0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Dec 29, 2008

JE, MWANAMKE/MWANAUME KUFUJWA KATIKA UHUSIANO NI KUTOKUJIAMINI AU KUOGOPA KUACHWA?

Imesemwa sana na itaendelea kusemwa kuhusu kutojiamini kwenye uhusiano. Wataalamu wanaamini kwamba, watu wasiojiamini, wanakuwa na matatizo makubwa na magumu au mabaya zaidi wanapokuwa kwenye uhusiano, kuliko kwenye maeneo mengine ya kimaisha.

Kwa wanawake wanakabiliwa na adhabu mbili kwenye jambo hili. Kutokana na mfumo dume, mwanamke anakuwa tayari amepoteza kujiamini anapokuwa mbele ya mwanamume. Wakati mwingine hata kama alikuwa akijiamini hapo kabla, yaani kabla hajaingia kwenye uhusiano.

Kwenye uhusiano wa kifujaji, kama mwanamume ndiye mfujaji, mara nyingi sana, mwanamke aliye kwenye uhusiano huo, anakuwa ni yule mwenye kupenda kujibandikiza kama kupe, ambaye anaamini kuwa hawezi kuishi bila mume huyo. Anapigwa, analaliwa nje, anadhalilishwa kwa njia mbalimbali, lakini ameng’ang’ania.

Ni mara chache sana kukuta mwanamke asiye na utegemezi, yaani asiye tayari kumng’ang’ania mtu, kuolewa na mume mnyanyasaji. Kwa kuwa mtegemezi, mwanamke hatimaye humaliziwa kujiamini kwake kote.

Umewahi kukutana na mwanamke ambaye amewahi kuwa na msululu wa wanaume wanyanyasaji? Anaishia kubadili kutoka kwa mnyanyasaji wa kwanza, wa pili na kwendelea. Hajui kwamba, anakutana na wanaume hawa kwa sababu ya kutojiamini kwake.

Mwanamke anayejiamini hana hofu ya kumwacha mwanamume mnyanyasaji. Anajua kwamba hastahili kufanyiwa vile. Anatengeneza nguvu ya kihisia yake mwenyewe na anakuwa barabara, ngangari hata akiwa peke yake.
Mvuto wa kimapenzi ni nguvu kubwa sana, kama inavyojidhihirisha katika wingi wa picha za wanawake waliokaa kihasara hasara katika magazeti mengi. Wanaume hasahasa, wanaathiriwa sana na wanawake warembo. Baadhi ya wanawake wanagundua kwamba wanaweza kuwasisimua wanaume kwa kukaa au kuvaa kihasara hasara.

Mwanamke asiyejiamini ambaye anataka kibali cha kujihakikishia kuwa yeye ni mzuri au la toka kwa wengine, hutegemea mvuto wa kimapenzi kama ‘gia’ yake ya kuonekana.

Mwanamke anayejiamini hahitaji kukubalika kwa wengine kama ni ajenda yake ya kila siku.
Anajiamini kiasi cha kuweza kujidhihirisha katika uwezo wa aina nyingi; si katika kutegemea mvuto wa kimapenzi pekee.
Katika fasihi nyingi nilizosoma, karibu zote zinasisitiza umuhimu wa kujitegemea kabla ya kuingia katika uhusiano wowote.

Kama ningeweza kutoa ushauri wa kitabu cha kusoma ili mtu awe salama zaidi, ningeshauri kila mtu asome kitabu cha cha Stephen Covey.
Anazungumzia kufanikisha kujishinda mwenyewe kabla ya kuwashinda wengine.
Anazungumzia kuhusu mchakato toka kuwa mtu unayetegemea, unayejitegemea na unayetegemeana na wengine.

Kutojiamini au kuhisi kuwa huko salama hadi wengine wawepo au wathibitishe, kunaweza kusababisha madhara makubwa, hasa kama hujui kutojiamini maana yake nini. Watu wengi wasiojiamini wanapenda kutoa visingizio wanapopata matatizo, wakiwa hawajui kwamba wao wenyewe ndiyo chimbuko la matatizo waliyo nayo.

Mwanzo wa kuwa salama ni kujifunza kujicheka, ukijua kwamba hakuna mtu asiyekosea!
Jiambie kwamba, umekamilika na usitake mume au mke akukamilishe, kwani hataweza.

Jipende mwenyewe kwanza.


5 comments:
Andika Maoni Maoni
 1. kujiamini na kuaminiana ktk maisha ni jambo nzuri sana. kwani inafanyisha maisha yaende safi na kufanya watu wasiwe na magonjwa kama vile moyo

  ReplyDelete
 2. kaka Kaluse, naona hili la wanawake kutokujiamini, lina kaukweli ndani yake.
  Naogopa mama asije akasoma haya maoni yangu, maana nae siku hizi tangu nimuoneshe haya mambo ya Blog, huwa anapitia pitia.
  Anya way nilichotaka kusema ni kwamba huwa namuona mama yangu kama anataka kutoka na baba akishavaa utakuta anamuuliza baba hata mara tano kama amependeza, kama baba akimjibu kwa kifupi kuwa amependeza, haaminimpaka awaulize na dada zangu au mimi.
  Najitahidi sana nisiwe tegemezi, ndio maana naipenda sana hii blog.

  ReplyDelete
 3. Usijali dada Koero kwani akisoma mama atajua njia sahihi ikiwa anakosea. Niwakumbushe katika blog ya Yasinta aliandika kuhusu tabia ya KIBESI cha wanaume ndani ya ndoa, nilijaribu kumdadisi nje ya blog akanieleza amewaona wabongo fulani kule anakoishi wakiacha kila jambo lifanywe na wake zao. Kimsingi ni kwamba hakuna kitu kizuri kama tunaweka mambo kwa usawa wake. Mfano ikiwa mume/mke anakuwa mfujaji halafu mmoja ndiyo mwathirika wa ufujaji huo nadhani hii siyo njia ya kuenenda kabisa tujisahihishe. Kusema kwamba katika uhusiano kujenga tabia kwamba wanawake wanajibanza kama kupe tena ipo sana tu. Uwongo dada Koero? sema wewe kama nadanganya? wapo wanawake wanaodhani kwamba kila kitu ni lazima kiamuliwe na mwanaume au bila mwanaume hawawezi kukifanya. wanadhani kuwa kila jambo katika uhusiano wanaume ndiyo wenye uamuzi wa mwisho huku wakiumizwa na uamuzi wenyewe. Sasa hii inakuwa hatari kujibanza katika uhusiano ambao unajengwa kwa mtindo wa KIBESI na ufujaji ndiyo maana midume inalala nje wala haijali lolote kana kwamba anayemwacha nyumbani ni mpangaji wakati mkewe.
  basi naacha, nipo hoi hasira za kuwatetea wanawake, wanaumia. kwaheri

  ReplyDelete
 4. huwezi kujiamini kama hujitambui. utaishia kwenda tu kwa mabavu mabavu ya kitoto na ya kijinga tuuuu

  ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi