Wengi
wetu tunadhani kwamba machale ni kitu cha kufikirika na hayafanyi kazi kama
inavyosemwa. Ukweli ni kwamba machale yapo na yanafanya kazi sema tu
wengi hatufuati maelekezo ya machale yetu kila kitu tunabahatisha na mwisho wa
siku ni sisi tunaoumia.
Leo
nitaelezea namna kutumia machale yako ili yakusaidie kukuongoza katika shughuli
zako na maisha yako ya kawaida.
Machale
yako kwenye akili yetu ya kina (subconscious mind) na kama ilivyo kwa akili
yako inavyokuunganisha na ulimwengu au jamii inayokuzunguka kutegemea na namna
masafa yako yanavyotikisika na machale nayo yanakuunganisha na ulimwengu wa
nje. kwa kukuongoza katika safari yako ya kutafuta mafanikio
Kwa
hiyo wakati unapofikiria kufanya jambo lolote au kama unataka mafanikio kupitia
kitu chochote machale yako yatakuwa yanakuongoza na kukuweka katika mazingira
yatakayofanikisha safari yako ya mafanikio. Machale yatakuongoza katika kufanya
maamuzi sahihi.
Kwa
mfano kila mtu anahitaji awe na pesa au utajiri, kwa kuwa ni lazima uwe na kitu
cha kubadilishana ili upate pesa unafanya upembuzi na kuona kwamba ukifanya biashara
fulani au ukipata kazi fulani utaweza kuimarisha kipato chako na kupata
mafanikio.
Hapa
ndipo mtego ulipo, wakati unafanya jitihada za kutafuta mtaji ili kuanzisha
hiyo biashara unajikuta unakwama lakini inatokea fursa nyingine ambayo unaweza
kuifanya lakini unaiona kama isiyo na kipato unachokitarajia, hapo machale yamekuunganisha
na bishara ambayo ndiyo itakayokuletea mafanikio ingawa siyo ile uliyokuwa
unaitaka. Lakini pia kwa upande mwingine unaomba kazi fulani katika kampuni
halafu unapangiwa kazi tofauti na ile uliyokuwa unaitaka, hapo machale
yanakuongoza kupata kazi sahihi itakayotimiza ndoto zako.
Lakini
wengine kwa kutojua namna machale yanavyofanya kazi hupuuza kila milango ya
fursa inapofunguka kwa sababu fursa hiyo iko kinyume na malengo yao. Haya ni
makosa yanayofanywa na watu wengi kwa kutofuata machale yanapowaongoza.
Kwa
wale wanaojua utandaji wa nguvu ya mvuto ambao niliwahi kuileleza wakati fulani
hapa nilisema kwamba Mawazo yetu ya kina
yanatengeneza mawimbi na yanavuta kila tunachokiwaza na kuwa ndio maisha yetu
halisi. Sasa basi katika kuvuta tunachotaka machale kazi yake ni kukuongoza
katika safari yako ya kupata unachohitaji. Kwa hiyo unaweza kushangaa kila
unachoomba kinakuja kinyume na matarajio yako na hivyo unapuuza na kuendelea kuhangaika ili ufanikiwe
kwenye jambo hilo lakini juhudi zako hazielekei kuzaa matunda unayoyakusudia.
Kama
utapuuza na kushindwa kufuata machale yako yanavyokuongoza utaishi kufanya
maamuzi mabaya na kupoteza kile ulichokuwa unakitaka.
Hebu
tuangalie mfano ufuatao:
Utendaji
kazi wa machale…..
Labda
tuseme unatafuta kazi, kwa hiyo unatuma maombi kwenye kampuni fulani,
hiyo ni baadaya kufanya uchunguzi kwa kuongea na watu wanaofanya kazi katika
kampuni hiyo wakakuambia mambo mazuri wanayofanyiwa katika hiyo kampuni hususan
mishahara na marupurupu mengi sana. Unavutiwa na hiyo kampuni na kutuma maombi
huku ukiendelea kuelekeza nguvu zako za mvuto katika kampuni hiyo ili upate
kazi lakini pamoja na kuitwa kwenye usaili na kufanya vizuri inatokea unapigwa
dana dana katika kuipata hiyo kazi kwa ahadi za njoo kesho au subiri tutakuita.
Lakini
siku moja unakutana na rafiki yako wa siku nyingi anakupa taarifa kuhusu nafasi
ya kazi katika kampuni anayofanya kazi lakini nafasi hiyo iko kinyume na kazi
unayotaka kuifanya, lakini pia hata hiyo kampuni huipendi na unaiona ni ndogo
ukilinganisha na ndoto zako za kutaka kufanya kazi katika kampuni kubwa.
Hata
hivyo kwa shingo upande unaomba na kufanya usaili na ndani ya muda mfupi
unapata hiyo kazi ambayo baadaye inakuletea mafanikio makubwa na ndoto zako
nyingi zinatimia.
Hapo
machale yanakuongoza kupata kazi sahihi kwa ustawi wa maisha yako na si kazi
uliyokuwa unaitaka. Ukweli ni kwamba machale na akili ya kina vinafanya kazi
kwa pamoja.
Kwa
hiyo kila tunachofanya au tunachotaka kukifanya, kama vile kupata kazi nzuri,
kuanzisha biashara, kununua gari, kujenga nyumba au kujiendeleza kielimu vyote
hivyo machale yatakuongoza lakini kama nilivyosema kuwa iwapo hutayasikiliza
machale yako hakuna utakachofanikiwa kwani unaweza ukapata unachohitaji lakini
kisikupe amani na matokeo yake ni vurugu tupu, na hapo ndipo unapoweza kumsikia
mtu akisema, ‘machale yalinicheza wakati nilipotaka kufanya jambo fulani lakini
nikapuuza sasa nimekwama.’
Kwa
hiyo ni vyema sasa tukaanza kufuata machale yetu, tunatakiwa kuyapa umuhimu na
kuyaelewa ili yaweze kutuongoza kwa kushirikiana na akili ya kina, na hapo
ndipo utakapokuwa unafanya uchaguzi mzuri na kupata unachokihitaji.
Machale
yanaweza kukupa taarifa kwa njia mbali mbali……
Ni
zipi hizo?
Machale
yanaweza kukupa taarifa kupitia njia zifuatazo:
1;
Rafiki
2;
Mpenzi wako au mwenzi wako, hapa kidogo kwa wanaume kuna ugumu kusikiliza
machale yao kama taarifa itapitia kwa mke au mpenzi wake; kwani kutokana na
mfumo dume wapo wanaume wengi tena kiasi cha kutosha hawawaamini wake zao au
wapenzi wao, kwa hiyo machale yanapopitisha taarifa kupitia kwa watu hao, kuna
ugumu kama taarifa hiyo itasikilizwa na kufuatwa.
3;
Ndugu, jamaa na marafiki
4;
mtoto njia hii nayo inaweza isiaminiwe kwa sababu siyo watu wote wanaoweza
kuwaamini watoto, lakini ukweli ni kwamba watoto ndiyo njia inayotumiwa na
machale katika kutoa taarifa kuliko njia nyingine yoyote
5;
Radio na Magazeti kupitia taarifa mbalimbali zinazotanganzwa kupitia Radio au
katika magazeti kwa mfano unataka kununua kiwanja au shamba, wakati umeshapata
shamba na ukawa unataka kulipa halafu siku moja kabla ya malipo unasikia
taarifa kupitia radio au magazetini kwamba eneo unalotaka kununua lipo kwenye
mipango miji kwa hiyo wale waliojenge bila kufuata taratibu nyumba zao
zitabomolewa na kama ni viwanja vitachukuliwa kwa matumizi yaliyokusudiwa. Hiyo
ni taarifa ambayo imeletwa na machale.
6;
Wapita njia au watu usiowafahamu wanaweza kukupa taarifa muhimu wakiwa kwenye
mazungumzo yao yasiyokuhusu.
Labda
unataka kuacha kazi baada ya kupata kazi mahali pengine ambapo walikuahidi
kukupa mshahara mkubwa na marupurupu mengi sana, mara unakutana na watu wako kwenye
mazungumzo yao lakini wanazungumzia matatizo ya kampuni inayotaka kukuajiri kwamba
imefilisika na watafunga muda si mrefu au wanazungumzia ubaya wa mkurugenzi wa
kampuni hiyo jinsi anayoajiri na kufukuza wafanya kazi hovyo kwa uonevu. Hii
nitaarifa kupitia machale yako.
Niliposema
machale yanakuunganisha na ulimwengu wa nje nilikuwa na maana hiyo kwamba kazi
yake kubwa ni kukulinda kwa kukuongoza upite njia sahihi, kinachotakiwa ni sisi
kuwa tayari muda wote kupokea taarifa ya machale yetu.
Watu
waliofanikiwa na ambao wanaijua siri hii ya kutumia machale yao vizuri ndiyo hao
tunaosema wana kismati, Bahati au kuwasingizia wana kizizi. Watu hawa ni ngumu
kutapeliwa au kuingizwa chaka.
No comments:
Andika Maoni Maoni