0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Dec 9, 2008

JE HAYATI MUNGA TEHENAN ALISEMAJE JUU YA MAUAJI YA ALBINO YANAYORINDIMA HAPA NCHINI?

Leo nimeona niweke makala hii ya Hayati Munga Tehenan, aliyoitoa katika gazeti la Jitambue.
Nimeona niiweke makala hii hapa ili wasomaji na wanablog wenzangu watoe maoni yao.

ALBINO: Kisa cha kifo cha jirani.

Haikuanzia kwa albino, wala haitaishia kwao. Hii inatokana na ukweli kwamba, maisha yanajifungua na matukio ni sehemu ya kujifingua huko. Hakuna anayeweza kuzuia matukio, bali tunaweza tu kujua namna ya kuyakabili vema. Ilianzia kwa watu wenye vipara, siku za nyuma. Ikaja kwa akina bibi, ikahamia kwa watoto wa mitaani. Sasa albino ndiyo shabaha. Ni nani anaita hili la kuuawa albino na kuchukuliwa viungo vyao ni tatizo la ushirikina?Kwani ushirikina ni nini hasa? Hebu tuliite kuwa ni tatizo la ushirikina, sawa. Ni wangapi ambao kati yetu siyo washirikina? Najua wengi watasema wao siyo washirikina. Ni kutokujua tu, lakini karibu kila mmoja wetu ni mshirikina, bali wa jambo au upande ganindipo mahali tofauti ilipo, hilo tuliache kwanza. Ni nani hasa ambaye anapelekewa viungo hivyo vya albino? Ni mganga bila shaka. Kuna ushahidi kuwa ni mganga? Kama upo, hadi sasa umetoa picha kubwa kwa kiasi gani kuonesha kwamba, ni kweli kinachoendelea ni mahitaji ya mganga kwa mteja wake?

Tunapotafuta ufumbuzi wa tatizo tunaweza kuhangaika nalo kwa miaka mia moja bila kupata ufumbuzi, endapo hatutajua kiini cha kuwepo tatizo. Kwa nini iwe albino, na ni albino wa aina gani, masikini au matajiri, wasomi au wale ambao hawajasoma?Kama tukiendelea kusema albino anauawa kwa imani za kishirikina, inabidi tujenge ushahidi wenye nguvu kuunga mkono nadharia tete hiyo. Vinginevyo nasi tutakuwa ni washirikina tu, na kila kitu kitaenda kishirikina tu. Kwa nini tusione kuwa wanauawa kwa sababu nyingine? Tunapong”ang’ania sababu moja ambayo hatuna ushahidi nayo kwa kiwango kikubwa, nasi tuna upungufu.

Mtu mmoja alimwambia jirani yake kwamba, ataona. Alimwambia,’tutaona kama utafika kesho.” Ilipofika alfajiri ya hiyo kesho, wakati jirani anaenda kujisaidia, akapigwa na kitu kizito kisogoni na kufa. Polisi walipofika kwenye eneo la tikio na kuhoji majirani, waliambiwa kuhusu maneno yale ya jirani.Polisi walikimbia kwenda kumkamata jirani yule. Walimtuhumu kuwa ndiye muuaji. Jirani alikanusha kwamba, hahusiki, lakini ilikuwa vugumu kuwashawishi polisi.Alishasema hadharani na jirani wote walikiri. Ni ushahidi upi tena unahitajiwa? Yule jirani alikaa ndani ya miaka miwili akisubiri uchunguzi zaidi ukamilike.Ilitokea kama bahati kwamba, wauaji wa mtu yule wakawa wanatamba kwenye vilabu vya pombe za kienyeji. Ndugu wa mtuhumiwa akapata habari ile, wakaenda polisi kutoa taarifa. Polisi waliwakamata watu hao wanaotamba kwa kuwafungulia mashtaka, kufuatia kukiri kwamba, wao ndio waliouwa.

Walisema watu wale kwamba, walikuwa na uadui na marehemu na walikuwa wanatafuta namna watakavyomuua bila kufahamika. Ndipo waliposikia maapizo ya jirani, akimwambia marehemu kwamba, hangefika kesho. Hapo ndipo walipoona nafasi yao imafika kutimiza lengo lao. Huo kwao ndio uliokuwa muda muafaka. Mtuhumiwa au jirani aliachiwa huru. Alikaa ndani kwa miaka miwili, kila mtu akiamini kwamba, ndiye aliyemuua jirani yake. Ni polisi wa upelelezi tu ndiyo waliokuwa kwenye moto wa kushindwa kudhibitisha. Lakini, hakimu au jaji, angeweza kutafuta kapenyenye kembamba ka sheria na kumtia hatiani, kama muuaji.

Ndiyo ilivyo kwenye hili suala la albino. Hivi tumesahau kwamba, kuna wazazi, ndugu na jamaa wa albino ambao wanaamini kuwa na mtoto albino katika familia ni mkosi, aibu au tatizo kubwa? Hakuna aliyesahau jambo hilo labda ajifanye tu amesahau. Kama ni hivyo tuna uhakika wa kiasi gani kwamba, albino wote waliouawa baada ya yule wa awali kuuawa, waliuawa kwa lengo la kuchukuliwa viungo vyao kupelekwa kwa waganga? Kama uhakika upo, utakuwa ni sawa na ule wa jirani, wa kutumia kauli yake kama ushahidi. Hakuna anayeweza kusama kwa uhakika mkubwa kwamba, hao albino waliouawa hadi sasa, wameuawa kwa sababu za kishirikina.Ukisema kwa sababu, walikatwa viungo ndiyo ushahidi, utawafanya wale wote ambao ndugu zao walikufa kwa kukatwa viungo, hata kwa ajali warejee upya vifo vyao.

Kukatwa viungo hakuhusiani na ushirikina, jambazi, au kichaa, anaweza kuuawa na kukatwa viungo. Hivyo, huo ni ushahidi mwepesi. Kwenye hilila albino najikuta nikivutwa zaidi na habari ile ya jirani yetu. Isije ikawa wazazi, ndugu na jamaa wa albino wanaoamini kwamba, kuwa na mtoto albino ni mkosi, wauaji halisi. Walikuwa wanasuburi mazingira ambayo ni mwafaka kwao kutimiza haja yao ya kuondoa mkosi huo. Kumbuka, mwaka jana mwalimu mmoja kule Ruvuma alimuua mwanae mlemavu na wakati anaumwa alikuwa akisema, alikuwa akisubili mazingira muafaka kufanya hivyo. Hali ya uchumi wa wengi inabana, kila mmoja anajaribu kujiuliza tatizo na kutafuta suluhu. Kuna wale wanao amini kwamba, ni sera mbovu za nchi, kuna waoamini ni kwa sababu hawakusoma, wengine ni kwa sababu hawana mtaji na wengine ni kwa sababu wana laana au wamelogwa na wengine ni kwa sababu wameoa wake wenye mikosi.

Lakini kuna wengi wanao amini kwamba, ni kutokana na kuwa na watoto au ndugu ambao wana kasoro fulani. Kumbuka ulemavu kama albino kwa wengi bado ni kitendawili. Kwa hiyo, ni rahisi kwa wazazi au ndugu kuamini kwamba, ugumi wa hali ya maisha unasababishwa na kuwepo kwa mtoto au ndugu ambaye ni albino familia. Wengine sio hali ngumu ya maisha balihuamini kwamba, albino kwenye familia husababisha mikosi ya mara kwa mara kama kuugua, ndugu kugombana, wanandoa kuachana na mengine ya aina hiyo. Hawa wote nao ni watuhumiwa wazuri, ambao huenda kwa sasa wanaishi chini ya kivuli cha kauli ya yule jirani kwamba mwenzake hatafika kesho. Albino wa kwanza alipouawa na kudaiwa kwamba, ni kwa sababu za kishirikina, ikawa ni sawa na wale wauzaji ambao walikuwa pembeni wakasikia kauli ile ya’ hutafika kesho.”

3 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. Nakiri sikuwa msomaji mzuri wa Jitambue, lakini hizo mara chache nilizosoma sikutoka patupu.
    Aliyoyaandika Munga nayaunga mkono. Sitoongeza neno kwa sababu ntaharibu utamu.
    Lakini nitasema tu kwamba, mauaji ya albino yanaliaibisha taifa letu. Wenzetu majirani wanatumia mauaji hayo kutukejeli. Inafedhehesha sana.

    ReplyDelete
  2. Na apumzike kwa amani. Uzuri ni kwamba kazi zake aliziweka kwenye namna moja ama nyingine ya kumbukumbu na kwa nyie kuendelea kutukumbusha ni BARAKA kwake na kwetu pia.
    Blessings

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi