0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Dec 23, 2008

MWANZO WA BINADAMU, MASWALI NI MENGI KULIKO MAJIBU. JE UKWELI NI UPI?

Kama nilivyosema wakati nafungua huu mjadala kuwa nadharia ya uwepo wa binadamu imejaa utata mtupu.
Katika dini tulifundishwa kwamba binadamu wa kwanza kuumbwa alikuwa Adam na Eva, na nilipokuwa shule, napo nilifundishwa kuwa chanzo cha binadamu ni nyani, halafu akawa anabadilika hadi kufikia kuwa binadamu.

Lakini bado kuna Maswali najiuliza, hivi ni kwa nini, nyani wengine wamegoma kubadilika hadi leo? Yaani wamebaki kuwa nyani badala ya binadamu.
Je na sisi kwa nini tumesita kuendelea kubadilika?

Kama tulikuwa kama nyani, halafu tukabadilika na kuwa binadamu, inakuwaje tusiendelee kubadilika zaidi na zaidi? Au kulikuwa na mipaka ya kwamba tukifikia mabadiliko kama haya tuliyonayo iwe ndio basi?

Kama ingekuwa binadamu aliumbwa kama nyani na kubadilika kufuatana na mazingira labda na mambo mengine, mbona basi leo hii uhusiano wa kinasaba kati ya binadamu na nyani sio mkubwa kama ule uliopo kati ya binadamu na panya weupe?
Yaani wale panya niliowaeleza awali katika makala iliyopita kuwa ndio wanotumika kufanyia utafiti masuala mengi yenye kumgusa binadamu, kwani kinasaba panya hawa wanakaribiana na binadamu.

Basi kuna haja ya kuamini kwamba binadamu wa kwanza alikuwa ni panya kisha akabadilika na kuwa kama alivyo leo.
Lakini bado najiuliza kwa nini huyu panya asiendelee kubadilika, amefungwa na kitu gani?


Hivi karibuni wakati naperuzi peruzi katika mtandao nimekutana na mijadala mikali kuhusu asili ya viumbe hai.
Kwa mfano nchini Marekani mjadala huu umeingia mashuleni ukiwa na nguvu mpya, kutokana na vijana wengi nchini humo kupambazukiwa na kukataa kukaririshwa elimu za wanasayansi wa kale zisizo na mashiko.

Vitabu vingi vya Baiolojia vilikuwa vikisema kwamba asili ya viumbe hai ni mwendelezo wa mabadiliko (Evolution)
Walimu wengi wa nchini Marekani na Ulaya ambako jambo hili limeshika nguvu wanapinga nadharia hii ya mabadiliko na wanaamini kwamba viumbe hai viliumbwa na kitu, jambo au nguvu yenye akili.
Wataalamu wa mabadiliko nao wanapinga na kusisitiza kwamba nadharia yao ni ya kisayansi na ya wale wanaopinga ni ya kidini.

Hivi sasa hata wale waumini wa nadharia ya mabadiliko iliyoasisiwa na Charles Darwin wameanza kuitilia mashaka nadharia hiyo kiasi cha kuitupilia mbali ili kutafuta nadharia mbadala.

Kwa mfano, Mwanabaiolojia mashuhuri kutoka nchini Sweden, Sren Lvtrup, ameweka wazi kwamba, anaamini siku moja nadharia hii ya Darwin ya mabadiliko itakuja kuwekwa wazi kwamba ni nadharia ya uongo kupita kiasi katika historia ya sayansi.

Lakini Nadharia hii ya mabadiliko inaendelea kufundishwa katika mashule yetu ambayo yanahudumiwa na kodi za walalahoi, huku nadharia hii ikiendelea kutiliwa mashaka kila uchao.

Kwa kuwa nadharia ya kidini ina msimamo wake tofauti na ule wa sayansi, sasa kwa nini wanafunzi wasifundishwe nadharia zote mbili, kila moja ikiwa na ushahidi wake ili waweze kupembua ubora na udhaifu wa kila nadharia na kuwawezesha kwa ridhaa yao wenyewe kuamua nadharia ipi kati ya hizo mbili ina ushahidi bora kuzidi nadharia nyingine?

Bado napata kizunguzungu katika kujadili hii mada, kwani kila ninavyozidi kutafuta ukweli nakutana na nadharia zinazopingana, ingawa kila moja haitoi ushahidi unaojitosheleza.

Je wenzangu mnayo maoni gani juu ya hili?

Nahisi mada hii inaelekea kunishinda, naomba msaada wenu.

6 comments:
Andika Maoni Maoni
 1. sasa hii ya kidini natuwaachie wenye imani zao kwa sababu kiimani hupaswi kuuliza maswali. ni sharti upokeee kila kitu kama ulivyoambiwa na kukiamini vinginevyo utakufuru.

  kuhusu binadamu kuwa nyani, ina mantiki kidogo. historia inaonyesha binadamu wa kale aliishi juu ya miti na mapangoni. sio lazima awe nyani lakini kwa kuhushi polini na juu ya miti ni sawa na nyani. mpaka alipovumbua moto ndo akahamia chini na kuanza kujenga vibanda na kula chakula kilichochomwa badala ya kibichi kama cha nyani.

  akagundua nyumba na upuuzi mwingine tulionao leo. hii inaonyesha ni kwa kiasi gani suala la nyani lilnaingia akilini kidogo kwamba hata kama hakuwa nyani lakini maisha yake yalifanana sana na yale ya nyani.

  kubadilika kwa ngozi na mwili kunaendelea. kutokana na ugunduzi wa kisayansi, binadamu anazidi kuwa mayai mno. ukiwaangalia wazee wazamani walivyopekua bila kudhulika, wewe huwezi, unhaitaji viau. watu wa kale walikuwa na manyoya ya kuzuia baridi, sisi tuna sweta na bila sweta twafa maanake tumebadilika na labda tunaendelea kubadilika. naishia hapo kwa leo.

  ReplyDelete
 2. Subiri naja. Ntatoa maoni baadae. Wacha nika-charge akili maana mengine si ya kukurupukia.
  Blessings

  ReplyDelete
 3. Nipo natafakari!
  Na naanza kuwachumnguza binadamu wote waishio karibu na nyani waishipo kama wanajua kuongea vizuri!:-)

  Kufundisha asili ya binadamu kusije tu kukasababisha sisi tuabuduye mbuyu na kudhani binadamu alikuwa panzi na baada ya kufa atageuka au kuzaliwa kama mjusi ndio maana uzito wa dunia hauongezeki kwa sababu Saddam Husein Kafa na simba kajifungua, TUSITENGWE tu kimtazamo.

  ReplyDelete
 4. Kazi kweli kweli, nimepita fasta fasta. Naenda sugua kichwa kaka!

  ReplyDelete
 5. Sayansi (ambayo sasa hivi inaunga mkono mawazo ya Darwin) inaamini kuwa mabadiliko ndiyo yaliyowafanya viumbe wawe hivi tunaowaona leo. Na mabadiliko haya yanaendelea hata kama hatuyaoni.

  Ni hivi: kwa kadiri ya kanuni ya natural selection, mabadiliko katika mazingira husababisha mwitikio fulani katika kundi la viumbe. Mwitikio huo hutofautiana kati ya kiumbe mmoja na mwingine kutokana na tofauti za kinasaba baina yao.

  Mabadiliko haya huchukua miaka kwa mamilioni ili kuyapima. Kwa kuwa hakuna binadamu anayeweza kuishi miaka hiyo kushuhudia mabadiliko hayo, ndio maana kuna ushahidi unatumika kuelezea haya kwa mfano mabaki ya viumbe yaitwayo fissils vilevile ushahidi wa kimazingira kwa kutazama uhusiano wa kinasaba kati ya kiumbe mmoja na mwingine.

  Suala la binadamu na nyani, sikubaliani nalo, lakini pia maelezo yake yanashawishi. Ilivyo ni kwamba nyani na binadamu walikuwa jamii moja (si kiumbe mmoja). Ni mabadiliko ndiyo yaliwafanya watokezee tofauti tunazoziona hivi leo ambazo hata hivyo si kubwa. Na mabadiliko haya yanaendelea japo hatuyaoni. Huko mbeleni binadamu atabadilika kuwa kiumbe mwingine kabisa kama ambavyo na nyani atabadilika kuwa kiumbe mwingine. Sababu ni kwamba mabadiliko yanaendelea.

  Nikuulizeni swali: Unafikiri kwa nini tuna vidole vitano vinavyotofautina urefu? Kwa nini kile cha mwisho kiwe kifupi? Je, tutakosea tukiamini kuwa baadae (miaka mingi ijayo) kile kidogo kitapotea? Changamoto.

  Kuhusu panya. Panya na Nyani kwa hakika ukaribu wao unatofautiana sana. Binadamu, kisayansi yu karibu zaidi na nyani kuliko panya. Ukichunguza DNA utaona kuwa zile za binadamu zinafanana zaidi na nyani kuliko ilivyo kwa panya.

  Kwa nini panya anatumika zaidi, nadhani ni kwa sababu anapatikana zaidi kuliko nyani. Na udhibiti wa nyani maabara ni mgumu kuliko ule wa panya. Lakini pia, pamoja na kwamba panya hatuko naye karibu kama nyani, lakini tuko nae kundi moja kwa maana ya sifa za jumla jumla. Mifumo yote ya ndani ya miili yetu inafanana. Mmeng'enyo. Umpuaji. Uzazi. Ufahamu. Na kadhalika. Kwa hiyo ndio maana anatumiwa zaidi katika sayansi.

  Je, nadharia ya Darwin isifundishwe? Nadhani ifundishwe kwa sababu inashawishi japo kama nilivyokuwa nikiandika kwenye makala alizozinukuu mwandishi wa makala hii, zinaongozwa zaidi na imani, yaani hazijipambanui wazi wazi na dini/imani. Na kwangu mimi huu ni udhaifu mkubwa wa nadharia hii.

  Nadhani kuna haja ya kuurekebisha mfumo wetu wa elimu ili elimu iwe na kusudi la kumjengea mwanafunzi uwezo wa kuhoji kila nadharia anayokutana nayo. Jambo ambalo nina hakika halipo kwenye mfumo wetu hivi sasa. Vinginevyo, walimu wetu hawataelewa wanafundisha nini na hivyo kitakachobaki ni kuwakaririsha wanafunzi nadharia ambazo hata wao hawakuzielewa walipokuwa wakifundishwa na wahadhiri wao.

  Nasubiri maoni ya wengine tupate changamoto zaidi.

  ReplyDelete
 6. Mmmm! Wanasayansi wanatuchanganya sana na tatizo wapo wengi sana sasa sijuw tumwamini nani tumwache nani

  ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi