa jina naitwa Almasi Halifa Nimetimiza miaka 49 kamili Julai mwaka huu, 2009. Nilizaliwa Kilosa ambako baba yangu alikuwa mwalimu wa shule ya msingi. Nikiwa na miaka minne hapo hapo Kilosa kwenye kitongoji cha Ulaya, mama yangu mzazi alifariki wakati akijifungua. Bahati mbaya zaidi ni kwamba alifariki yeye na mtoto wake, ambaye angekuwa ndiye mdogo wangu pekee.
Baada ya mama kufariki, baba aliomba uhamisho kwa imani kwamba, kifo cha mkewe kiliwa ni mono wa mtu. Alipewa uhamisho na kupelekwa sehemu inayoitwa Wami Dakawa humohumo mkoani Morogoro. Nikiwa na miaka minane, baba aliamua kuacha kazi. Wakati huo, kwa mujibu wa kumbukumbu zangu alikuwa kama amechanganyikiwa kidogo.
Nasema alikuwa kama amechanganyikiwa kwa sababu alikuwa ni mkali sana, mkatili, na anayeonesha kabisa kwamba, hakuwa na amani na nafsi yake. Pamoja na kwamba likuwa ni mwalimu {Kabla hajaamua kuacha kazi} Mimi mwanaye nilianza shule nikiwa na miaka minane baada ya kuhamia Dakawa. Tema huko akuanza shule kulitokana na shinikizo la wenzake.
Ukweli ni kwamba tangu kifo cha mama yangu, baba yangu alikuwa kama adui yangu. Nikiwa na miaka mitano alikuwa akiniachia kazi kama kupika mboga, hasa maharage na nyingine zenye kuhitaji kukagua maji tu. Nilifanya kazi hizo na kuna wakati nilikuwa nakosea.
Nikiwa na miaka mitano nilikuwa napigwa sdana kwa makosa ambayo hata mtu wa miaka 15 asingekwepa kuyatenda. Nilikuwa nashinda na kulala na njaa wakati mwingine. Kuna wakati ba aalikuwa anaondoka na kwenda kushinda kwenye kaduka kake kalikokuwa karibu na eneo la sabasaba, bila kuacha chochote. Sisi tulikuwa tukiishi mji mpya.
Nilikuwa nashinda na njaa au kulala na njaa kwa sababu alikuwa akiondoka asubuhi akiwa amesahau au kufanya kusudi bila kuacha chochote na alikuwa akichelewa sana kurudi. Hakuwa mlevi, lakini sijui alikuwa akipotelea wapi.
Kulikuwa na watoto jirani tuliokuwa tukisoma wote, ambao nadhani walikuwa wamewaambia wazazi wao kuhusu maisha yangu. Kwani wazazi wao waliwaambia waniambie niwe naenda kule nyumbani kwaokama kujisomea kidogo. Lakini nilijua walikuwa walikuwa wakitaka niende hapo kwa ajili ya kula.
Hii ilinisaidai kidogo kwa sababu, hata kama nisingekunywa chai asubuhi, kwa kuwa shule tulikuwa tukila buruga {aina ya uji wa njano}, nilijua jioni ningepata chakula cha kwa rafiki zangu. Sijui hata hivyo ilitokeaje,kwani baba alijua nakula ile nyumba ya jirani. Kwa kweli nilipigwa sana siku hiyo na alikwenda pel kuwatukana wale wasamaria wema.
Nilianza tena maisha ya mateso na shida. Lakini wale wenzangu walikuwa wakiniambia kwamba, nivumilie kwani nitakuwa mkubwa na nitalipiza kwa baba. Wakati nikiwa darasa la tatu walikuja ndugu zake babawawili kuishi nasi. Mmoja biamu yake na mwingine ndugu wa huyo binamu. Walikuwa bado vijanawadogo tu , hawakuwa wanzidi miaka 20.
Sasa hapo mateso yalikuwa makubwa sana. Hawa jamaa walikuwa wanafanya makosa na kunisingizia mimi. Walikuwa wakiiba fedha za baba, walikuwa wakiharibu vitu na nilikuwa nasingiziwa mimi. Nilikuwa napigwa sana. Hawa ndugu zake baba nao walikuwa wakinipiga sana bila makosa.
Walikuwa wakijitahidi sana kuninyima chakula na mambo ya namna hiyo. Nikiwa hilohilo datrasa la tatu niliamua kuacha shule. Sikuona sababu ya kusoma, na nilijua nisingemudu tena. Nilikuwa nikienda karibu na kiwanda cha tumbaku, eneo ambalo linaitwa Tumbaku kufanya vibarua. Kwa mwaka mzima sikuhudhuria shule na nnilianza kweli kuwa mtundu.
Huko nilianza hata kujifunza kuvuta bangi, ingawa mara chachechache. Nilijifunza kuchungulia wanawake wanaooga hapo karibu na kiwanda, kama walivyokuwa wakifanya wakubwa. Baba hakuwa akijua kwamba nilikuw siendi shule na pengine hata angejua asingejali , kama angejali ingakuwa ni kwa kunitimua hapo nyumbani tu labda.
Asubuhi nilikuwa na sare za shule na huku nikiwa na nguop za kazi kwenye mfuko wangu wa madaftari. Jioni, nilikuwa narudi kama vile nimetoka shule. Wale ndugu zake baba waligundua kwamba, nilikuwa sijali kuhusu chakula chaona nilikuwa nawajibuhovyo, hivyo walinikomoa. Walimwambia baba kuwa nakula kwa jirani na eti nimesema baba anamalizia fedha zake kwa wanawake.
Nadhani ujumbe waliotaka kumpa ndugu yao, yaani baba, bali wakaona ingekuwa salama kwao kuupitishia kwangu. Siku hiyo nilipigwa hadi jirani ikabidi waingilie kati. Baba alinitukana sana, hasa kwa kunisimanga kuhusu mama yangu kufa.
Nilitahayari sana na ilibidi nimwambie kwamba, kama yeye ana akili mbona ni masikini. Sijui hata nilifikiria nini kusema hivyo. Niliamua sasa kwamba sijali. Nilikuwa natoka asubuhi bila sare za shule bali na nguo zangu za kawaida na kwenda kibaruani. Nilikuwa nimekata tamaa bila shaka.

FUATILIA MKASA HUU WA KUSIKITISHA KESHO..........
Tuko pamoja hiyo kesho Kaka.
ReplyDeleteInasikitisha lakini inafunza pia.
Kuna mambo kadhaa ambayo kwa aliyesoma mpaka hapa anaweza kuwa amejifunza. Naamini kesho tutaendelea kujuvyana mengi kuhusu mkasa huu.
Asante kwa UELIMISHAJI huu
Blessings
Wakati naanza kusoma nimelengwalengwa na machozi inasikitisha lakini inafunza. Nasubiri mwendelezo.
ReplyDelete