0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Dec 1, 2008

KWA NINI MUDA UKUENDESHE?

Kwao hakuna kitu kinachoitwa muda.
Nilipoandika kuhusu mwili wa hisia, bwana Kitururu alikuja na hoja kwamba, ni vigumu sana kwetu kuuratibu mwili wa hisia kwa sababu ya ubize wa shuguli zetu za kila siku. Ukweli ni kwamba nilipinga hoja yake. Kwa nini?.
Kwa sababu wanaadamu wamejilundikia majukumu mengi kutokana na ushindani, kila mtu siku hizi anataka kushindana, katika kutafuta kuuridhisha mwili, ambao nao kamwe hauridhiki. Watu wanaishi kwa utashi na si kwa uhitaji, na ndio sababu ya tunashuhudia watu wakisingizia kuwa bize au kukimbizana na muda kutokana na mikanganyiko ya majukumu waliyojiwekea.

Kuna wakati niliwahi kusoma habari za watu wa imani ya Kihindu na wale wa imani ya Buddha, ambao kwao suala la muda au kuwa bize haliko, yaani hakuna kitu kinachoitwa muda kwenye maisha yao. Nami nakubaliana nao. Kuna wanaoamini kuwa muda ni pesa, au wanoamini kwamba muda una nguvu na unahitaji kutumiwa kwa njia ambayo inaonyesha kwamba unapewa heshima yake, ambayo ni lazima iwe kubwa kuliko binadamu mwenyewe.

Mtu asipokuwa makini anaweza kukubaliana kabisa na kauli au dhana hizi ambazo kwa nje zinaonekana zina uzito, wakati kwa ndani hazina kitu, ni tupu. Ni kauli au dhana ambazo zinaashiria kwamba, muda ulivumbuliwa na sio kwamba uliumbwa na binadamu.
Naamini unafahamu tofauti kati ya kuvumbua na kuumba. Kwa kawaida tunavumbua kitu ambacho ni cha kimaumbile na kilikuwepo siku zote, isipokuwa hakuna aliyekuwa amebaini kuwepo kwake. Kuumba ina maana ya kutengeneza kitu ambapo hapo awali hakikuwepo au kilikuwepo na kinatengenezwa tena na tena.
Binadamu alivumbua muda, kwani haukuwepo hapo awali. Mungu hakutengeneza kitu kinachoitwa sekunde, dakika, saa, siku, wiki, mwezi, mwaka, muongo, karne na vyote unavyovijua vyenye kupima muda. Mungu alitengeneza vile vitu ambavyo binadamu anadhani vilitengenezwa kwa sababu ya kupima muda. Wanatumia mzunguko wa dunia kwenye mhimili wake wa kulizunguka jua kama kipimo cha muda.

Lengo la mungu kufanya mizunguko hiyo haikuwa kupata muda, bali kitu kingine kabisa. Ndio maana suala la muda limeanza juzi tu, binadamu akiwa tayari ni mjanja. Kuna kuishi na kutenda yale ambayo mtu anaamini ndio yaliyomleta hapa duniani, lakini hakuna muda. Binadamu amevumbua muda kwa lengo la kujipa maradhi ya moyo, hofu na mashaka. Amevumbua muda katika hofu zake za kukabili kutokujua kwake amekuja hapa duniani kufanya nini. Kwa sababu ya muda anakwambia, “maisha ni mafupi sana”, au “ponda mali kufa kwaja”

Kama ukiweza kuishi bila kujali muda, unaweza kuanza kuhisi tofauti. Nikisema kuishi bila kujali muda, sina maana kwamba ukiambiwa umalize kazi uliopewa leo ukatae, hapana. Sisemi kwamba ukiambiwa mradi uliopewa ukamilike mwezi ujao, useme, “nitakamilisha siku yoyote’, hapana. Unapaswa kukumbuka kwamba ni wajibu wako kufanya kwa juhudi, kufanya kwa dhamira na kujitolea zaidi na zaidi, na sio juu yako kuendeshwa na muda wa mwisho uliopewa kukamilisha mradi huo (deadline)

Kama umefanya na imefikia mahali huwezi kukamilisha kwa kadiri ya muda uliojiwekea, au uliopewa, basi huna haja ya kujiuwa. Kama ni kazi yako, unajua namna ya kujiambia , na kama ni kazi ya mtu, ni suala la kujieleza na kujionesha ni kwa nini umeshindwa kwenda kwa mujibu wa ulivyotaka wewe. Kumbuka kwamba dunia hii imekuwepo na ilibeba watu, wanyama na mimea ya kila aina, lakini imepita yote. Hata kama utafanya usiku na mchana na asubuhi na jioni ili kuwahi muda usiishe, utaondoka nawe pia, ukiwa hujamaliza unayotaka kumaliza.


