Kama kubaka ni hali ya mwanaume au mwanamke kulazimisha kufanya tendo la ndoa bila hiyari ya mwingine, basi wanawake wengi sana walioko kwenye ndoa hubakwa na waume zao kila siku.
Kubakwa huku kunatokana na ukweli kwamba wanawake wengi hulazimika kukubali kufanya tendo la ndoa na waume zao kutokana na mazingira mbalimbali yaliyo nje ya upendo.
Kuna ndoa nyingi ambazo zimekufa, ingawa wanandoa wanaishi pamoja. Zimekufa kwa sababu hazina mawasiliano kabisa. Lakini cha ajabu ni kwamba, watu hawa wanakutana kimwili na pengine kuzaa watoto. Kwa sehemu kubwa kwenye ndoa za aina hii, wanawake huwa hawako kwenye ukamilifu wao kimawazo.
Mara nyingi athari huwa ni kwa wanawake kwa sababu wao kimaumbile huishi kihisia. Kutokana na kuathirika kimawazo hamu yao ya kushiriki tendo la ndoa nayo hupotea.
Kwa kuwa hawana hamu ya kushiriki tendo la ndoa, waume zao wanapowaambia, ‘geuka huku’ (hawaongei zaidi ya hapo kwa sababu hakuna mawasiliano), hufanya hivyo. Na hufanya hivyo huku wakiwa hawataki.
Sio wengi wanaoweza kukataa kwa sababu hawakulelewa katika mazingira yanayoweza kuwafanya wakatae. Wamelelewa kwenye mazingira ambayo yamewaambia, miili yao hawana haki nayo mbele ya utashi wa waume zao!
Ukiacha mawasiliano kuna ndoa ambazo wanaume ni Malaya sana, walevi, au wapigaji. Kwenye ndoa za aina hii unaweza kukuta mwanamke bado anaendelea kuwepo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo ya utegemezi au watoto. Pamoja na kuendelea kwao kuwepo, hamu ya tendo la ndoa na waume zao nayo inakuwa haipo
Lakini mwanaume hatakiwi kunyimwa mwili wake anapouhitaji. Kwa hiyo, kinachotokea ni mwanamke kufanya mapenzi kwa kujilazimisha au kulazimishwa..
Kuna kesi nyingi ambapo tumesikia juu ya wanaume kuwauwa wake zao kutokana na kuwakatalia unyumba au wakiwa wanapigana baada ya mwanamke kukataa kushiriki tendo la ndoa.
Kwenye ndoa nyingi wanawake hubakwa, yaani hushiriki tendo la ndoa bila hiyari zao. Hulazimishwa au hujilazimisha kutokana na nafasi ambayo jamii imewapa.
Ni kwa nini basi tunapozungumzia kubaka tusiwaambie wanawake na kuwashauri wawe macho na ubakaji huu ambao una athari kubwa kwao na kwa jamii wakiwemo watoto wanaozaliwa kwenye ndoa hizi za kibabe?
Kaka Shabani hapa umenena, unajua wanawake wengi wanalijua hili ila kitu kinachowaponza/tuponza ni woga. Kuna kitu umenikumbusha ambacho kilinichafua sana nilipokuwa nyumbani ngoja nikitulia nitakifanyia kazi... Kwa kweli wanawake sijui hizi huruma zetu tulizonazo? Mungu wape ngungu wanawake.
ReplyDelete!!!!!!!
ReplyDeleteNa ile ishu ya wanawake wa Zimbabwe kubaka wanaume......
ReplyDeleteHalafu nasikia kwa sheria za Zimbabwe, haitambui kuna suala la mwanamke kumbala mwananume, ila inatambua mwanamke kubakwa na mwanaume.
Mwaka huu wanawake waliowabaka wanaume huko Zimbabwe, walikuwa wanapewa maonyo ya mdomo au faini ndogo ndogo kwa shambulio shurutishi.
Nawashauri kina dada kuwa dawa ya ndoa za namna hii ni kujitoa.
ReplyDelete