0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Mar 15, 2009

TUNAJIDANGANYA KWA KUAMINI KUWA NDOA NI TENDO!

Hakuna haja ya kununiana

Baadhi yetu tumelelewa na kukutana na mazingira yaliyotufundisha hivyo kwa hiyo ndivyo tunavyoamini. Tunaamini kwamba tunapooa au kuolewa tunafanya hivyo ili kushiriki tendo la ndoa kama dhana ya kwanza. Ni kitu gani kinachotokea basi pale ambapo haturidhiki na kuridhishwa kiunyumba na wake au waume zetu? Ni kwamba huwa tunadhani au kuamini kwamba hapo ndoa haina maana na hivyo huwajengea chuki wenzetu na pengine kutoka nje ya ndoa zetu tukidhani tutapata nafuu.

Hebu tujiulize je ni kweli dhana ya ndoa ni kufanya mapenzi? Jibu ni siyo kweli hata kidogo. Hebu tujiulize tena baada ya kuoana na kuishi kwenye ndoa kwa muda fulani wake au waume zetu wakapata matatizo ya kimaradhi au ajali au mengine ambayo yatawafanya wasiweze kabisa kushiriki jambo hili tutafanyaje? Huenda jibu kwa wale wanaoamini kwamba ndoa maana yake ni kufanya mapenzi watasema kwamba watakwenda nje au kwa wanaume wataoa wake wengine. Huu ni ujinga mkubwa mno kwani tunaweza kufanya hivyo ikiwa ni wenzetu waliopata matatizo lakini kama ni sisi tutaona inavyoumiza.

Tendo la ndoa katika ndoa ni muhimu na kwa kiasi cha kutosha husaidia pia kuimarisha uhusiano. Lakini pale kunapokuwa na tatizo kwenye suala hilo ndipo hapo upendo unapopimwa kama ni wa dhati, bandia, au upendo wa kimradi. Kama upendo wetu ni wa dhati tutajitahidi kuangalia mazingira ambayo huenda yatawafanya hao wenzetu wawe kama walivyo. Tunapojadili kwa upendo udhaifu fulani ni wazi tutawapa wengine nguvu ya kujikagua na kuzidisha upendo kwetu.

Lakini tunapokuwa wakali na kulaumu au kuchukia na kulaani tutawafanya wenzetu wajione wanyonge na pia tutawafanya au kuwapa nafasi ya kuhalalisha kwamba huenda sisi tumetawaliwa sana na tamaa ya kimwili kuliko uwezo wa kufikiri kiasi kwamba linapotokea tatizo tunakuwa vichaa na hivyo uwezekano wa kutoka nje au kuvuruga ndoa ni mkubwa. tujifunze kufahamu na kukubali ukweli kwamba ndoa bora na imara hazifanywi hivyo na tendo la ndoa, bali hufanywa hivyo na wanandoa kusaidia kutatua kila tatizo linalotokea.

Ni vizuri tukawa wazi kusema matatizo tunayohisi kwa wenzetu badala ya kuhisi tu na kudhani watayaona. Tukifanya hivyo tutakuwa tumeshindwa jukumu letu la kupenda kwani tutakuwa tumejitazama wenyewe zaidi..

12 comments:
Andika Maoni Maoni
 1. Shabani hapo umenena, unajua ni kweli kabisa wengi huzani ndoa ni kufanya mapenzi. Hawajajua kuwa kumpenda mtu ni kumpenda mtu kama alivyo sio kwa sababu kufanya mapenzi. Kuna watu ambao hawawezi kabisa kueleza matatizo yao kwa mwenza wake. Hapa nina maana kama hasikii ile raha ya mapenzi/tendo la ndoa basi atanuna tu bila kusema kitu. Mawazo yake kuwa mwenzake anajua. Kwa sababu katika ndoa ni LAZIMA kuongea kubadilishana mawazo sasa kama unamwogopa mke/mume wako hhaina maana kuishi naye. Pia ni kweli hakuna ndoa ambayo haina matatizo
  Nami nasema ni kweli kabisa hakuna haja ya KUNUNIANA

  ReplyDelete
 2. Umitufumbua macho Kaluse

  ReplyDelete
 3. Ndoa,Upendo na Tendo la ndoa ni vitu vitatu vyenye maana tofauti kabisa.Kila mtu anaweza kuwa na tafsiri yake kuhusu hayo mambo matatu ukiachana na tafsiri za kisheria na kiimani kv dini.Mimi natafsiri hayo mambo kama ifuatavyo;
  Ndoa ni tendo la mke na mume kuishi pamoja.Yaweza kuwa kwa hiyari ya wawili hao au wamelazimishwa kuishi pamoja(ndoa ya mkeka)au imetokea ktk mazingira ambayo hata wao hawajui ilikuwaje lakini ikatokea wanaishi pamoja.
  Upendo ni hali ya mtu kujikubali na kujipokea kisha kuwakubali wengine na kuwapokea kama walivyo,yaani kukubali mazuri yao na mapungufu yao.
  Tendo la ndoa ili ni suala la kimaumbile zaidi,yaani mwili unahitaji kufanya mapenzi kama vile unavyohitaji kula na kunywa ingawa kwenye suala la mapenzi unaweza ukaudhibiti mwili na usipate madhara.
  Makosa tunayoyafanya sisi ni kuchanganya ndoa na tendo la ndoa kisha kuuita UPENDO.Kwa hiyo ina maana kitu kimojawapo kati ya ndoa na tendo la ndoa kinapokosekana basi nao upendo huonekana kuwa haujatimia au umekwisha kabisa.
  Nionavyo mimi kitu cha muhimu ndani ya ndoa ni kuwa na upendo kisha mambo mengine yafuatie.Mtu mwenye upendo wa dhati hawezi akaanza kumchukia mtu kwa sababu tu amekatika mkono au mguu kwenye ajali au hawezi kufanya tendo la ndoa kwa sababu ya maradhi au namna nyingine yeyote.

  ReplyDelete
 4. Mh!!, hata mimi mwenzenu nilikuwa sifahamu haya mambo. Awali niliposoma hii habari sikuielewa, nashukuru kaka Katawa amesherehesha vizuri sasa nimeelewa.
  Lakini nadhani wanaume ndio wenye udhaifu huu wa kuamini kuwa ndoa ni tendo la ndoa, na ndio maana hukimbilia kutafuta nyumba ndogo.

  ReplyDelete
 5. koerooo unaonge hili kkwa kuwa wewe sio mwanaume nini?

  kwani we hufanyii tendo hilo?

  ReplyDelete
 6. koerooo unaonge hili kkwa kuwa wewe sio mwanaume nini?

  kwani we hufanyii tendo hilo?

  ReplyDelete
 7. Fred nakubaliana na wewe.
  Labda kwa kuongezea wengi huingia kwenye ndoa kwa kutarajia kupendwa na kusahau wajibu wao ni kupenda.Wanataka kupewa upendo kwa bahati mbaya kutoka kwa mtu ambaye naye hakupewa upendo,basi hapo ni vurugu tupu.Pia wewe mhusika kabla haujaingia kwenye hiyo ndoa, kama uliamini ndoa ni kufanya ngono basi inapokosekana ngono kitakachotokea ni ugomvi tu.Da Koero nikusahihishe kidogo binadamu yeyote asiye na upendo katika ndoa yake lazima atatoka nje.

  ReplyDelete
 8. Fred nakubaliana na wewe.
  Labda kwa kuongezea wengi huingia kwenye ndoa kwa kutarajia kupendwa na kusahau wajibu wao ni kupenda.Wanataka kupewa upendo kwa bahati mbaya kutoka kwa mtu ambaye naye hakupewa upendo,basi hapo ni vurugu tupu.Pia wewe mhusika kabla haujaingia kwenye hiyo ndoa, kama uliamini ndoa ni kufanya ngono basi inapokosekana ngono kitakachotokea ni ugomvi tu.Da Koero nikusahihishe kidogo binadamu yeyote asiye na upendo katika ndoa yake lazima atatoka nje.

  ReplyDelete
 9. Nimezungumzia jambo ambalo nimelifanyia utafiti na hata watafiti wengi wankiri hivyo kuwa wanaume kwa kiasi kikubwa ndio wasioweza kudhibiti mihemko yao ya kimapenzi. kwa sababu wao wameaminishwa kuwa ndoa ni tendo la ndoa.
  Hebu chunguza migogoro mingi ya ndoa, mingi utakuta kuwa wanaume ndio wanolalamika kunyimwa tendo la ndoa, na ndio sababu utawasikia wakisema, "Nimeamua kumtafutia nyumba ndogo kwa sababu ananinyima" au "kila siku anadai anaumwa nanndio sababu ya kumuolea mke wa pili"

  Wanawake ni wavumilivu sana, kwa sababu wao wamfundishwa kuwa hawapaswi kuomba tendo la ndoa baliwasubiri waombwe, na kamawakithubutu kuomba, dhana ya kuhisiwa kuwa ni malaya itaanzia hapo. na huenda ukaibuka ugomvi mkubwa. Kwa mwanaume kuambiwa na mke kuwa, "Sijatosheka" ni matusi makubwa.
  Jamani sipigi Blah..Blah.. hapa, najua ninachokizungumza, na hata wanaume mnalijua hili ila mnajitia hamnazo!!!!!

  ReplyDelete
 10. koero hao ni wanawake wa enzi zile na sio nyie kizazi cha dotcom.

  wewe koero unaweza kuniambia kuwa hujawahi kumtongoza mtu au kuomba tendo la ndoa?

  maandishi mengine yamepitwa na wakati na usijibu kwa kuyarejea maandishi, rejea kwakowewe mwenyewe na kwa marafikizo

  ReplyDelete
 11. Kamala...

  Haya, sitajibu.

  Maana umenifunga mdomo.

  ReplyDelete
 12. kweli hiyo, wanasema mkiijua kweli itawaweka huru

  ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi