0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Sep 7, 2011

BINTI MSAGAJI KATENGENEZWA NA WAZAZI!

Malezi huweza kuwaathiri!




Mwanamke ambaye ana tabia a kujilaumu yeye kama mwanamke na kulaani kuwa kwake mwanamke, yuko kwenye nafasi kubwa ya kumuuwa mtoto wake wa kike kisaikolojia. Kuna wanawake ambao kwa kuudhiwa na waume zao au hata na wanawake wenzao huwa wanapenda sana kuropoka kauli za kudhalilisha jinsia ya kike.


“Mimi nakwambia sisi wanawake hatufai kabisa, kuzaliwa mwanamke ni jambo baya sana………ningekuwa naweza nimwombe Mungu anibadilishe niwe mwanaume …. Wanawake ni wajinga sana….” Kauli za aina hii zinaporudiwa mara mbili au tatu humfanya mtoto wa kike kuziamini na huanza kuwa na wasiwasi na jinsia yake. Hata watoto wa kiume nao huziamini kauli hizi na kuanza ‘ubabe’ wa kiume kuanzia hapo.


Mtoto wa kike anapozisikia kauli hizi kutoka kwa mama yake na kwa sababu mama yake ndiye ‘shujaa’ wake, huanza kujenga dhana kwamba, kama mama yake hapendi kuwa mwanamke, kwa sababu mwanamke ni mjinga na dhaifu, naye hana budi kuikimbia hali hiyo.


Anaikimbiaje?


Kuna njia nyingi za kukimbia hali hiyo, lakini kubwa na ya karibu ni kwa mtoto huyu kuanza kujibainisha na jinsia ya kiume. Kwa sababu akili ya mtoto haichuji, huanza kuhisi vibaya kuwa kwake mwanamke mbele ya wenzake, hasa wanaume. Kujibainisha na jinsia ya kiume ni pamoja na kufuatana na wanaume, kuvaa kiume, kuongea kiume, kutembea kiume na kufanya kazi za kiume.


Siyo lazima, lakini mtoto huyu anaposhindwa kupata mahali ambapo atadondosha dhana au imani hii, ni wazi atakuja kujibainisha kimapenzi, atajibainisha kama mwanaume. Matokeo ya jambo kama hili ni kuwa na mwanamke ambaye anataka kuwa mwanaume kwa wanawake wenzake kimapenzi.


Kama sio kauli za akina mama kujilaumu, kauli za akina baba kuwalaumu wanawake pia na akina mama kuzikubali kivitendo, zinaweza kuwaathiri watoto wa kike kimakuzi. Baba anapokuwa na tabia ya kutoa kauli kali na chafu dhidi ya mama, na mama kuonyesha kukubaliana na kauli hizo kwa vitendo ni hatari sana.


Hebu sikia kauli kama hii kutoka kwa baba: “Mwanamke gani anayezaa mitoto ya kike tu, ni afadhali kuoa mke mwingine…..” majibu ya mwanamke anayekashifiwa ni haya: “Kwani mimi nimetaka, si Mungu mwenyewe, kwani hata mimi si ninapenda watoto wa kiume……” Kwa mtoto wa kike majibu kama haya, huwa yanasikika masikioni mwake kama, “Hata mimi sitaki watoto wa kike kwa sababu hawana thamani, lakini sina uwezo wa kuwakataa..”


Akina mama, yawapasa kuelewa kwamba, kauli zao na kuzipa kauli za waume zao nguvu, huweza kuwaathiri sana watoto wao. Kila neno wanalotamka kwa watoto ni lazima walikague mara mbili. Waume zenu wanapotoa kauli zinazobagua watoto kijinsia mbele ya watoto hao ni lazima mzikanushe sawia na kuwaeleza watoto ukweli utakaowapa nguvu ya kufurahia jinsia waliyonayo.




3 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. Watu wengi wanafikiri watoto ni watoto yaani hawaelewi kitu ni wajinga...la hasha si wajinga kabisa tena inawezekana sisi watu wazima ndio wajinga. Kwa hiyo tujifunze kuheshimiana, kuwa na maneno mazuri mbele ya watoto hata kama umemchukiza mwenzako. Ahsante kwa darasa kaka Shaban!!

    ReplyDelete
  2. Nakubaliana na mambo mengi katika makala haya. Mfumo dume, mila kengeufu na mazingira kwa ujumla vina nafasi kubwa katika kufinyanga utu wetu.

    Hata hivyo tafiti mpya zinaonyesha kwamba tabia hii ya usagaji/ushoga inawezekana ni tabia ambayo mtu anazaliwa nayo na inabidi itazamwe katika mtazamo huo. Ni kwa sababu hii tiba za kujaribu kuwabadilisha mashoga na wasagaji zimeonyesha kutofanya kazi. Tazama hii link hapa chini:

    http://matondo.blogspot.com/2009/10/wanasaikolojia-mashoga-na-wasagaji.html

    ReplyDelete
  3. mimi mwenyewe huwa nasema,
    kwa nini wanaume ni wepesi sana kupata pesa kuliko wanawake
    hivyo nakuwa na dhana kwamba wanaume wana ujanja fulani wa kupata pesa nyingi. pengine na wanawake wenzangu wana mawazo hayo hayo.

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi