0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Dec 19, 2008

JE WANASAYASI WANASEMA UKWELI KUHUSU MWANZO WA MWANAADAMU?

Mada ya Yasinta aliyoipa kichwa cha habari kisemacho, Je Binadamu na Nyani ni jamii moja? imenifanya na mimi nifungue mjadala mpya.

Kuna wakati nilisoma habari iliyoandikwa na Bwana
Bwaya juu ya sayansi ya viumbe aliyoipa kichwa cha habari kisemacho;
Viumbe na mabadiliko ya “kubahatisha”

Naomba ninukuu maelezo ya makala hiyo hapa chini;
‘Marehemu Darwin amejaribu kuonyesha kwamba viumbe vilitokea kwa bahati, vikapitia mabadiliko ya uasili wao kufanya asili nyingine iliosababisha kugeuka na kuwa viumbe vya aina nyingine kabisa.Ili kufafanua anachosema Darwin na rafiki zake, tuchukulie mfano wa viumbe kama samaki.

Samaki, kwa mujibu wa kanuni ya “natural selection”, walipitia mageuzi kadhaa yaliyosababisha tofauti katika kundi lao la samaki. Tofauti hizi ziliendelea kuwa kubwa kiasi cha kusababisha kutengenezeka kwa aina fulani ya samaki waliokuja kufanya kundi la viumbe tofauti kabisa na samaki wengine waliobaki.

[Kundi hili linafahamika kama amphibia lenye mifano ya viumbe kama mamba na vyura].

Maana yake ni kwamba katika samaki, walitokea samaki waliokataa asili yao na kufanya asili nyingine iliyosababisha kutokea kwa viumbe vingine. Utetezi wa mabadiliko haya yanayosemwa na akina Darwin, ni mazingira. Kwamba samaki hawa, kwa mfano, waliishi katika mazingira yanayotofautiana kiasi cha kugeuka kwa asili yao.

Kwamba asili hugeuzwa na mazingira kwa maana ya samaki kubadili tabia zake ili kuendana na mabadiliko ya mazingira alimo, ni jambo ambalo linatupasa kufikiri kwa tahadhari.Kwamba asili ya kiumbe ndiyo inayomsaidia kugeuka ili kukabidili mabadiliko katika mazingira yake na kwamba asili yake ilibadilika, ikimtenga na wenzake, ili kufanya kundi lingine linalojitegemea la viumbe jamii nyingine, hilo si jambo rahisi’.

Kisha akaendelea kusema katika makala nyingine aliyoipa kichwa cha habari kisemacho:
Fossil kwa sababu gani?

Katika makala hiyo alisema, naomba kunukuu:

‘Kwa mfano inavyoonekana, maisha hasa ya viumbe yalianzia baharini. Kwa maana hii, viumbe wa kwanza waliishi majini wakibadilika badilika na kuishia kufanya aina nyingine ya maisha yasiyotegemea maji, yaani maisha ya nchi kavu. Sasa katika kuangalia mlolongo huu, tunaambiwa viumbe walijikuta wakijiongezea “viungo” (adaptive features) vilivyowawezesha kukabiliana na aina vyingine ya maisha’

Kisha akaendelea kuandika:

’Kwa ule mfano wetu wa samaki, ni kwamba baadhi ya samaki walianza kupoteza uwezo wao wa kupumua kwa kutegemea maji, na badala yake, wakaanza kuwa na vitu kama mapafu vilivyowasababisha kugeukia maisha nje ya maji. Baadae makoleo yao yaliyotumika kuogelea (fins) yakatengenezeka kuwa (miguu?) ili waweze kuishi vizuri nchi kavu. Na mlolongo kama huo unaotufikisha kwa viumbe kama binadamu.’
Mwisho wa kunukuu.

Labda ningependa kuweka bayana kuwa wakati nasoma habari hii sikuwa mwanablog lakini nilivutiwa sana na habari hiyo ambayo aliiandika kwa kirefu sana.


Hivi karibuni nilikuwa nasoma habari moja juu ya nadharia ya hayati Charles Darwin juu ya wanasaikolojia kutumia Panya katika tafiti zao .

Je Darwin anasemaje kuhusu hili?

Kwa mujibu wa utafiti wake anasema kuwa Binadamu na panya ni viumbe wenye asili moja wanaofanana kitabia,. Wote ni mamalia wanaofanana kisaikolojia.
Mfumo wa viungo vyao vya ndani vinafanana na pia mfumo wao wa ubongo katika mawasiliano unafanana vile vile.

Chembe chembe za kwenye ubongo wa binadamu zinazotumika katika kutoa taarifa unafanana na mfumo wa panya.
Kwa mfano majaribo yoyote ambayo yameshindikana kufanyika kwa mwanaadamu kutokana na sababu mbalimbali za kiusalama yamefanyika kwa panya.

Kwa kawaida Ubongo wa mwanaadamu ni mkubwa kuliko wa panya, lakini ukubwa unapolinganishwa na mwili ni dhahiri kuwa tofauti hiyo itatoweka

Ukweli ni kwamba ukubwa wa ubongo wa binadamu ukilinganisha na wa panya ni kutokana na ukubwa wa kitu kinachoitwa Neocortex.
Hili ni eneo linalohusiana na kuona na kusikia.

Darwin anaendelea kubainisha kuwa mwanaadamu, nyani na panya wana asili moja (common ancestors)

Kwani wanafanana kitabia kwa asilimia kubwa sana kwa sababu wote ni mamalia na wana mfumo wa viungo vya mwili vinavyoshabihiana, na ndio maana ikasemekana kuwa binadamu anatokana na nyani.

Je kuna ukweli juu ya jambo hilo?


Hapa naomba msaada wa bwana Bwaya.

Je Samaki walianza kuwa nyani katika hatua ya kuelekea kuwa wanaadamu, au walibadilika moja kwa moja na kuwa wanaadamu?

Je kama ni hivyo panya wanaingiaje kwenye mkumbo huu?

Nilikuwa najaribu kupitia vitabu mbali mbali vya kisayansi katika maktaba yangu nikakutana na na ndharia nyingi za kuchekesha, kiasi kwamba ziliniacha nimechanganyikiwa.

Kama Bwaya alivyowahi kusema katika mfululizo wa makala zake za kisayansi kuhusiana na nadharia hizi za akina Darwin hata kufikia kumwita Fyatu,

Katika makala yake ya ‘
Sayansi na ghiliba zake

Naweza kukubaliana na yeye.

Lakini ninayo maswali ambayo najaribu kuyatafutia majibu

Hivi nadharia hizi zina ukweli kiasi gani?

Kwa kuwa nadharia hizi ni za miongo kadhaa iliyopita, Je hakuna wanasayansi wapya wanaoweza kutupa jibu sahihi?

Kwa nini tuendelee kuaminishwa na kukaririshwa na nadharia hizi zenye utata?

Je dini nazo zinasemaje kuhusu jambo hili?

Je tusimamie wapi?

Naomba kufungua mjadala.

7 comments:
Andika Maoni Maoni
 1. Shabani somo hili nzuri sana inabidi tufungue darasa(shule) maana mmh hapa inabidi ubongo ufanye kazi kweli mi limenishinda nawapisha wananchi wengine

  ReplyDelete
 2. Nasubiri "utambuzi wa kujitambua" ili ni"jielewe". Kw akuwa Kaka Bwaya anayashughulikia saana haya, na kwa kuwa anayaandika kwa mapana yake, na tumsubiri. Najua yuko aakusanya dodoso za kuja kumwaga hapa.
  Ninaendelea ku-tune

  ReplyDelete
 3. Bwana Bwalya ni kati ya vijana ambao nikisoma kazi zao napata picha ya anakoelekea. I like the guy. Nshasoma kazi hizi miezi kadhaa iliyopita na nikakubali huyu mshikaji anayaweza mambo. Ameonyesha kuitumia elimu yake vizuri

  ReplyDelete
 4. Naungana na da Yasinta, kaka mkubwa Mubelwa na Mtingwa, ama niseme nakubaliana nao kuwa yaandikwayo na kaka Shaban na kaka Bwaya yanafikirisha kwa kiasi kikubwa.
  Naukubali uandishi huo. Wanaitumia vema elimu. Lakini naziheshimu kazi za wanablog wanaosugua vichwa kabla ya kuandika.

  ReplyDelete
 5. Nimepita na naendelea kusugua kichwa!

  ReplyDelete
 6. inamaana ndio sababu mimi napenda sana kuogelea? kwa sababu nilikuwa samaki au niliogelea tumboni mwa mazangu?

  mimi sijui nisemeje laskini tahitaji utambuzi zaidi hapa!

  lakini mwanzo u natuhusu nini bwana sisi kazi yetu si kuishi tu?

  ReplyDelete
 7. Katika sayansi inaonekana kabisa kuwa viumbe wanahusiana kwa mlolongo unaoanzia kwa kiumbe mmoja aliyeishi baharini(Sayansi inaamini uhai ulianzia majini) Kwa maana nyingine kiumbe huyo mmoja ndiye aliyeasisi kutokea kwa kila kiumbe unachokijua leo.

  Kwa hiyo inakuwahivi: Uhai ulianzia baharini kwa viumbe wanaofanana. Baadae mabadiliko yalikuja kusababisha wengine wahamie nchi kavu.

  Kutokea kwa viumbe hao, kunaelezwa kwa nadharia mbalimbali. Ila ile inayojulikana kama natural selection, ndiyo inayokubalika zaidi kama alivyoinukuu Kaluse.

  Viumbe walikuwa wakibadilika kwa kasi na namna tofauti kiasi cha kusababisha wingi wa viumbe tunaouona leo hii.

  Kwa maana hiyo, tunaweza kusema zamani hizo wanyama na mimea walikuwa kiumbe mmoja. (yaani dunia ilikuwa na jamii moja ya viumbe) waliokuja kugawanyika kuwa mimea na wanyama. Wanyama nao waliendelea kuitikia mabadiliko ya mazingira yaliyokuja kufanya kutokea kwa aina mablimbali za wanyama.

  Umbali kati ya mnyama mmoja na mwingine unatokana na urefu wa historia ya wawili hao. Na kila kundi la viumbe wenye uhusiano wa karibu wamewekwa kwenye kundi linalofanana.

  Kwa hivyo, utaona wanyama kama panya na binadamu wana tabia nyingi zinazowafanya wakaribiane, ila sio kama binadamu na nyani. Kama ni undugu basi, kwa kadiri ya sayansi, binadamu na nyani ni mtu na kaka ake wote wakiwa wajomba wa panya.

  Ni namna gani mabadiliko haya yalitokea, kwa kweli pamoja na kufundishwa kwa kina, bado naona kuna utata wa wazi(japo ni kweli maelezo yanashawishi kitaaluma. Kwa mfano, nadharia hii inarahisisha mno mabadiliko kuliko hali halisi.

  Je, sayansi inatenda haki? Ndio maana kule kwangu nilitaka kuonyesha kuwa sayansi hapa imetumia zaidi imani kuliko ushahidi. Nimeandika kwa kasi kubwa, msomaji anatarajiwa kusamehe makosa yote ya mwandiko.

  ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi