0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Jun 12, 2009

SEMINA ZA UTAMBUZI KUANZA JULY 2009

Wanafunzi wa Utambuzi wakiwa darasani pale Kimara Rombo

FAMILIA YA JITAMBUE – FAJI

SEMINA ZA ELIMU YA UTAMBUZI

Familia ya Jitambue (FAJI) ni Umoja wa Wananchi wa Tanzania wanaojishughulisha na maarifa ya utambuzi. FAJI ni Taasisi iliyosajiliwa Mwaka 2007 yenye namba ya Usajili 15579 chini ya Msajili wa Jumuiya, Wizara ya Mambo ya Ndani.

Utambuzi ni maarifa yanayolenga kumuwezesha mtu kubaini kuhusu yeye na yanayomzunguka ili aweze kukua, Kimwili, Kiakili, Kihisia na Kiroho. Kwa kuyapata maarifa hayo yanamuwezesha kuachana na mazoea yanayomuumiza na kuumiza wengine; kukabiliana na vikwazo, vurugu na changamoto mbalimbali za kimaisha; kufikiri vizuri, kujiamini, kuwa mbunifu, kufikia malengo yake na hivyo kujiletea mabadiliko katika maisha yake na maendeleo ya jamii kwa ujumla. Pia humfanya mtu awe na ufahamu yakinifu wa ubinadamu wake na hivyo kuweza kuishi maisha yenye Furaha, Amani, Utulivu na Upendo wa kweli. Kujifunza maarifa hayo huhitaji kuwa na sifa yoyote maalumu kama cheti cha shule, umri, jinsia, dini, imani nk. Kitu kikubwa ni uwezo wako wa kuyatekeleza unayojifunza kwa vitendo.

Kwa sasa FAJI inajishughulisha kusambaza maarifa hayo kupitia vyombo mbalimbali vya habari pamoja na Madarasa yaliyopo kwenye Kituo cha FAJI Kimara Rombo Dar es Salaam.

Maarifa haya pia yanatolewa kwa njia ya Semina kwenye Shule, Vyuo, Taasisi na Mashirika mbalimbali.

Baadhi ya mada zinazofundishwa ni:-

Namna ya kupata utajiri pamoja na mafanikio katika biashara, kiuchumi, kazini na shuleni; namna ya kujenga mahusiano mema kazini na upendo wa kweli katika ndoa, suluhu ya tendo la ndoa; namna ya kujiamini; kuondoa msongo wa mawazo, chuki, kijicho na hasira za ziada; kinga ya uchawi; namna ya kupata chochote utakacho maishani; kuondoa tabia sugu kama ulevi, uvutaji sigara n.k., kuondoa hofu na aibu, kupata afya nzuri kimwili kwa njia ya tiba mbadala, kufikiri vizuri, n.k.

Tunafundisha mada nyingi zaidi ya zilizotajwa hapo juu.

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia:
Sanduku la barua namba 22040 Dar es Salaam. Simu namba 0715 627003 au 0784771301 na 0713 250701, Email – faji.jopo@gmail.com au fika katika kituo cha FAJI kilichopo barabara ya Morogoro Kimara Rombo na utaliaona Jengo la Taasisi ya FAJI kulia kwako ukiwa unatokea Ubungo.

6 comments:
Andika Maoni Maoni
 1. Bwana Kaluse. Ningekuwa huko ningejaribu sana kuhudhuria semina hizi kwani Kamala amenipa tamaa kubwa ya mimi pia kujitambua. Nikikaribia kuja huko tutawasiliana. Endelezeni kazi hiyo njema iliyoanzishwa na Munga Tehenan!

  ReplyDelete
 2. Ni kweli watu wengi wangehitaji kuhudhuria hii semina. Lakini nina imani tutapata yote kupitia/kusoma hapa kwa kaka Shabani pia Kamala. Ubarikwe

  ReplyDelete
 3. Kaka Masangu na dada Yasinta,

  Hizi semina ni za kudumu, na sasa tumepanua wigo wa kufundisha mpaka vyuoni bila kujali viwango vya elimu kwani maarifa haya ni zaidi ya taaluma nyingine unazozifahamu.
  Pia tuko katika mchakato wa kutoa mafunzo haya kwa njia ya posta (Distance Leaning), kwa njia ya CDs, majarida, redio na TV.

  Bado tunazo changamoto nyingi za kuweza kumudu gharama za uendeshaji wa mafunzo haya lakini kwa kutumia nguvu zetu wenyewe bila ufadhili kutoka nje tumeweza kufikia hapo tulipo.

  Hayo ndiyo malengo tuliyojiwekea na tunaamini tutamudu, na semina hizi zitawanufaisha wengi.
  Karibuni sana

  ReplyDelete
 4. Hi muhimu na hongereni kwa kulifanyia kazi!

  ReplyDelete
 5. Pengine maelezo haya yanaweza kuwasaidia wale ambao kwa fikra fupi wanaamini kuwa UTAMBUZI ni DINI fulani inayopingana na karibu kila kitu katika dini za kisasa. Yaani kuweza kujitambua na kisha kujiuliza "faida na hasara" ama "ukweli na uongo" wa kila utakacho kufanya wengine wanakuona m'bishi.
  Sijui ni wapi wanapoona mstari mwembamba wa ubishi na utashi wa uelewa?
  Asante saaana na tutaendelea kuwasiliana ili kujua namna ya kupokea madarasa kwa njia ya "mbali"
  BARAKA KWENU

  ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi