Nimepata ujumbe kupitia simu yangu ya kiganjani kutoka kwa wadau mbalimbali wa blog hii ya utambuzi. Ujumbe wenyewe ni wa kunipa pole na kunishauri juu ya hatua za kuchukuwa ili kuepuka usumbufu nilioupata baada ya kompiuta yangu ku crush.
Pia wapo wana blog wenzangu, Dada Yasinta Ngonyani na Bwana Fadhy Mtanga, nao walinipa pole kwa mkasa huu.
Kwa kweli toka juzi nilikuwa na wakati mgumu sana kwani nimepoteza mafaili yangu yote yakiwemo yale yenye makala zangu nilizoandaa kwa ajili ya kuibua mijadala mbalimbali ya maarifa haya ya utambuzi niliyopanga kuiweka humu.
Ukweli ni kwamba nitajitahidi mpaka kufikia kesho niwe nimerejea kwa kasi ya speed mia moja. Kuna wakati nilitaka kuingiwa na fikra hasi kwa kujilaumu kwa kutochukuwa tahadhari, lakini nilipokumbuka habari niliyowahi kuisoma miaka kumi uliyopita ya bwana mmoja bingwa wa kutokata tamaa Mgunduzi wa balbu hii ya umeme, bwana Thomas Edison, niliona kwamba changamoto niliyopata ni ndogo sana ukilinganisha na changamoto alizowahi kupata huyu jamaa.
Labda kwa kifupi kwa wale wasiomjua Thomas Edison, huyu jamaa alifanya majaribio 1000, wakati akiwa katika mchakato wa kugundua Balbu. Ingawa wakati mwingine watu wanatofautiana ki takwimu katika kuelezea habari zake, lakini mimi kitabu nilichosoma kinasema alifanya majaribio 1000 ya kutengeneza balbu ndipo akafanikiwa kuwasha hii balbu ya umeme tunayotumia,
Hebu fikiria majaribio 1000 ndio ufanikio, ajabu ee!!
Pia katika majaribio hayo alikuwa anapata vikwazo kadhaa, lakini tukio mojawapo kubwa ni lile la maabara yake kuungua na hivyo kupoteza mafaili yake yote ya kumbukumbu za ugunduzi wake. Cha kushangaza wakati anaangalia yale majivu ya makabrasha yake aliwaambia wasaidizi wake kuwa imekuwa vyema yale mafaili yaliyohifadhi kumbukumbu za majaribio yake yaliyoshindwa yameungua kwa hiyo hakuna haja ya kuhangaika na majaribio yaliyoshindwa na badala yake waanze upya.
Si hivyo tu bali alikiri kwamba katika majaribio hayo pia amejifunza kushindwa!
Baadae ndipo wakafanikiwa kuwasha balbu.
Je umeona jinsi mtu huyu alivyo na akili za ajabu?
Hivi ni mara ngapi sisi tunakwama katika shughuli zetu na kujipongeza japo kwa kushindwa kwetu?
Katika makala ya hivi karibuni ya mwanablog Bwaya alizungumzia kitu kinachoitwa Dialectic Thinking. Alisema kila jambo lina pande mbili, kwa mfano kama kuna kushinda basi kuna kushindwa, na kama kuna kupata, kuna kukosa pia.
Mifano iko mingi sana.
Lakini swali la msingi hapa ni, je tumefundishwa nini kuhusiana na hizi pande mbili?
Je ni kweli kuna upande mbaya na mzuri?
Ni nani aliyekufundsha hivyo?
Ukweli ni kwamba hakuna upande mbaya katika kila jambo, bali tafsiri zetu ndizo zinazotupotosha.
Kufanikiwa na kutokufanikiwa kwa jambo lolote ni mojawapo ya changamoto za kujifunza. Tunaweza kujifunza kutokana na kufanikiwa na pia tunaweza kujifunza kutokana na kutofanikiwa. mimi nimejifunza kutokana na chanagamoto hii ya compiuta yangu ku Crush.
Je kuna haja ya mimi kujilaumu?
Hapana, sidhani kama kuna haja ya kujilaumu bali najipongeza sana kwa mafanikio niliyofikia tangu nilipofungua blog hii ya utambuzi, kwani naamini wapo wasomaji na wana blobg wenzangu wamejifunza mengi kupitia blog hii kama vile na mimi nilivyojifunza mengi kupitia maoni yao na michango yao mbalimbali waliyoitoa katika blog hii.
Si hivyo tu, bali pia nimejipatia marafiki kadhaa wengi wakiwa ni wanablog wenzangu na nimejifunza mengi kupitia blog zao.
Naomba radhi kwa usumbufu uliotokea, nawatakia sikuku njema.
Dec 8, 2008
BADO TUPO PAMOJA!!!!!!!!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
mawazo mazuri sana kwani hicho kitabu itabidi wengi wasome, maana ulivyojieleza tu inaonekana ni kitabu kizuri sana. Kwa sababu kuna wengi sana ambao wana hasira na tena zile za haraka. Hawajajua kuwa HASIRA HASARA pia hawajua kuna kupata na kukosa.
ReplyDeleteasante sana kwa mada nzuri nimejifunza kitu.
Nianze kwa kumnukuu Dr. Martin Luther King Jnr, wakati fulani alipata kusema, "I say to you today, my friends, that inspite of the difficulties and frustrations of the moment, I still have a dream." Hii ni hotuba maarufu sana ya mwanaharakati huyu wa usawa dhidi ya ubaguzi.
ReplyDeleteAlikuwa na ndoto. Bwana Kaluse naye ana ndoto, kwamba pamoja na changamoto anazokumbana nazo kwa kompyuta iliyomhini, siku moja mambo yatakuwa sawa.
Napenda kukupa pole kwa mara nyingine. Lakini unapaswa kufarijika kama utarejea kauli ya Dr. Kenneth Kaunda, wakati fulani akiwa katika siku za mwambo, alipata kusema, "troubles strengthen the mind as work does to the body."
Kumbe unavyosugua kichwa namna ya kuiponya kompyuta yetu, ndivyo unavyokomaa kimawazo. Hupaswi kukata tamaa. Na nakuamini, hukati tamaa.
Hukati tamaa kwa sababu bwana mmoja, Henry Ford alisema siku moja, "failure is the chance to begin again more intelligenly." Hivyo tunaamini, ukirudi, kasi yake, uzito wake, hizo fikra zako chanya hautapimika wala kukadirika.
Huku ni kukwama kwa wakati mfupi tu. Kukwama huku kuna umuhimu wake. Umuhimu huwa nauona kila ninaporejea usemi wa mshairi mmoja wa zamani wa Uingereza. Mshairi huyo Robert Browning alisema, "A minute's success pays the failures of years."
Unajua nini kaka? Ikisha kupona, utayasahau masahibu yote. Nami nakupa moyo, ili kitendea kazi chetu kipone, mapambano ya kifikra kwa ujenzi na ustawi wa jamii yetu uendelee.
Nakutakia mafanikio ili urejee haraka.
Ni hayo tu!
Pole sana Kaka Shaaban na pia SHUKRANI kwa Da Yasinta na Kaka Fadhy na wale wote ambao kama mimi hawajaweza kutoa maoni kwa muda muafaka kulingana na mambo mbalimbali. Nikirejea kwako na namna ya kujilaumu kwenye kile tuonacho kama maanguko, napenda kumnukuu MPIGANAJI Nelson Mandela aliposema "The Greatest Glory In Living Lies Not In Never Falling, But In Rising Every Time We Fall" Sina mengi ya kusema maana umeelezea haya yote bila hata kunukuu kauli hii. Umesema utarejea kwa speed 100 na waweza kuona kuwa hiyo tayari ni Greatest Glory. Kwa kuharibikiwa kwa PC yako umekumbuka kutufunza juu ya mtengenezaji wa balbu nami nime-search na kupata mawili matatu juu yake ambayo yamekufanya usikate tamaa nami pia sitakata tamaa kwenye harakati zangu. Umeona fahari ya yale uliyokuwa ukifanya na sasa unajua kuwa una kazi ya ziada kurejesha yale ufanyayo kwa nguvu zaidi.
ReplyDeletePole sana Shebbie, lakini kwa hakika najivunia moyo na hatua zako za kutokata tamaa.
Blessings