0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Dec 7, 2008

MAJUMUISHO YA MAKALA YA MUDA YAMEOTA MBAWA!!!!!!!!!

Compiuta ime Crash
Wasomaji wapendwa, tangu juzi nilikuwa naandaa majumuisho ya makala ya muda ambayo niliiweka hapa na kupata changamoto toka kwa wadau mbalimbali, lakini kwa bahati mbaya compiuta yangu imeingia virusi ambavyo vimetafuna mafaili yangu yote.

Kibaya zaidi virusi vyenyewe nilivibeba na flash disc, ambayo nayo imekwenda na maji, imekuwa kaputi.

Jana kutwa nzima nilikuwa na fundi wangu akijaribu kuinusuru, kwa kuifomati na kuweka windo mpya, kazi ambayo ilikamilika jioni kabisa.

Naomba msibabaike, naamini kila kitu kitaenda sawa kwani natarajia mpaka kesho nitarejea ulingoni.

4 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. Pole sana Shambani nategemee kila kitu kitaenda safi. kila la kheri

    ReplyDelete
  2. Pole sana kaka, maendeleo huja na mamboleo. Tunasubiri kwa hamu urejeo.

    ReplyDelete
  3. Ahsante sana dada yasinta na kaka Mtanga,

    Kwa kweli toka juzi nilikuwa na wakati mgumu sana kwani nimepoteza mafaili yangu yote yakiwemo yale yenye makala zangu nilizoandaa kwa ajili ya kuibua mijadala mbalimbali ya maarifa haya ya utambuzi niliyopanga kuiweka humu.

    Ukweli ni kwamba nitajitahidi mpaka kufikia kesho niwe nimerejea kwa kasi ya speed mia moja.
    Kuna wakati nilitaka kuingiwa na fikra hasi kwa kujilaumu kwa kutochukuwa tahadhari, lakini nilipokumbuka habari niliyowahi kuisoma miaka kumi uliyopita ya bwana mmoja bingwa wa kutokata tamaa mvumbuzi wa balbu hii ya umeme, bwana Thomas Edson, niliona kwamba changamoto niliyopata ni ndogo sana ukilinganisha na changmoto alizowahi kupata huyu jamaa.

    Labda kwa kifupi kwa wale wasiomjua Thomas Edson, huyu jamaa alifanya majaribio 1000, ingawa wakati mwingine watu wanatofautiana ki takwimu katika kuelezea habari zake, lakini mimi kitabu nilichosoma kinasema alifanya majaribio 1000 ya kutengeneza balbu ndipo akafanikiwa kuwasha hii balbu ya umeme tunayowasha,

    Hebu fikiria majaribio 1000 ndio ufanikio, ajabu ee!!
    Pia katika majaribio hayo alikuwa anapata vikwazo kadhaa, lakini tukio mojawapo kubwa ni lile la maabara yake kuungua na hivyo kupoteza mafaili yake yote ya kumbukumbu za ugunduzi wake, cha kushangaza wakati anaangalia yale majivu ya makabrasha yake aliwaambia wasaidizi wake kuwa imekuwa vyema yale mafaili yaliyohifadhi kumbukumbu za majaribio yake yaliyoshindwa yameungua kwa hiyo hakuna haja ya kuhangaika na majaribio yaliyoshindwa na badala yake waanze upya.

    Si hivyo tu bali alikiri kwamba katika majaribio hayo pia amejifunza kushindwa!
    Baadae ndipo wakafanikiwa kuwasha balbu.

    Je umeona jinsi mtu huyu alivyo na akili za ajabu?

    Hivi ni mara ngapi sisi tunakwama katika shughuli zetu na kujipongeza japo kwa kushindwa kwetu?

    Katika makala ya hivi karibuni ya mwanablog Bwaya alizungumzia kitu kinachoitwa Dialectic Thinking.
    Alisema kila jambo lina pande mbili, kwa mfano kama kuna kushinda basi kuna kushindwa, na kama kuna kupata, kuna kukosa pia, mifano iko mingi sana.

    Swali la msingi hapa ni je tumefundishwa nini kuhusiana na hizi pande mbili?

    Je ni kweli kuna upande mbaya na mzuri?

    Ni nani aliyekufundsha hivyo?

    Ukweli ni kwamba hakuna upande mbaya katika kila jambo, bali tafsiri zetu ndizo zinazotupotosha.

    Kufanikiwa na kutokufanikiwa kwa jambo lolote ni mojawapo ya changamoto za kujifunza. Tunaweza kujifunza kutokana na kufanikiwa na pia tunaweza kujifunza kutokana na kutofanikiwa. mimi nimejifunza kutokana na chanagamoto hii ya compiuta yangu ku Crush.

    Je kauna haja ya mimi kujilaumu?

    Hapana, sidhani kama kuna haja ya kujilaumu bali najipongeza sana kwa mafanikio niliyofikia tangu nilipofungua blog hii ya utambuzi, kwani naamini wapo wasomaji na wana blobg wenzangu wamejifunza mengi kupitia blog hii kama vile na mimi nilivyojifunza mengi kupitia maoni yao michango yao mbalimbali waliyoitoa katika blog hii.

    naomba radhi kwa usumbufu uliotokea, nawatakia sikuku njema.

    ReplyDelete
  4. Pole sana kaka. Nadhani hupaswi kujilaumu. Kwa sababu hata kama ungejilaumu bado hakuna kinachoweza kubadili ukweli kwamba mafaili yameharibika. Pole sana. Jipe moyo. Tunakusubiri kwa hamu.

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi