Kitambi ni hali ya
kiafya ya mtu mnene ambapo mafuta ya ziada mwilini huongezeka eneo la tumbo kwa
kiasi kikubwa.
Mtu akiwa na kitambi anapata athari kubwa ikiwamo kupungua
kwa umri. Katika karne hii, hili ni mojawapo ya tatizo kubwa la kiafya duniani.
Hata hivyo, tatizo la kitambi kiafya linarekebishika.
Katika mawazo ya
kizamani na hata sasa katika baadhi ya nchi mtu akiwa na kitambi anaonekana ni
tajiri.
Tatizo la unene na vitambi litazidi kuongezeka ikiwa
serikali, hususan wananchi wenyewe hawatachukua hatua za dharura na mipango
madhubuti kulikabili.
Vitambi hupunguza maisha ya watu wenye hali hiyo ya afya, hivyo
kusababisha upotevu wa rasilimali watu.
Ili kuepukana na athari hiyo watu wahakikishe wanabadili
namna wanavyoishi na milo yao. Wengi wana muda mchache sana wa kutayarisha
vyakula visivyo na mafuta mengi majumbani mwao, hivyo wanakula nje zaidi, yaani
kwenye hoteli na migahawa na matokeo yake ni kuwa na vitambi.
Kuna wengi wanatambua athari za tatizo la unene na vitambi,
lakini hawafanyi chochote kulirekebisha, hii inatokana na ukweli kwamba idadi
kubwa ya watu hawajui maana halisi ya kuwa na afya njema.
Watu wengi, hasa
vijana wamekuzwa kwa kula chipsi, mikate na vyakula vya sukari na si mbogamboga
na matunda.
Ukweli ni kwamba watu wengi hawafanyi mazoezi ya kutosha kama
ilivyokuwa zamani hivyo, watu wenye vitambi wanaongezeka kila sehemu.
Kwa ujumla, umri wa mtu mnene mwenye kitambi huwa pungufu kwa
miaka 8 had 10 ukilinganisha na mtu mwenye umbo la kawaida.
MAGONJWA
Hii inatokana na ukweli kwamba uzito wa mtu husababisha
magonjwa ya moyo, aina fulani ya kisukari, magonjwa ambayo huua mamilioni ya
watu duniani kote. Kifupi ni kuwa ukiwa na mafuta mengi mno utakuwa kwenye
hatari ya kukumbwa na magonjwa kama ya kupanda kwa presha, magonjwa ya
moyo, kansa. Kuongeza uzito au kunenepa
kunasababisha mwili ushindwe kupata sehemu ya kutosha ya kuhifadhi mafuta na
hivyo kuanza kuyatunza mafuta hayo kwenye sehemu za ndani ya mwili, kuuzunguka
moyo na ndipo matatizo yanapoanza.
USHAURI
Kila mtu aepuke kula vyakula vyenye mafuta mengi na kutokula
chakula kupindukia na ule unaposikia njaa, kutotia mafuta mengi kwenye chakula
na kutotumia sukari nyingi.
Kila mtu anatakiwa kufanya mazoezi ya kukimbia, kutembea au
kuogelea angalau kwa nusu saa kila siku.
Watu wanashauriwa kuacha kutumia vyakula vya kopo na hasa
vile vyenye gesi nyingi. Wale ambao ni wanene kupita kiasi waonane na daktari
kwa ushauri wa kitaalamu.
No comments:
Andika Maoni Maoni