Je wewe ni mtu wa kupenda ghafla, yaani mwanaume anapokutamkia kwamba
anakupenda huwa unamuamini kwa kiasi gani, unakuwa ni mwepesi wa kumuamini na
kujitoa kwa ajili yake au unakuwa na kujivuta vuta ili kujiridhisha kabla ya
kuingia katika uhusiano? Hebu fikiri kabla ya kuamua, jipe muda kwani hakuna
jambo lililo jema kama subira linapokuja swala la kupenda. Subira itakuepusha
kupoteza muda wako katika mahusiano ambayo hayana mashiko wakati dhamira yako
ilikuwa ni kumpata mwenzi mwenye sifa muafaka, pale utakapoingia mahali ambapo
sipo. Kwa kawaida kutoka katika uhusiano huo kuna gharama kubwa na kunaweza
kukusababishia matatizo mengi yakiwemo ya kiafya.
Hapa chini nitajaribu kueleza makosa kadhaa ambayo wanayafanya wanawake linapokuja swal la kupenda:
Hapa chini nitajaribu kueleza makosa kadhaa ambayo wanayafanya wanawake linapokuja swal la kupenda:
1.Kumbadili mtu awe vile utakavyo:
Usije ukajidanganya kwamba unaweza kumbadilisha mtu mzima na akili zake.
Kama umepata mwanaume ambaye kwa mtazamo wako unamuona ana sifa muafaka lakini
anatabia ambazo huzipendi kwa mfano ulevi au kuvuta sigara vitu ambavyo
vinakukera sana, usije ukajidanganya kwamba unaweza kumbadilisha na akaacha
tabia hizo, anaweza kuacha kwa muda tu ili kukuvuta ukiingia kingi imekula
kwako, tabia hiyo inaweza kujirudia. Ni vyema kama kuna tabia ambazo umezipenda
lakini zipo ambazo huzipendi kutoka kwa mwenzi wako, basi weka uzingativu
kwenye zile tabia unazozipendfa na zile usizozipenda achana nazo, kama ataamua
mwenyewe kuziacha sawa lakini kama akiamua kuendelea nazo, basi zisikuumize
kwani unaweza kujikuta ndoa yako inakuwa na migogoro isiyokwisha kwa sababu ya
kuonekana una ghubu kwa kujaribu kumbadilisha mwenzi wako na mwisho wake upendo
unakuwa haupo na kisirani katika ndoa kinaongezeka. Kitendo cha kuonekana kuwa
na ghubu kinaweza kumuingiza mwanaume katika tabia nyingine mbaya ya kutotumia
muda mwingi kukaa nyumbani kwake na kutafuta kampani nyingine, kama akipata
kampani ambayo siyo nzuri anaweza kuangikia katika nyumba ndogo ambayo
itamkubali bila masharti.
2.Njoo tuishi:
Unaweza kukutana na mwanaume ambaye ana nyumba nzuri au amepanga nyumba
nzuri na ana kila kitu ndani pamoja na usafiri, anakuwa mwepesi kukupa funguo
za nyumba yake ili uhamie muishi pamoja, lakini haweki msimamo wake wazi kwamba
ana matarajio gani na wewe. Kabla ya kukubali kupokea funguo na kuhamia kwake
jiulize kama unampenda kwa dhati au umekubali kwa sababu ya nyumba yake nzuri.
Kumbuka nyumba na vitu vingine vinavyotizamika kwa macho (material things)
havina mashiko linapokuja swala la kupenda. Kupenda kunahusisha vitu vya ndani
kama vile kupenda kwa dhati bila masharti wala kuangalia sifa za nje, kuwa na
amani moyoni kila umwonapo mpenzi wako, kuwa na furaha wakati wote mnapokuwa
pamoja, kupatwa na msisimko wa mapenzi kila umwonapo au usikiapo sauti yake nk.
Lakini kama utamkubali mwanaume kirahisi kwa sababu tu kakukabidhi funguo za
nyumba yake wakati huna mapenzi ya dhati ni janga kubwa kwa sababu hivi vitu
vya nje vinaweza kutoweka kirahisi, sasa je ikitokea si mapenzi nayo yatakuwa
yamekwisha? Kumbuka kwamba kile kilichokupeleka kwake hakipo.
3.Amekuwa ni liwazo kwako
Liwazo linaweza kuwa sehemu ya mapenzi lakini hivi vitu haviendi pamoja.
Unaweza kuwa na mwanaume ambaye mnapendana na mnakamilishana hii ni tofauti na
mwanaume unayempenda na ukamgeuza kuwa liwazo pale unapohisi upweke. Jiulize,
je ni kwamba mnapendana na mnafurahi kuwa pamoja au unampenda kiasi kwamba
huwezi kuishi bila uwepo wake. Hapa nazungumzia utegemezi wa kihisia, yaani
unakuwa king’ang’anizi mpaka mwanaume anakuona kero, badala ya kufurahia
mahusiano yenu mwanaume anakuona kuwa ni kero kutokana na kuwa tegemezi wa
kihisia. Hakuna mwanaume anayependa mahusiano ya aina hii anachoka haraka
kihisia na atajitahidi kwa kila namna kukukwepa na ikiwezekana kukutosa na
kutafuta ustaarabu mwingine jambo ambalo litakuumiza sana.
4.Mwanaume king’ang’anizi:
Mwanaume kutongoza na kukataliwa siyo jambo linalowashughulisha sana kwao
kujaribu na kukosa ni sehemu ya maisha, lakini lipo suala la kung’ang’ania,
yaani mwanaume kumfuatilia mwanamke kwa hali na mali na kujitoa ili kuhakikisha
anampata mwanamke anayemtaka. Huu ni mtego wa mapenzi, kwani kwa mwanaume
kung’ang’ania na kufuatilia mwanamke kwa muda mrefu bila kuchoka hata
asumbuliwe kiasi gani haimaanishi kwamba mwanaume huyo amempenda mwanamke huyo.
Wakati mwingine ni matamanio tu ndiyo yamemsukuma kutokana na sifa za nje alizo
nazo mwanamke huyo. Kupenda kwa mwanaume kunahusisha zaidi sifa za nje kuliko
za ndani na ndiyo maana mapenzi ya aina hiyo hayadumu yanaanza kama kichaa na
kuyeyuka ghafla kama kipande cha barafu juani. Pale mwanamke anapokutana na
mwanaume king’ang’anizi na asiyekubali jibu la hapana, kabla ya kukubali
ajiulize kama anakubali kuwa na mahusiano na mwanaume huyo kwa sababu amempenda
kwa dhati au kwa sababu ya uking’anga’nizi wake? Kumbuka kwamba wapo baadhi ya
wanawake wanaweza kumkubali mwanaume tu kwa sababu amemfuatilia sana, anajiwa
na huruma anakubali kuwa na mausiano naye siyo kwa sababu amempenda bali kwa
sababu ya huruma. Ni vyema ukajiuliza kama na yeye atathamini huruma yako au
akishapata alichokitaka atakugeuka na kuwa mwiba mchungu kwako? Tafakari na
chukua hatua.
5.Baada ya kupanda mbegu mmea ukachipua.
Umekuwa na uhusiano na mwanaume huyu kwa muda mrefu, lakini hakuwahi
kukutamkia kwamba ana matarajio gani na wewe kuhusiana na swala la ndao, ghafla
unakoma kuziona siku zako… Mimba hiyo! Je unafanyaje?
Kwanza naomba ufahamu kwamba, kupata mimba haimaanishi ndiyo kuolewa. Hili ni kosa ambalo wanalifanya wanawake wengi tena wa kiwango cha kutosha, wanaamini kwamba kubeba mimba kutawahakikishia kuolewa na mwanaume aliyempa ujauzito. Kwa huku kwetu sheria haziwabani sana wanaume linapokuja swal la kulea mimba na matunzo ya mtoto kwa hiyo mwanaume kumtosa mwanamke aliyebeba ujauzito siyo jambo la kushangaza. Wanawake ambao ni single mother wanajua kuhusu jambo hilo. Kwa hiyo kama unabeba mimba fanya hivyo ukiwa umejiandaa kujitwika changamoto zitakazojitokeza na usije ukajifariji ukidhani kutakuwa na masaada kutoka kwa mwenzi wako, utakuwa unajidanganya. Kama akikubali mfunge ndoa sawa, kama akikubali kulea mimba na mtoto atakeyezaliwa pia ni sawa, akikataa wala usivunjike moyo, simama imara na songa mbele na maisha kwani kuzaa kabla ya ndao siyo mwisho wa maisha, yapo maisha tena mazuri sana ukiwa na mwanao. Kwanza unaye mtu wa kukuliwaza, na pili utakuwa umajihakikishia kwamba wewe si mgumba, na tatu leo na kesho umekuwa mtu mzima unaye wa kukushika bega kuliko kutegemea ndugu zako.
Kwanza naomba ufahamu kwamba, kupata mimba haimaanishi ndiyo kuolewa. Hili ni kosa ambalo wanalifanya wanawake wengi tena wa kiwango cha kutosha, wanaamini kwamba kubeba mimba kutawahakikishia kuolewa na mwanaume aliyempa ujauzito. Kwa huku kwetu sheria haziwabani sana wanaume linapokuja swal la kulea mimba na matunzo ya mtoto kwa hiyo mwanaume kumtosa mwanamke aliyebeba ujauzito siyo jambo la kushangaza. Wanawake ambao ni single mother wanajua kuhusu jambo hilo. Kwa hiyo kama unabeba mimba fanya hivyo ukiwa umejiandaa kujitwika changamoto zitakazojitokeza na usije ukajifariji ukidhani kutakuwa na masaada kutoka kwa mwenzi wako, utakuwa unajidanganya. Kama akikubali mfunge ndoa sawa, kama akikubali kulea mimba na mtoto atakeyezaliwa pia ni sawa, akikataa wala usivunjike moyo, simama imara na songa mbele na maisha kwani kuzaa kabla ya ndao siyo mwisho wa maisha, yapo maisha tena mazuri sana ukiwa na mwanao. Kwanza unaye mtu wa kukuliwaza, na pili utakuwa umajihakikishia kwamba wewe si mgumba, na tatu leo na kesho umekuwa mtu mzima unaye wa kukushika bega kuliko kutegemea ndugu zako.
6.Pesa inapokuwa sehemu katika kupenda.
Wapo baadhi ya wanawake kabla ya kumkubalia mwanaume wanaangalia anamiliki kitu gani, amesoma kwa kiwango gani, ana kazi ya aina gani, anafanya shughuli gani, anazo fedha za kutosha au yuko katika mazingira ya utafutaji yanayoashiria neema huko mbeleni. Sikatai kwamba wanawake kabla ya kumkubali mwanaume wanataka kujihakikishia usalama, na kama nilivyowahi kusema hapa mara nyingi kwamba usalama kwa mwanamke maana yake ni mtu kuwa na fedha, tofauti na zama za kale za mawe ambapo uwindaji na kilimo kilimuweka mwanaume shupavu katika nyanja hizo kukimbiliwa na wanawake. Siku hizi hayo hayapo, fedha imekuwa ni njia ya mkato katika kupata kila kitu. Kwa mwanamke fedha ni mtego umnasao kama panya na kipande cha nguru mtegoni. Siku hizi ukiwa na fedha una uwezo wa kumpata mwanamke umtakaye, fedha imekuwa kama tufani, inabeba waliomo na wasiokuwemo, hata wale watakaotokwa na povu kupinga hoja hii, nadhani hawajapata bahati ya kukutana na wanaume wenye fedha, laiti wangepata wasingeweza kusimama hapa na kupinga hoja hii. Kwa ushauri tu, si vibaya kuangalia mwanaume mwenye muelekeo wa kutafuta lakini hicho kisiwe ni kigezo namba moja, kwani kama akikuonyesha sifa hizo kabla ya kuingia kwenye uhusiano kisha ukaingia na baadaye ukagundua mwanaume huyo si mali kitu wenyewe mnaita mwanaume suruale, utaumia sana.
7. Uzuri wa kitandani
Ninaposema uzuri wa kitandani namaanisha kuridhishana katika tendo la
kujamiiana, kwa kawaida wanawake ndiyo wahanga wakubwa linapokuja swala la njaa
chumbani, wao ndiyo kwa asilimia kubwa hawaridhishwi na wenzi wao katika tendo.
Siyo kwamba waume zao wana udhaifu, la hasha, inawezekana wanazo nguvu kama za
simba, lakini kwa kawaida tendo la kujamiiana haliwi zuri eti kwa sababu tu
mwanaume anazo nguvu kama za simba, bali inahitaji usanii na utundu ukiwemo
werevu wa kihisia kuweza kumfikisha mwanamke kileleni. Wanaume wengi kwa sababu
ya mazoea wanadhani swala la kumfikisha mwanamke kileleni ni kutwanga kwa
kutumia msuli. Si kweli hata kidogo, ni kumuandaa mwanamke kwa maneno matamu
kabla hata ya kuelekea kitandani. Kwa hiyo wapo wanaume wenye ufundi huo
linapokuja swala la kujamiiana, nia mafundi hodari wenye uwezo wa kuwafikisha
wenzi wao peponi, lakini inawezekana katika maeneo mengine ya kimaisha wakawa
watupu kabisa. Siyo wawajibikaji, wanyanyasaji wakubwa, hawana staha,
hawawaheshimu wenzi wao na ni wenye vurugu kichwani. Wakati mwingine mwanamke
anaweza kunasa kwa sababu hiyo tu, ya ufundi wa kitandani, lakini akajikuta
anaishi katika machungu kutokana na kutothaminiwa na kunyanyaswa kupita kiasi.
Kinachomuweka si kingine ni ile starehe ya muda mfupi wawapo kitandani tu basi.
Kuna haja ya kujiuliza, Je ni kitu gani hasa kinachokufanya umpende mwenzi
wako? Kama utamkubali na udhaifu wake na una uwezo wa kuhimili hizo tabia
zisizofaa kwa maana kwamba hazikuumizi kihisia (kitu ambacho si rahisi sana kwa
wanawake) ni sawa, lakini kama huwezi, sikushauri kuingia katika uhusiano wa
aina hiyo, kwani ni kujitafutia kaburi la mapema.
No comments:
Andika Maoni Maoni