0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Mar 15, 2016

Je inakuwaje wanawake wasiotulia huopoa wanaume wenye muafaka...?


Kuna jambo moja huwa linawaacha wanawake wengi na maswali yasiyo na majibu na wengi huwa wanajiuliza maswali bila ya kupata majibu.

Kuna baadhi wanawake ambao hawajatulia, vijana wa mjini huwa wanawaita "utulivu ziro" yaani sio kwamba ni makahaba, hapana, lakini wanakuwa na tabia ya kutotulia na kuonekana kama wana vurugu kichwani. Kwa wanawake wengi huwa wanawaona wanawake wa aina hii kama sio wife material, yaani hawako katika kundi la wanawake wanaofaa kuolewa kutokana na tabia zao hizo za kutotulia.

[​IMG]
Lakini jambo ambalo huwa linawaacha wanawawake wengi na mwaswali ni pale wanapowaona wanawake wa aina hii wakiopoa wanaume wenye muafaka, yaani wanaume wenye sifa zinazowavutia wanawawake wengi kuolewa nao. Hapo ndipo yanapoibuka maswali mengi kwa baadhi ya wanawake wakijiuliza.

"Ni kitu gani kimemvutia huyu mwanaume kwa mwanamke yule.....!"

[​IMG]

Lakini jambo la kushangaza zaidi ni kwamba uhusiano wao unaweza kukua hadi kufikia kufunga ndoa, na usije ukadhani kwamba yule mwanamke atabadilika tabia, la hasha, anaweza kubaki na tabia yake hiyo hiyo ya kutotulia na bado akamudu kumshika huyo mwanaume barabara. Mwanaume huyo anaweza kujikuta amenasa na hawezi kuchomoka, na hata ikitokea wakitengana, haitapita muda wararudiana pamoja na uhusiano wao kutawaliwa na vurugu fulani fulani.

[​IMG]

Wapo baadhi huwa wanabadilika na kujenga uhusiano imara hata kuwashanganza watu wengi, lakini huwa ni wachache sana, narudia kusema, mara nyingi huwa ni wachache sana, lakini wengi wao pamoja na kutotulia na kuonekana kuwa na vurugu kichwani, lakini humudu kuwashika wanaume wenye muafaka na kuwaacha wanawake wenzao vinywa wazi.

Je ni jambo gani linatokea?Ukweli wa jambo hili umegawanyika sehemu mbili:

Mosi: Wanaume wengi watulivu, wapole, yaani wale wanaoitwa "husband material" ni watu ambao huwa hawana mbinu wala guts za ku approach na kuwapata wasichana wanaofanana nao i.e watulivu, wapole na wanaoitwa "wife material"! Hii inatokana na ukweli kwamba wanaume wapole huwa pia wana aibu na ni waoga sana wa kutongoza! Upande wa pili, wanawake watulivu huwa ni waoga na wagumu sana kupatikana.. meaning unatakiwa uwe na mbinu za ziada kuweza kuwapata. Hili ni tatizo la kwanza ........................................................................................

Pili: Wanawake wengi "utulivu ziro" wanawafahamu wanaume ambao ni "husband material", na wanafahamu kwamba ni waoga, na wana aibu. Wanawake hawa hutumia ujanja wao wa mjini kujisogeza karibu na wanaume hawa (kitu ambacho wanawake wapole hawathubutu kufanya kwa kuogopa "nitaonekanaje?") na kuanzisha nao mahusiano pole pole huku wakijua kabisa kwamba wanaume hawa wakishanasa watafanya kila liwezekanalo kuhakikisha hawajinasui! ...................................... 

 Matokeo yake sasa.. utakuta wanaume wapole, watulivu, wakioa wanawake utulivu sifuri huku wanawake wapole, watulivu wakichukuliwa na wanaume utulivu sifuri ambao ndio hasa wenye mbinu na uthubutu wa kuwafata na kuwatongoza..!

No comments:
Andika Maoni Maoni

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi