0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Sep 14, 2011

THAMANI HULETWA NA UHABA!


Mafuta yalipanda thamani kutokana na uhaba!Uhusiano wa uhaba na thamani ni mada ambayo ikianza kujadiliwa aina kikomo. Kila mmoja wetu anajua kwamba maji ya mito kwa ajili ya kunywa ni kuhimu kwa maisha a binadamu.


Watu wa vijijini ambako kuna mito mingi hawaoni thamani thamani ya maji na ndiyo maana wanakunywa bure. Kwa maana hiyo pamoja na umuhimu wa maji, watu hao wanaona kwamba hayana thamani kwa sababu ni mengi. Lakini watu wa miji kama Dar wanaona maji ni muhimu kwa sababu kwanza wanayanunua.Pili, yakikatika kwa muda wa wiki mtu, watu wanatafutana! Ndoo moja ya maji inapanda sana. Kwa hiyo kumbe thamani ya kitu inaongezeka kukiwa na uhaba wa kitu hicho.


Kama kitu siyo haba kama yalivyo maji kwa watu wa vijijini, thamani ya kitu hicho hupungua! Ni kama ilivyotokea hivi karibuni baada ya wauzaji na wasambazaji wa nishati a mafuta walipoanya mgomo baada ya serikali kushusha bei ya nishati hiyo, hali ilikuwa ngumu kweli hapa nchini na ilifikia hatua walanguzi waliuza mafuta kwa bei mbaya ambayo wengi hawakuitarajia, lakini walilazimika kununua.

Hali hiyo inaweza kutokea pia kwenye chakula, madawa na vitu vingine ambavyo vinakuwa haba baada ya janga Fulani kutokea.


Katika nchi kama Marekani umeme haukatiki na hivyo watu hawaoni umuhimu wake kwa sababu sio haba.

Mtu wa Marekani kwa mfano akija huku kwetu ambako umeme ni swala la ‘kukata shingo’ atagundua kwa mara ya kwanza thamani ya umeme. Unapokikosa kitu, kinatengeneza thamani kwa sababu ni haba.Pia uhaba ni kama mwalimu. Kwa mfano, kama kuna uhaba wa petroli au dizeli. Wenye agari wanakaa kwenye vituo vya mafuta kwa muda mrefu wakisubiri ili wapate huduma hiyo.

Wakati mwingine wanalazimika kupata mafuta kwa njia ya kuruka kama upatikanaji wake unakuwa wa mashaka zaidi.


Lakini uhaba huu kama mwalimu; baadhi ya watu badala ya kukaa kwenye foleni na kupoteza muda wanaamua kutotumia gari katika safari ambazo si za muhimu sana.

Sasa tunakuwa macho kutokana na uhaba. Tunaanza kujua kwamba kila kilometa moja inakula mafuta kiasi gani wakati zamani tulikuwa tunajaza mafuta tani yetu na kwa fujo!Sasa tunafanya maamuzi kwamba niende na gari au niende kwa miguu! Sasa akili yetu inakuwa na neon uhaba kwa karibu zaidi kuliko neon wingi.
Uhaba maana yake ni umasikini. Uhaba ni neon la kiuchumi lenye maana, mahitaji yamezidi rasilimali. Kitu kikiwa haba bei yake inapanda.
Ndio maan sasa hivi serikali ya Tanzania inadai kwamba bei ya vyakula inapanda kwa sababu mvua haikunyesha na hivyo kuna uhaba wa vyakula.
Pia uhaba unaweza kuoanishwa na upatikaaji wa kazi. Kazi ambazo ni adimu zina mishahara mikubwa kuliko kazi ambazo sia adimu.
Kazi adimu ni zile ambazo mafunzo ake ni magumu na hivyo si kila mtu anaweza kuingia na kujifunza.
Wale wanaojitoa muhanga na kusomea fani hizo ngumu wakishamaliza hupata mishahara minono kuliko wat waliosomea fani ambazo ni rahisi kiulinganifu! Na kama serikali zingeweka mishahara sawa kwa fani rahisi na fani ngumu hakuna mtu ambaye angekuwa anasomea fani anasomea fani ngumu!


Kwa hiyo sababu mojawapo ya kuweka mishahara juu kwa ani ngumu ni kuwavutia watu wajitoe muhanga kusomea fani hizo ili wakihitimu wapate mishahara mikubwa! Kwa hiyo fani zenye wataalamu haba zina mishahara minono kuliko fani zenye wataalamu wengi.


Sasa swali linalobaki kwako ni kwa kiasi gani umejiandaa kifani pale kampuni yako itakapoamua kupunguza wafanyakazi? Uko katika watu wenye kazi adimu katika kampuni yako hata kama leo ukiamua kuacha kazi unaamini kwamba kampuni yako itatetereka? Soma kila wakati ili uwe na moja ya fani ambayo kama janga la kutaka kupunguza wafanyakazi likitokea basi wewe uwe mmoja wa wale watakaosalimika.
Na ndio maana wale wanaotetemeka sana wakati wa kupunguza wafanyakazi ni wale wafanyao kazi zisizo na ujuzi!
1 comment:
Andika Maoni Maoni
  1. Ahsante kwa darasa hili la kuelimisha...naweza nikasema kwa kweli hasa hili la umeme nimeshuhudia mwenyewe kwa vile mimi ni mtu wa sehemu mbili siishi sehemu yenye umeme tu. Na nshukuru kwa hili hasa kwa wanangu maana tuwapo nyumbani TZ huwa hawapati shida kwa vile wanajua basi wanakuwa wamejiandaa ila huwa napata maswali sana....Ahsante tena kaka Shaban...naona nianze kusoma kuwa daktari ..maana ...naacha

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi