Ilikuwa ni kazi kweli kweli, lakini yote yalikuwa ni majaaliwa
Kuna wakati Rais wa awamu ya pili ndugu Ali Hassan Mwinyi aliwahi kusema kuwa moto mkubwa huanzishwa na cheche, akimaanisha kuwa jambo lolote kubwa linaweza kuanzishwa na jambo dogo sana.
Jana wakati narudi kutoka katika mihangaiko yangu majira ya saa tatu usiku nilipata mkasa ambao mpaka leo hata sijui ilikuwaje, nilipanda basi la kuelekea Buguruni pale maeneo ya Posta majira ya sa tatu usiku hivi. Tulipofika Maeneo ya Kariakoo walipanda abiria wengine watatu lakini walionekana kuwa wamelewa sana. Wakati tukiendelea na safari mara ukazuka mzozo kati ya mmoja wa wale abiria waliolewa na abiria mwingine, kisa huyo abiria mwingine kakanyagwa na yule mlevi.
Vikazuka vita vya maneno, ilianza taratibu hivi, lakini kwa jinsi basi lilivyokuwa likiendelea na safari na ndivyo wimbo wa matusi kati ya abiria hao ulivyozidi kupamba moto, kutahamaki wakaanza kutupiana matusi ya nguoni na ya kudhalilisha sana haya yakilenga kuwadhalilisha wazazi wa kike, naamini mmeelewa mpaka hapo namaanisha nini.
Nilianza kuhisi shari mapema kabisa lakini sikuwa na jinsi nilikaa siti ya mwisho, kwani kama ningekaa karibu na mlango ningeshuka, lakini basi lilijaa na hapakuwa na njia ya kupita.
Vita ile ya matusi na ilianza kuwa kuwahusisha abiria wengine ambao walikerwa na matusi ya wale abiria walevi, ghafla wakaanza kupigana huku basi likiendelea kwenda kwa kasi. Mara zikazua kelele za abiria wengine wakimtaka dereva asimamishe basi ili watu washuke kwenye basi ili kuepuka ule ugomvi ambao sasa uligeuka kuwa ugomvi wa kupigana zilizidi mle ndani ya basi.
Dereva alisimamissha basi na kwa kuwa walikuwa wamengushana sakafuni kwenye basi ilibidi tupite juu ya viti ili kuelekea mlangoni, nilipoukaribia mlango abiria mmoja akamuamrisha dereva apeleka basi kituo cha Polisi pale Buguruni, nilikuwa bado sijateremka, ghafla basi likaondolewa kwa kasi ajabu, abiria mmoja akanisukuma na kujikuta niko chini kwenye lami na niliona tairi la nyuma la lile basi likipita usawa wa uso wangu, kutahamaki nikasikia sauti ya gari lingine likifunga breki za ghafla, nilipogeuka niliona gari dogo likiwa usawa wa pale nilipoangukia, nilijizoa pale na kujisogeza kando ya barabara, huku wapita njia wakinizunguka kutaka kujua kama nimeumia au la, ili wanikimbize hospitali. Nilijichunguza na kuona kuwa nina michubuko kidogo katika mikono yangu kutokana na kuangukia kwenye lami, lakini nilihisi mkono wangu wa kulia ukiuma kwa mbali, niliyapuuzia yale maumivu na hata niliposhauriwa niepekwe hospitali nilikataa kwani hata basi lenyewe lilishatokomea kusikijulikana.
Nilipanda basi lingine na kurudi nyumbani kwangu, nilipolala, ndio nikanza kusikia mausmivu makali ya mkono wangu wa kulia, na sikulala pamoja na kumeza vidonge vya kutuliza maumivu. Alifajiri na mapema niliwahi hospitalini na baada ya kupigwa X-Ray ikaonekana kuwa mkono wangu umeteguka kwenye kiungo. Nikatibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Bado najiuliza, hivi ilikuwaje, kwa nini wale abiria ambao hawakulewa hawakuwapuuza wale abiria waliolewa na kuwaona kama wajinga hivi ili kuepusha shari? kwa nini walishindwa kuwavumilia kwa dakika chache ambapo kila mtu angeshuka kwenye basi na kuelekea nyumbani kwake?
Ni kitu gani wangepoteza kwa kuwapuuza walevi wale? Hivi kama lile gari lingenikanyaga ni nani angelaumiwa, ni wale abiria walevi au dereva? Na lile gari dogo je? kama dereva asingefunga breki ingekuwaje?
Pamoja na kuwa mkono wangu wa kulia umefungwa bendeji na hauna kazi lakini kwa kutumia mkono mmoja wa kushoto nimemudu kuwapasha yaliyonikuta jana.

Kweli sasa ndio watu au mtu utakapoamini kila mtu ana Mungu wake au malaika wake anayemchunga. Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kupisha mbali mkasa huu. Kwani lingekuwa ni pigo kubwa sana kumpoteza kaka yetu mtambuzi. Kama nilivyosema najua pia huyo dereva aliyefunga breki alikuwa na malaika aliyemtuma afanye hivyo. Cha kushukuru hapa u mzima na upo na familia yako. Ila pole sana wa yote kaka.Kweli kwa nini watu wasiwe tu kimya na kuwaacha wengine wagombane?
ReplyDeleteLoh, Kaluse, pole sana kwa ajali iliyokupata na kwa maumivu na usumbufu wote uliotokea.
ReplyDeleteKweli Mwenyezi Mungu amekulinda sana, ingekuwa historia sasa.
Ugomvi wa wengine umesababisha hasara kwa wengine. Huyo aliyekanyagwa na mlevi alipaswa atumie ustaarabu wa kibinadamu wa kujua kuwa mtu anapolewa akili yake haifanyi kazi barabara na maamuzi ya mtu mlevi mara zote hayapewi umakini wala maana yoyote katika eneo lolote. Yaani anakumbusha ule usemi kuwa, 'ukijibizana na mjinga, watu watashindwa kutambua mjinga baina yenu ni nani na hivyo kuwachukulia wote kuwa ni wajinga', ndiposa, 'hata mpumbavu mara nyingine huhesabiwa hekima ikiwa akaa kimya'. Huyo aliyekuwa si mlevi hakutumia busara ama alizidiwa jazba au alikuwa na hasira ama masumbufu ya mawazo hata kabla ya kupanda basi na kukanyagwa na mlevi.
Hizi habari nimezipokea kwa mshtuko mkubwa sana, lakini hata hivyo ni jambo la kumshukuru mungu kuwa uko salama kabisa na kwa kuwa unawapenda wanablog wenzako na na wasomaji wako umemudu japo kwa mkono mmoja wa kushoto kutupasha kile kilichokusibu.
ReplyDeleteKama walivyosema dada Subi na dada Yasinya, kuwa ni vyema watu kukaa kimya wakati kwingine ili kuepusha shari kwani kukaa kimya ni silaha nzuri sana kwa mtu mwenye busara pale anapokabiliana na mjinga.
Kwa nini watu wanakosa subira kwa jambo dogo namna hiyo, kwani kukanyagwa ndio umepungukiwa na nini?
Pole sana kaka yangu natumaini utapona na kuendelea kutuelimisha kama kawaida kupitia kibaraza chako hiki makini.
Kuna wakati Hayati Munga Tehenan, wakati anatufundisha maarifa haya ya utambuzi aliwahi kusema kuwa kuna watu wanakuwa na silka ya kuhamisha hasira, yaani anaweza kuudhiwa aidha na mke, mume, rafiki, jirani, au hata bosi wake, na kwa kuwa hana au hakuwa na uwezo wa kukabiliana na huyo aliyemuudhi, basi hasira hizo zitamshukie mtu mwingine, na ndio maana kwa wale wanaoishi jijini Dar wanalijua hili, kuwa sehemu nzuri saaana inayotumiwa na watu wa aina hii ni kuzihamishia hasira zao kwa makondakta wa daladala au hata kwa abiria wenzao, na kwa mkasa huo uliompata kaka Kaluse ndio unatupa picha halisi ya watu wenye tabia hizo. Wakati mwingine Utashangaa mtu jambo dogo sana lakini huo moto utakaolipuka hapo utadhani kafanyiwa jambo kubwa sana.
ReplyDeleteBusara hekima na subira vikitumiwa vizuri daima hutupa matokeo mazuri sana na hutuepusha na mambo mengi sana ambayo yangeweza kutuletea madhara.
Kaka Kaluse hii ni changamoto kwako, nakumbuka tulijifunza pale kwenye madarasa yetu ya utambuzi kuwa matukio mengi yanayotutokea yanatokana na namna tunavyofikiri, kwamba tunavuna kile tulichopanda.......hata wewe mara nyingi makala zako zimekuwa zikizungumzia jinsi mawazo yetu yalivyo na nguvu. Ni jambo la kustaajabisha kidogo kuwa hili limekutokea wewe peke yako miongoni mwa abiria waliokuwepo ndani ya basi lile......Nakupa pole lakini jaribu kuchunguza mawazo yako au fikra zako.
We Kaluse una loho ngumu kama ya mkurya...lol! yaani unaumwa nkono na bado unatuandikia kutujuza masahibu yalokukuta?
ReplyDeleteEnewei, kumbuka kila jambo hutokea kwa sababu fulani ili kutufunza jambo...nadhani wote mushaelewa, ne!
Duh!!!
ReplyDeletePengine sikustahili KUPOTEA namna hii, lakini imeshatokea. Na nimerejea wakati usio wa furaha hata kidogo. Hii ni habari ya kuhuzunisha mno hasa pale uliposikia mlio wa breki na kuliona tairi la gari.
Kwenye kusikiliza reggae nilijifunza kitu kimoja (kati ya vingi) kuwa "sometimes let someone be right for the sake of peace."
Kama huyo aliyekuwa hajalewa angepuuza kukanyagwa msingepitia kote huko.
Lakini hatujui hatma yao wote waliokwenda polisi (kama walikwenda)
Pole Kaka na unapendwa na ndio maana umebaki. ILI UIKAMILISHE KAZI YA ALIYEKUWEKA HAPA.
Blessings
ni masoma tunayoyapata. wale abiria walikuwa na maumivu yao kwa kiigereza wanaita pain body ndio maana wakatwangana.
ReplyDeletesasa dirisha hukuliona? hiyo ndo noma ya urefu lakini ungejitupa dirishani. na mimi niliwahi kuiona hiyo ubungo siku moja na nikaruka nje ya gari chwwiiiiiiii
Pole sana sina cha kuongeza mengi yameongelewa na wenzangu
ReplyDeletePole sana Bwana Kaluse...Wale majambazi waliovamia nyumba yako walikuacha mzima wewe na familia yako. Patashika hii nayo imekuacha mzima. Na kwa vile uko mzima basi halijaharibika neno na mengine yote ni madogo. Ubarikiwe!
ReplyDeleteNawashukuru sana wote kwa kunipa pole kutokana na masaibu yaliyonikuta, naamini yate ni sehemu ya maisha,
ReplyDeleteKaka Ramson nakubaliana na wewe, kuwa kiala jambo linalotutokea linatokana na namna tunavyofikiri, nakubali kuwa hiyo ni changamoto kwangu, kukagua fikra zangu isije ikawa nimejitakia mwenyewe......
Yani mpaka leo nikiisoma hii habari inanifikirisha sana. Pole sana Mkuu!
ReplyDelete