0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Dec 26, 2008

MWANZO WA BINADAMU. BADO NATAFUTA MAJIBU........

Bado naendelea kupata changamoto, awali nilitaka niachane na hii mada kwa sababu kwa jinsi ninavyozidi kutafuta majibu ndivyo ninavyozidi kupata maswali mengine.

Haya sasa, Rafiki yangu Bwaya naye kaja na changamoto nyingine.


Hapa inabidi nitulie kidogo.

Ukweli ni kwamba namuheshimu sana huyu bwana, kwani mjadala huu niliuanzisha kutokana na makala zake ambazo kama mnakumbuka niliwahi kuziunganisha katika makala yangu ya kwanza wakati naanzisha mjadala huu.

Wako baadhi ya wasomaji wangu ambao hawakunielewa kwa kudhani kuwa napinga hoja za bwana Bwaya, labda niweke wazi kwamba sikuwa na msimamo unaotofautiana sana na yeye, bali lengo langu lilikuwa ni kujaribu kuhoji baadhi ya nadharia ambazo bado zilikuwa zinaacha maswali.

Hata hivyo, sikatai kama zipo hoja ambazo zilikuwa zinaonyesha kutofautiana na yeye, naamini hiyo ilikuwa ni changamoto nyingine katika kujaribu kuibua hoja mpya.

Lakini kama alivyowahi kusema bwana huyu kwamba hakuna kujifunza bila ya kutofautiana, nadhani tofauti hiyo imeleta mwanzo mpya wa mjadala huu.

Ukweli ni kwamba nisingependa kuufunga kabisa huu mjadala ili tuwape nafasi wanazuoni watarajiwa ambao bado wanaendelea kukaririshwa ujinga huu wa wanasayansi.

Wachangiaji wengine kama Kamala, kaka Kitururu, na dada Yasinta nayaheshimu sana maoni yao, kwani kwa upande wao nao wamesema kile wanachokiamini, bila kuwasahau Mtwiba, na kaka Fadhy Mtanga walioomba nafasi ya kutafakari kabla ya kuleta chanagamoto zao.
Ningependa kuwaambia kwamba mada hii bado ipo na itaendelea kuwepo, nasubuiri changamoto zao waziweke hapa barazani tuzione.

Bwaya kajenga hoja mpya, katika changamoto yake amesema kwamba nadharia ya mabadiliko ipo na mwanaadamu anaendelea kubadilika. Naweza kukubaliana nae.


Lakini, si kwamba mabadilikon hayo yanatokana na uharibifu wa mazingira wa vyanzo vya maji, hewa tunayovuta vyakula vya viwandani tunavokula, madawa ya hospitali tunayotumia kila tuuguapo na kila uchafu uliojaa hapa duniani?

Kwa mfano siku hizi wanazaliwa watoto wenye mapungufu mengi ya viungo, na hata wale wanaozaliwa wakiwa na viungo vyote, bado si salama kwani hukumbwa na mabadiliko mengine kila wanavyokua. Je mabadiliko anayosema Bwaya ni haya au mengine? Hiyo ni changamoto nyingine.

Bado natafuta majibu.

2 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. nimekufuata leo, nimekaribia sana, yani ile sana. Topiki imenishinda lakini niliwahi kumhoji mwalimu wangu wa historia maana mambo ya sayansi ya siasa na historia ndiyo mwake, nilimuuliza hivi Ni kweli kwamba binadamu alimubwa na mungu hasa katika nadharia ya dini? au ni kweli kwamba tumetoka na evolution of man? vipi huu mkanganyiko wa MAN APES OR APE MAN? wanasayansi wanasema yao nimeshindwa bwana kwaherii kwa leo.

    ReplyDelete
  2. Mahali popote patakuwa na utata wa DINI na HISTORIA. Japo twaijua dini kutokana na Historia lakini hakuna suluhisho la ukinzani wa pamoja. Kutakuwa na ukweli (japo kwa kiwango fulani) kama ukitaka kujua asili ya mtu kutokana na Historia na pia kwenye dini. Ni kwa kuwa Historia haiamini katika Dini sana na dini haitegemeni historia kutenda kazi, basi utaona mkanganyiko wake unaingia mahala pengi. Kuna ukaribu kiasi na unaweza kutetewa na wengi juu ya binadamu kutokana na nyani lakini kama tutaenda nyumba na kuangalia asili ya nyani, na asili ya asili ya nyani na asili ya asili ya asili ya nyani na zaidi na zaidi utaishia mahala ambapo utaambiwa kuwa "havikuwekwa kwenye historia" Na ndipo nguvu ya Dini inapokuja kwa kuwa haikupi nafasi ya kuhoji zaidi ya kitambu cha mwanzo (kwa wale watumiao biblia) wanaposema "hapo mwanzo palikuwako neno .......". Wamesema neno alitoka kwa nani naye neno alikuwa nani kwa hiyo unajua neno ni nini. Got it? Ndipo nguvu ya dini inapoizidi ya Historia na ukishaambiwa kuwa baada ya hapo Mungu akaanza kuumba na aliumba wanyama kisha akamuumba binadamu hutashangaa kuwa yawezekana nyani alikuwa karibu na utendaji wake wa kazi ulionesha kuweza kumudu kazi nyingi ndio maana tukaboreshwa kutoka katika ufahamu, mwonekano na utendaji wa nyani. Kwa hiyo nasikitika kuwa maelezo yangu yote hayatakuwa na suluhisho la msingi kuwa mwanzo wetu ni nini, ila najua tupo na kila mtu aamini kwa imani ama uelewa wake. Swali nililowahi kuuliza kwa kaka Kitururu ni kuwa kwani mwanzo wako ni upi na ni lini? Ukiweka maanani sayansi si twaambiwa ni mjuunganiko wa mbegu za X na Y? Na twajua zaweza kutokana na nini? Vyakula si ndio? Ina maana yawezekana ni sehemu ya vyakula hivi tulavyo tulikotoka? Je tukifa hatutakuwa mbolea kisha tukafyonzwa na mimea na wengine wakala wakapata mbegu tukarejea tena? Ni kweli hii ni mara yako ya kwanza kuishi kama kiumbe? Ama ulishakuwa binadamu ama kiumbe kingine na pengine utarejea kuwa binadamu ama kiumbe kingine? Labda ndio maana ma-Rasta wanasema tunza uhai kwa kutokula nyama maana wanahisi ni mzunguko wa binadamu unaendelea. Wait!! Twaweza kuwa twajila bila kujua. Si ndio? Gosh!!! Tatizo la ku-dig down ni hili. Kuwa utafika sehemu utajiona ukijikatili mwenyewe.
    Mwanzo wa Binadamu ni upi? Sina jibu moja, nasubiri wadau waendelee.
    Blessings

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi