0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Mar 13, 2009

KAMA KIFO HUJA HIVI, BASI KIFO NI KITAMU.

Sioni sababu ya kukihofia kifo tena

Nilikuwa nimelala sebuleni kwenye mkeka huku nikiwa nimelalia mto, ni wakati huo ndipo nilipoanza kuhisi visindano vikinichoma kwenye nyayo, lakini havikuwa na maumivu sana.

Ghafla nilianza kuhisi miguu ikianza kufa ganzi na kupoteza uhai taratibu, na kwa kadiri muda ulivyokuwa ukizidi kwenda ndivyo ile ganzi ilivyokuwa ikizidi kupanda. Ile hali iliendelea hivyo hadi mpaka kwenye nyonga, na kutoka kwenye nyonga ghafla ilipanda mpaka shingoni, hadi hapo nilihisi kama kuna jambo ambalo si la kawaida linanitokea kwani mwili wangu kuanzia miguuni mpaka shingoni ulikufa kabisa, yaani nilihisi kama nimekatwa shingo na kubakia na kichwa tu chenye uhai, nilianza kupaza sauti kumuita mama ambaye alikuwa jikoni akiendelea kuandaa chakula cha jioni.

Nilimsikia mama akinijibu kwa mbali kuwa anakuja lakini sikuoana dalili ya yeye kuja, mara mdogo wangu wa kiume akapita pale sebuleni na kuniona, kwa kweli sijui alihisi nini kwani nilimsikia akipiga kelele za kumuita mama huku akisema “ Mama Eggy anakufa”
Mama alikuja mbio ,alipofika na kuniona nae alipiga kelele “mama yangu mwanangu anakufa”

Kuanzia hapo sikujua kilichoendela, lakini katika hali ya kustaajabisha nilijikuta nikiwa nautazama mwili wangu ukiwa umelazwa kitandani hopitalini, na hospitali yenyewe nilikuwa naifahamu vizuri kwani ilikuwa iko jirani na nyumbani. Sijui hasa nilikuwa nimekaa au nimesimama, nilikuwa kama naelea hewani lakini nilikuwa nauona mwili wangu umelala kitandani nikiwa nimetoka humo.

Nilimuona daktari ambaye nilikuwa namfahamu alikuwa amesimama akiendelea kuchukuwa vipimo, na pembeni alisimama nesi mama mtu mzima akiwa anaruka ruka kwa wasiwasi kwa kuchanganyikiwa huku akisema “Daktari angalia asije akatufia hapa mtoto wa watu” yule daktari hakumjibu aliendelea kuufanyia mwili wangu vipimo lakini jasho lilikuwa likimtoka hasa nadhani ni kwa ajili ya wasiwasi, baada yakipimo cha mapigo ya moyo kutompa majibu aliyoyategemea.

Mwili wangu ulikuwa umevaa gauni la bluu ambalo nilihisi hilo gauni lilikuwa ndio tatizo hivyo nilipata wazo la kwenda nyumbani ili kuchukuwa nguo lenye rangi nyingine ili niweze kubadilisha na kutoa lile gauni.

Kabla sijaenda nyumbani kuchukuwa nguo, nilitoka nje ya chumba kilichokuwa na mwili wangu, na kuwaangalia mama na kaka yangu ambao walikuwa wamekaa kwenye korido ya ile hospitali, walikuwa wanalia wakidhani kuwa huenda nitakufa. Niliwatoa wasiwasi kwa kuwaambia kuwa wasilie kwani mimi ni mzima, lakini hawakunisikia na wala hawakuonesha kwamba walikuwa wakiniona pamoja na kwamba niliwasogelea karibu.

Niliondoka pale na mwendo wangu ulikuwa ni kama upepo kwa kuwa huo mwili niliokuwa nao ambao ndio mimi hauwezi kujibainisha kama huu mwili tulio nao, ingawa nilikuwa na ufahamu wa kila kitu na kila jambo lililokuwa liliendelea kwa wakati huo.
Niliweza kupenya ukutani na darini kwa staili ya kuelea, na nilipofika nyumbani nilifungua kabati langu ili kuchagua gauni lingine, lakini sikupata gauni nililolitaka, hivyo niliamua kurejea kule hospitalini.
Nilipofika nilimkuta yule daktari akiwa bado amekaa na kushika tama na yule nesi alikuwa analia huku akisema “ masikini mtoto wa watu”

Nilianza kuukagua mwili wangu tena, ghafla ukatokea ukimya wa ajabu, kama vile nilikuwa nasubiriwa kufanya uamuzi, nikajiambia “ pengine haya yamenikuta kwa kuwa simjui mungu” nilijikuta nikisema kwa sauti ambayo hata hivyo haikuwasitua waliokuwa pale ndani “Mungu usiniuwe hadi nikujue”

Itaendelea wiki ijayo………….

10 comments:
Andika Maoni Maoni
 1. Shabani, kwanaza nimefurahi halafu nimeogopa. Kweli hakuna sababu ya kuogopa kifo. Ila kwa wale walio hai ni uchungu sana. Pole sana kwa mama na kaka bila kujua mtoto/kaka amekuwa pepo. Hii ni kweli au?

  ReplyDelete
 2. Kasule naomba nikuulize hii ni hadithi,au ni true story? samahani kwa kuanza kuuliza hivyo,mimi imenigusa sana nikitu ambacho kilitokea kwenye familia yetu,mama yangu mdogo alipatwa na mkasa kama huu.

  Kusema kweli yeye ilimchukua siku 3 akawa katuacha,siku yakwanza ganzi ilianzia miguuni mpaka kwenye magoti,siku ya pili ilikuwa kiuno na tumbo na siku ya tatu ilimalizia kifuani mpaka kichwani na mtu akawa kaondoka,usiombe ikakutokea imenikumbusha mpendwa wetu ni mama yangu mdogo aliyezaliwa pamoja na mama yangu mzazi.

  Ilikuwa ni vigumu kuamini na mpaka leo bado naona kama sio kweli labda ni ndoto tuu,lakini ukweli unabaki pale pale hatunae tena.

  ReplyDelete
 3. Dada Yasinta na Dada Passion

  Hii ni habari ya kweli na inamuhusu mwanafunzi mwenzetu wa madarasa ya utambuzi kama nilivyo ambatanisha picha yake kwenye habari hii.

  habari hii ni ndefu sana na nimejitahidi kuifupisha ili angalau msomaji apate picha ya jinsi sisi wanaadamu tulivyo na nguvu za ajabu.

  Wiki ijayo nitaimalizia habari hii.
  samahani kama nitakuwa nimewakwaza kwa kuifupisha lakini wiki ijayo naimalizia.

  ReplyDelete
 4. Vipi kuhusu kile kifo cha polepole ambapo mtu unakuwa na maumivu sugu ya miaka mingi kiasi kwamba hata dawa kali kabisa za kutuliza maumivu zinakuwa hazikusaidii tena? Kifo cha aina hii ndiyo tukiogope? Naomba ninukuu kauli ya Mwanafalsafa Simon Kitururu hapa "Kabla ya kufa ni vigumu kweli kuhitimisha maongezi ya KUFA"

  ReplyDelete
 5. tehe passion hii story nami naijuwa na ni ya kweli na kifo kwa kweli kina aina nyingi na jinsi nyingi pia za kutokea

  matondowewe swali lako du!

  kifo hicho naogopa kusema lile ninalolijua kwani lawez kutisha kidogo na hivyo inabidi kulisemakwa nji nyingine kabisa lakini kumbuka kila jambo lina wakati wake na sababu za kuwa vile lilivyo.

  ReplyDelete
 6. Duh!
  Jamani mimi niliwahi kuota.

  Nikiwa kidato cha Tano,siku moja wakati wa usiku nilota ndoto.Niliota nimekufa nikiwa shuleni,wanafunzi wenzangu walikuwa wakilia sana kwa uchungu ila mimi nilikuwa nimekaa pembeni ninawaangalia baadaye maiti yangu iksafirishwa hadi nyumbani ambako wazazi wangu waliipokea kwa kulia sana nakumbuka mama yangu alizimia karibu mara tatu.Baaba ya hapo nikapelekwa kwenye makaburi kuhifadhiwa,wakanizika na wao kurejea nyumbani.Nilikaa kaburini kwa muda kama wa saa 1,baadaye mikaona nirudi duniani wakati narudi duniani nikashituliwa na hodi iliyogongwa kwenye chumba nilichokuwa nimelala.Nilijaribu kuitafakari sikupata jibu.Bwana kamala na Shabani mnasemaje juu ya hii ndoto?

  ReplyDelete
 7. nuru ni ndoto tu we unadhani ninini?

  wewe kama mwanamadarasa pale faji, tutafikia somo la ndoto.

  ila kumbuka ni ndoto tu na wala mama yako na wanafunzi wako hawajalia wala nini. huu mfano alioutoa kaluse ni wa live na sio ndoto.

  ila kila ndoto ina maana yake na sababu zake na inabidi ujue kuitafsri vyema

  ReplyDelete
 8. Kamala,

  mimi nadhani Nuru kaomba darasa humu na sio faji, unaonaje kama ukimjibia humu?
  Kuna wadau wangependa kujifunza kupitia swali hilo.....

  AU.........

  ReplyDelete
 9. ur blog get high ranking in google, you can realy earn from google ranking,if u want to earn money from googleads plan, then we can earn together just mail me at manngnth@gmail.com, you will realy earn $500-800 in month from your blogspot,we both can make profit

  ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi