Kutuhumiana kunakuwa kwingi
Kuna watu wengi ambao wanaamini katika jambo hili, kwamba kama mtu hana wivu, ina maana kuwa hampendi mpenzi wake. Wanaamini hivyo, kiasi kwamba wapenzi wao wanapokuwa na wivu juu yao hujisifu kwamba wanapendwa. Hali hii inatokana na kutofahamu tofauti iliyopo kati ya kupenda na kutamani au tendo la ndoa.
Unapohisi haja ya kujamiiana unapohisi kushiriki tendo la ndoa, yaani unapokuwa na hisia ya kushiriki tendo ni lazima utakuwa na wivu. Unakuwa na wivu kwa sababu tendo la ndoa sio upendo. Penye upendo hakuwezi kuwa na wivu.
Unapokuwa na mtu au kujifunga na mwanamume au mwanamke kimwili ni lazima uwe na hofu kwa sababu tendo la ndoa siyo uhusiano bali ni aina ya matumizi yasiyo halali ya mwili wa mwingine. Kwa kujifunga na mtu kwa sababu ya tendo la ndoa kila wakati utaogopa kwamba huyo mwenzako atachukuliwa na mtu mwingine atakuacha. Huo ndo wivu ndiyo maana ya wivu.
Kwenye tendo la ndoa zaidi kilichopo ni watu wawili wanaonyonyana au kila mmoja hutumia mwili wa mwingine isivyo halali. Hakuna mapenzi kwenye tendo la ndoa kuna kila mmoja kutaka kufaidi mwili wa mwenzake au kupata kitu au mambo kutika mwili wa mwenzake. Kwenye kupenda tendo la ndoa halina nguvu hivyo wivu hauwezi kuwepo.
Hofu za kuachwa na mwenzake humfanya mpenzi kutoruhusu mambo Fulani, humfanya kuchukua juhudi za kumlinda huyo mpenzi asikutane na mtu mwingine wa jinsia tofauti. Je hujaona wapenzi wanapigana na kutoana roho kwasababu ya mwenzake kumwangalia sana mwanamke au mwanaume fulani? Halafu bado unaita kwamba mtu mwenye wivu anapenda.
Kuongea ndiyo kabisa kwana kuna wakati mwanaume au mwanamke humkataza mwenzake asiongee na mtu yeyote wa jinsia tofauti, labda tu yule ambaye amekubaliwa kuongea naye. kila wakati mtu anahofu kwamba mwenzake atachukuliwa. Halafu mtu bado anataka tuamini kwamba huko ndiyo kupenda.
Kumbuka kwamba upendo unakuwa wa kweli na mzuri pale unapotolewa kwa hiari, bila kutisha wala kulazimisha, bila kuhangaika, bila tafrani. Pale ambapo mpenzi au wapenzi wamefungwa kutokana na wivu. Upendo hapo hauwezi kuchipuka. Kwenye kulazimishana, kufungana, na kulindana upendo haumei.
Mimi ninaposema nakupenda kama kweli nakupenda siwezi kukuumiza ukiwepo wala usipokuwepo. Kwa hiyo nikisema nakupenda ni wazi nitauchunga mwili wangu na kuuweka kwa ajili yako. Lakini kama nakutaka, nataka mwili wako, nataka tendo la ndoa kutoka kwako nikiwa gizani nitaugawa mwili wangu kwingine kwingi. Ndiyo maana penye wivu ni pale panapohusisha tendo la ndoa tu.
Unapomlinda mtu, kumbuka umemshusha sana kiasi kwamba unamchukulia kama kifaa, chombo, kama mali na sio binadamu. Yule anayeonewa wivu naye ataendelea kuwepo kwenye uhusiano na siyo kwa sababu anampenda hapana atakuwa kwenye uhusiano kwa sababu nyingine. Utampenda vipi mtu ambaye anakulinda na kukuchunga, mtu asiyeamini kwamba unaweza kulinda mwili wako mwenyewe?
Tendo la ndoa linapopewa uzito mkubwa kwenye uhusiano wivu ni lazima utakuwa mkubwa. Mtu akiacha tendo la ndoa na wivu huondoka. Wapenzi ambao hawapendani na kufikia mahali hakuna anayetaka kusikia kuhusu tendo la ndoa, kamwe hawaoneani wivu. Unafikiri ni kwa nini? Ni kwasababu wivu unatoka kwenye tendo la ndoa na siyo mahali pengine.
Kwa hiyo ukitaka kuacha wivu inabidi ulibadili swala la ndoa liwe upendo. Kama ukipenda mtu ile kumpenda tu ni dhamana na usalama wa kutosha kuwa hatakwenda kwa mtu mwingine. Kama kweli unampenda mtu utajua kwamba huwezi kwenda kwa mtu mwingine. Lakini kama akienda ujue hakuna upendo na huwezi kufanya lolote ameamua kwenda ni yeye. Hata kama utaamua kumuua bado haina maana kwa sababu maiti haina matumizi yeyote ya maana huwezi kuipenda.
Kama kuna wivu ujue kabisa hakuna upendo bali hapo kuna tamaa ya mwili ambayo imefichwa nyuma ya neno kupenda. Kilichopo kati yenu ni tendo la ndoa tamaa ya mwili lakini siyo upendo. Mtu anayependa analijua jambo hili kwa sababu hana wivu. Hivyo hana shida ya kukagua simu ya mwenzake kuchakura mifuko au mikoba yake au kumtumia watu wamlinde.
Hatukufundishwa kupenda na hivyo wengi hatujui hata kupenda maana yake ni nini. Tumefundishwa kwamba watu wawili wakisema ni wapenzi jambo linalo wafunga ni tendo la ndoa. Ndiyo maana unaweza kusikia “yule mwanamke aliyemuoa alikuwa Malaya sana” nguvu inawekwa kwenye tendo la ndoa siyo mahali pengine. Lakini huyu Malaya anapopenda hawezi tena kuwa Malaya. Kama alikuwa Malaya ni kwa sababu hajawahi kupenda.
Watu wanaishi kama hawaishi, wanaishi kwa kuogopana. Kila mmoja anamwogopa mwenzake anaamini kwamba atatoka atamwacha. Unajiuliza ni kwa nini hawa watu wanaishi pamoja kama wanaogopana? Lakini siku zinaenda na maumivu yanaendelea.
Kumbuka kwamba uaminifu upo au haupo. Kama haupo huwezi kuulazimisha kwa kutumia wivu. Wivu ni dhana ya kujaribu kuleta uaminifu lakini haina nguvu hiyo. Kama uaminifu upo basi hapo kuna kupenda. Kama uaminifu haupo huwezi kuuleta wewe. Ni bora kujitenga kwa sababu huamini kwamba unaweza kuishi bila huyo mwenzio, kwa hiyo unajaribu kulazimisha kutafuta uaminifu.
Kama hakuna uaminifu basi hakuna haja ya kufanya uharibifu, Una haja ya kujua tu kwamba huyo mwenzako ambaye unampenda hawezi kupokea upendo. Kumbuka upendo wako unapomwagika kila ukiutoa inachosha. Huna haja ya kuchoka au kuumia….. toka

Kaka umenena. Natafakari.
ReplyDeleteSijui ni kwanini napenda kuamini visivyoaminika. Yaani kuamini kuwa kuna MATATIZO MAZURI. Na ndilo nikabilianalo nalo sasa. Kuwa TATIZO ZURI LA SASA ni kuwa UMEMALIZA KILA KITU. Namaanisha kuwa umenena yote nami naungana nawe katika mengi ya uliyosema.
ReplyDeleteAsante Kaka
Pamoja daima
Sina cha kuongeza.Umeonyesha tatizo na ukatoa dawa.
ReplyDeleteKazi nzuri kaka.
mh, wwewe unaweza kumwacha mkeo kwenye jera ya wanaume? je kama umefika mahala hamna pa kulala, kuna nafsi moja tu ya kushare na mtu ambaye ni mwanaume katangulia, unaweza kumruhusu mkeo alale pale na wewe ulale nje au kwenye gari?
ReplyDeletesijui lakini
Ni kweli kabisaaaaa. Tena namsubiri Koero aseme maana siku hizi sijui amekuwaje hata hatembelei sana hapa
ReplyDeletemarkus, Kama ukisoma kwa makini hii makala utagundua kwamba imejitosheleza.
ReplyDeleteSidhani kama ninaweza kuikosoa au kuongeza chochote bali kuiacha kama ilivyo.
;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;
Kwa sasa nina msongo wa mawazo ndio maana siku hizi nimekuwa mvivu sana kuandika, mwenzenu napata tiba ya ushauri nasaha mahali fulani, nikipona nitarejea kama kawaida.