Mpaka miaka ya hivi karibuni mambo ya uchumba yalikuwa hayawezi kufanyika bila ya kuwepo wazazi na familia. Mitoko mingi na kualikana ilifanyika majumbani wakiwapo wanafamilia wote. Kujitokeza kwa usafiri na ugunduzi wa magari kumesaidia sana kuharibu utaratibu mzuri wa mitoko ya kimapenzi na uchumba kwa ujumla.
Magari si tu kwamba yamesababisha mitoko isifanyike majumbani, lakini pia yamesababisha ifanyike bila kuwashirikisha wazazi. Gari siku hizi limebadilishwa kuwa kitanda kinachotembea chakufanyia ngono wakati wa mitoko.Vijana wadogo sio kwa hapa nchini tu bali hata huko katika nchi za magharibi na ulaya wamejinyakulia uhuru mkubwa mno kutoka kwa wazazi wao, na kuzipondoponda chini mila na desturi ambazo ziliweka misingi imara katika kulinda maadili ya uchumba kwa vijana.
Lakini pia Teknolojia mpya na matumizi yake mabaya nayo imechangia kwa kiasi kikubwa kusambaratisha mila na desturi zetu zilizokuwa zikilinda maadili yetu. Simu na mitandao ya mawasilano, ni moja ya mabadiliko yaliyotufikisha hapa.
Hafla na matamasha ya usiku nalo ni balaa jingine kwa watoto wetu wa kike na wa kiume. Ndani ya matamasha haya kuna tabia zizsizofaa za ulevi na uvutaji bangi pamoja na matumizi ya dawa za kulevya. Kwa watoto wetu wenye umri wa ubarubaru ni rahisi kuingia kwenye matumizi vileo au uvutaji bangi na pengine matumizi ya dawa za kulevya kwa sababu umri huo unaambatana na ushawishi wa kutaka kujaribu kila kitu.
Siku hizi vijana wamekuwa wakishawishiwa kutumia vileo au dawa za kulevya ili iwe rahisi kushawishiwa kuingia kwenye itendo vya ngono au kubakwa na kama wakikataa wanweza kuwekewa dawa hizo kwenye vinywaji vyao baridi ili iwe rahisi kwao kubakwa.
Lakini pia mitandao ya kijamii na matumizi yake mabaya yamesababisha mabadiliko makubwa ya kingono na mahusiano kwa vijana na hivi sasa hata watoto wa kiume ambao waliachiwa huria huku watoto wa kike pekee wakilindwa dhidi ya vitendo vitakavyowaingiza kwenye ngono za mapema au kubakwa, hivi sasa hata watoto wa kiume si salama tena, na siyo kwa sababu ya kuingia kwenye vitendo vya ngono za mapema na watoto wenzao wa kile la hasha bali kuingia kwenye mahusiano ya jinsia moja yaani kulawitiwa na watu wazima au watoto wenzao.
Je tunawezaje
kukabiliana na changamoto hizi?
No comments:
Andika Maoni Maoni