9 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. ndio maana wadhungu wanasema no hurry in africa. wazungu ni watumwa wa muda wakati waafrika ni mabwana wa muda kwamba waafrika wanamuda na kila kitu kinawezekana. hatujaumbwa kuishi kwa wasiwasi na mashaka bali kwa utulivu na upendo

    ReplyDelete
  2. NI kweli kabisa haraka haraka haina baraka pole pole ni mwendo. Naipenda Afrika yangu hakuna mambo ya mimi nitafika kwako saa saba kamili. Kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  3. Ukweli binafasi mawazo yangu ni tofauti kwani naamini suala la muda ni muhimu sana, kwa nini kazi ya miezi 6 ufanye kwa miaka 6 na utegemee kupata mafanikio?
    Suala ni kukubali kwamba tunahitaji muda tuutumikie sisi na kupanga muda kwa ajili ya familia, kpumzika, kazi na kufurahia maisha. Siyo kuwa busy tu kwa jina la muda.
    Mawazo yangu tu!

    ReplyDelete
  4. Ahsnteni wote kwa maoni mazuri, Kamala, Dada Yasinta, na Bwana Mbilinyi.
    Nimefurahishwa sana na maoni yenu kwa ujumla.
    Kama mkisoma makala yangu kwa makini mtaelewa nilikuwa namaanisha nini.
    Sikusema ukipewa kazi na kupangiwa muda (ingawa kiutambuzi haupo)wa kukamilisha kazi hiyo basi uifanye taratiiibu bila kujali huo muda uliopangiwa. hapana sikumaanisha hivyo ndugu zangu.
    Hivi, hebu tujiulize sisi sote, kabla muda haujavumbuliwa, Je wanaadamu walikuwa wanafanyaje kazi?
    Je walikuwa wakipewa kazi wanafanya taratibu kwa sababu kulikuwa hakuna kitu kinachoitwa muda? au walikuwa wanafanya kazi kwa bidii bila kujali kwa sababu muda ulikuwa haujavumbuliwa?
    Bado tunayo safari ndefu sana ya kujitambua, na ninaamini taratibu kwa jinsi ninavyoendelea kuelimisha juu ya maarifa haya hatimaye watambuzi watakuwa wengi.
    Naomba mrejee kusoma tena na tena makala hiyo, naamini ina maarifa yatakayowasaidia kuujua ukweli huu kwamba katika utambuzi hakuna kitu kinachoitwa muda, bali kuan kukamilisha kile ulichopanga au kupangiwa kukikamilisha.

    Bado nahitaji changamoto zenu.

    Pamoja tunawakilisha

    ReplyDelete
  5. Kazi nzuri kwa jinsi unavyoandika makala zako.

    tutafika tu

    ReplyDelete
  6. Nadhani kuna haja ya kuangalia kwa mapana zaidi maana hasa ya muda. Muda ni nini?

    Mimi nautazama muda kama kielelezo cha badiliko. Kama hakuna badiliko maana yake hakuna muda. Kwa sababu muda maana yake ni hesabu ya tofauti ya badiliko moja na lingine.

    Penye badiliko la haraka maana yake muda kwa mukhtadha huo, utakuwa mfupi kuliko penye badiliko la taratibu.

    Kwa hiyo muda unatokana na badiliko.

    Milele, ni dhana ya kutokuwapo badiliko. Yaani yalivyo leo, ndivyo yatakavyokuwa kesho na kesho kutwa. Kwa hivyo, muda hapo unakuwa sifuri.

    Mtu anapokufa, kwake muda ni sifuri hata kama saa yake inakuwa bado inatembea. Sababu ni kwmaba mwili wake hauna badiliko lolote la kibaolojia. Na tumekwisha kutangulia kusema kwamba muda haupo bila badiliko.

    Kwa hivyo, tunaweza kusema, wazo kwamba muda uligunduliwa si sahihi. Muda haukugunduliwa. Muda ulikuwapo tangu badiliko la kwanza lilipoanza. Kidini, uumbaji ulipofanyika.

    KInachoonekana kugunduliwa (kwa maana ya juu juu) ni namna ya kuhutathimini muda. Kwmaba sayansi imetuwezesha kuwa na njia za kimakenika kuutathimini muda haimaanishi kwamba muda umegunduliwa.

    Vile vile wazo kwamba tufanye mambo yetu bila kutilia maanani muda nadhani linahitaji kutazamwa kwa tahadhari hata kama linaonekana kuwa na mantiki kisaikolojia. Sababu ni kwamba kutathimini muda, iwe kwa kutumia njia za kimakenika ama za asili, hutusaidia kuyatekeleza majambo hayo kwa kuzingatia kuwa na sisi kama viumbe tuna badilika na kuna siku tutakoma kubadilika. Kama ingekuwa kwmaba hatubadikili, wazo la kutokuzingatia muda lingekuwa na nguvu. Lakini ni bahati mbaya kuwa sivyo ilivyo.

    Tofauti ya mawazo ni msingi wa mjadala. Asante kwa kazi nzuri ya kupangilia mjadala.

    ReplyDelete
  7. Haya, The Saga Continue.

    Ahsante sana bwana Bwaya kwa mchango wako.
    Naona nimechokoza hisia za watambuzi na watambuaji.
    bado nahitaji changamoto zaidi.
    Karibuni sana.

    ReplyDelete
  8. Kwa yoyote anaetaka kufanikiwa ni lazima ajali swala la mida, na ndio maana hao mabudha ni maskini na washamba sana, Mimi binafsi najali muda na ndio maana nafanikiwa.

    ReplyDelete
  9. time z money jamani huwezi kufanikiwa kama hautotunza mda

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi