Huu ni mchango wa mwanablog mkongwe Bwaya, juu ya mada niliyoiandika kuhusu watu kujali muda. Nimeona niiweke hapa barazani ili wasomaji wengine watoe changamoto, kwani naona mada hii imeamsha hisia za wasomaji wengi.
Nikinikuu mojawapo ya makala alizoandika mwanzuoni huyu Bwaya, kwamba hakuna kujifunza bila kutofautiana, nami nakubaliana naye, juu ya kauli yake hiyo.
Jamani kutofautiana sio dhambi nakaribisha maoni zaidi.......
**********************************************
Nadhani kuna haja ya kuangalia kwa mapana zaidi maana hasa ya muda. Muda ni nini? Mimi nautazama muda kama kielelezo cha badiliko. Kama hakuna badiliko maana yake hakuna muda.
Kwa sababu muda maana yake ni hesabu ya tofauti ya badiliko moja na lingine.Penye badiliko la haraka maana yake muda kwa mukhtadha huo, utakuwa mfupi kuliko penye badiliko la taratibu.
Kwa hiyo muda unatokana na badiliko. Milele, ni dhana ya kutokuwapo badiliko. Yaani yalivyo leo, ndivyo yatakavyokuwa kesho na kesho kutwa. Kwa hivyo, muda hapo unakuwa sifuri.Mtu anapokufa, kwake muda ni sifuri hata kama saa yake inakuwa bado inatembea. Sababu ni kwmaba mwili wake hauna badiliko lolote la kibaolojia.
Na tumekwisha kutangulia kusema kwamba muda haupo bila badiliko.Kwa hivyo, tunaweza kusema, wazo kwamba muda uligunduliwa si sahihi. Muda haukugunduliwa. Muda ulikuwapo tangu badiliko la kwanza lilipoanza.
Kidini, uumbaji ulipofanyika.KInachoonekana kugunduliwa (kwa maana ya juu juu) ni namna ya kuhutathimini muda. Kwmaba sayansi imetuwezesha kuwa na njia za kimakenika kuutathimini muda haimaanishi kwamba muda umegunduliwa.
Vile vile wazo kwamba tufanye mambo yetu bila kutilia maanani muda nadhani linahitaji kutazamwa kwa tahadhari hata kama linaonekana kuwa na mantiki kisaikolojia. Sababu ni kwamba kutathimini muda, iwe kwa kutumia njia za kimakenika ama za asili, hutusaidia kuyatekeleza majambo hayo kwa kuzingatia kuwa na sisi kama viumbe tuna badilika na kuna siku tutakoma kubadilika.
Kama ingekuwa kwmaba hatubadikili, wazo la kutokuzingatia muda lingekuwa na nguvu. Lakini ni bahati mbaya kuwa sivyo ilivyo.Tofauti ya mawazo ni msingi wa mjadala. Asante kwa kazi nzuri ya kupangilia mjadala.
Wednesday, December 03,
Dec 3, 2008
MCHANGO WA BWAYA JUU YA MADA HII YA MUDA, NAOMBA KUWASILISHA........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Yap kaka,
ReplyDeletenimekusoma vema. Muda ni kitu cha msingi katika badiliko lolote lile. Labda tuseme, kutoka katika hali fulani moja hadi hali fulani nyingine kuna kitu kinachokuwa kinapotea hapo. Ni muda.
Muda ndiyo unaoratibu mabadiliko na shughuli za maisha za wanadamu na vyote vilivyomo katika ulimwengu.
Kama hapana muda, jambo litakuwa static. Lakini hapana shaka watu huwa hatujui umuhimu wa muda katika uratibu wa shughuli zetu kadha wa kadha, pengine hadi muda uwe unatutupa mkono.
Ni hayo tu!
Samahani bwana Mtanga. Naomba nikuulize: Je, ni kwa namna gani muda unaratibu mabadiliko? Ama niseme muda unawezaje kuratibu shughuli kama ulivyosema? Naomba ufafanuzi.
ReplyDeleteAsante.