0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Dec 11, 2008

HATIMAYE NIMERUDI, HITIMISHO LA MADA YA MUDA HILI HAPA

Nilipoandika ile makala juu ya watu kuendeshwa na muda, wengi hawakunielewa. Hata wale wajuvi niliotarajia kuwa wataweza kutegua kile kitendawili, kiliwashinda.
Baada ya kushindwa kwa siku kadhaa kubainisha kile nilichokuwa namaanisha katika makala yangu iliyopita, kutokana na Kompiuta yangu kupata mushkleli wa kiufundi, hatimaye nimerejea tena baada ya kutibu ule ugonjwa uliyoikumba.
Hata hivyo wakati narekebisha kitendea kazi changu hicho sikujali muda na wala sikuendeshwa na muda, niilichojali zaidi ni ufanisi katika kushughulikia tatizo.

Niliposema kwanini uendeshwe na muda sikumaanisha watu wawe wavivu na kuacha kutekeleza majukumu yao kwa jinsi walivyopangiwa au walivyojipangia.
Kama unataka kuelewa ninachomaanisha huna budi kutoka kwenye muda, yaani chukulia kwamba hakuna kitu kinachoitwa muda hapa duniani, hapo ndipo utakapoelewa mantiki ya makala hii.

Ukweli ni kwamba tumefungwa sana na muda kiasi kwamba kila tunapotaka kufanya jambo lolote tunaendeshwa na muda zaidi kuliko ufanisi.
Je tunahitaji kutekeleza matakwa ya muda au ufanisi wa jambo tunalotaka kufanya?

Ninaamini kwamba mtu anatakiwa kufanya jambo mara moja, hapo hapo bila kusubiri, lakini asiwe na haraka katika kufanya. Kwa nini nasema asiwe na haraka? Ni kwa sababu ndani ya haraka mara zote mtu anakuwa amechelewa, ndani ya haraka kuna kusahau vitu vingi sana tena vya msingi, ndani ya haraka hakuna ufanisi bali kuna kulipua kwa sababu muda unakuendesha na huna budi kuuwahi ili usije ukachelewa.

Kwa nini tunaamini kwamba muda wote ambao tunaishi, yaani sasa hivi, muda huu tuliopo sasa ni muda wa dharura? Ni kwa sababu, muda uliopo ndio ulionao, na kamwe huwezi kutegemea muda ujao, kwani muda huo ujao iwe utakuja kweli au hautakuja, hiyo iko nje ya uwezo wako.
Hivyo kila sekunde tunayoishi, ni dharura.

Kwa nini ni dharura? Ni kwa sababu kama unataka kufanya jambo. Lifanye leo, sasa hivi. Unaweza vipi kuahirisha wakati muda huo ujao hauko chini ya uamuzi wako? Najua unaweza kuhisi ugumu, lakini hakuna kitu kigumu ndani yake na ukiendelea kusoma, utaona ninachokilenga kwa undani zaidi.

Nimezungumzia dharura na sijazungumzia haraka. Kufanya kwa dharura kuna maana kwamba, una muda mfupi sana na jambo, na inabidi lifanyike mara moja. Kwa hiyo, ili mtu umudu kufika unakotaka, inabidi ujue kwamba muda huu alionao ndio muda pekee wa kufanya kwa sababu muda ujao haupo na haukuhusu.


Kumbuka kwamba umezaliwa bila mkataba, bila makubaliano na yeyote na tena bila hiari yako. Jambo hilo halikuwa ndani ya uamuzi wako. Lakini pia utakufa bila ya taarifa za mapema, bila kupanga siku au muda. Hiyo nayo iko nje ya uwezo wako wa kuamua, na ukishakufa hutaweza kulalamika.

Kwa hiyo ambacho kiko chini ya uwezo wako unachoweza kukipanga ni muda huu, sasa hivi, ambapo unaweza kutenda kwa busara au kwa hasara.
najua mtu anaweza kupigwa na mshangao au kuingia kwenye kitendawili kingine kutokana na maelezo yangu haya.
Ninachosema ni rahisi sana, ishi leo, sasa hivi, kwani muda pekee uliopo ni sasa hivi.
Kuendeshwa na muda ni kujitia hofu na mashaka kusiko na sababu, kwa hiyo tujijengee utamaduni wa kutekeleza majukumu yetu kwa dharura na, muda usiwe ni egemeo la kutuendesha ili kutekeleza majukumu yetu.
Nadhani nimeeleweka sasa

4 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. Nafikiri naelewa unapolenga Mkuu. Lakini naweza pia kumuelewa aisiye jali muda ingawa kuna muda.

    Tusije tukawa tunazinguka na tafsiri au mitazamo ya muda tu lakini!

    Asante kwa ufafanuzi Mkuu!

    ReplyDelete
  2. Shabani! Asante sana kwa mada hii, Muda muda muda, kuna marafiki zangu mara nyingi wamekuwa wakiniuliza kwa nini ninyi waafrika hamna muda yaani kama unataka kwenda kumsalimia mtu ni kwenda tu. Kwa sababu wao ni lazima kuandika kwenye kitabu na hii nimegundua kama ulivyosema wanaandika kila kitu na mwisho wanasahau kile cha muhimu. Na pia inawaletea (stress) Kwa sababu kila kitu muda hata kula chakula au kunywa chai muda. Ngoja niwachekeshe kidogo kuna siku nilikuwa naenda mjini na ilibidi nienda kwa basi lakini eeh mimi bwana mwafrika nilitembea taratibu kama mwendo wa kinyonga na nikaona kuna wengine nyuma yangu wanakimbia utafikiri wanakimbiza mwizi kumbe kuwahi basi. Ni kweli hata mimi ilibidi nikimbie basi liliniacha wakati mimi nilikuwa hatua mbili tu kisa muda wa kuondoka ulishafika. GARI HALINGOJI MTU. Sijui kama nimeeleweka! kazi kwelikweli

    ReplyDelete
  3. Bwana ambiere Kitururu,
    Ukweli ni kwamba muda upo kwa wale wanamoamini na siwezi kuwalazimisha wale wanaoendeshwa na muda badala ya kujali ufanisi kukubaliana na mimi.

    Labda kama wakiamini kubadilika kwa hiyari yao. Lakini mbona ni rahisi sana kuachana na yale mambo tunayoyafanya kwa mazoea, kama mtu akiamua.

    ndio maana nilidokeza tangu awali katika maka yangu ya awali kuwa watu wa madhehebu ya Buddha na wale wa Kihindu kwao hawajui kuhusu muda.

    Unajua ni kwa nini?

    Ni kwa sababu ya kuepuka hofu na mashaka vinavyoweza kuleta misongo ya mawazo.
    Kuendesha na muda ni kujitafutian presha za bure ndugu yangu.

    Dada YASINTA, hao wazungu unaowasema nao washashitukia jambo hilo, ni vile tu hawawezi kubadilika kirahisi namna hiyo,
    Jambo lililopandwa vichwani mwao kwa karne na karne, haiwezekani wakaliacha kwa haraka, lakini nao wameshaujua ukweli.
    Ahsanteni sana kwa kutoa maoni yenu.

    ReplyDelete
  4. yasinta nimekuelewa sana. yana basi limeenda barabarani ili lipakie watu lipate pesa na kuwapeleka waendapo, harafu linawaacha hatua chache kama wewe kisa? mishale ya saa zao imezunguka, mmamaaaa yaani wanaongozwa na mishale ya saa zao. kama wanaharaka si watoke nyumbani na mabasi yao matupu wakimbie mjini wawahi muda? kama wanaharaka wanaenda kufanya nini vituoni sasa? kaluse tusaidie

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi