0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Nov 18, 2008

HOFU ZA KESHO BADO NI DUBWANA KUBWA LA KUTISHA?

Wamasai ni miongoni mwa jamii inayosifika kwa kufikiri vizuri, kwao kesho haina maana yoyote.

Naona makala yangu iliyopita inayozungumzia kuhusu kutoiogopa kesho haikueleweka kwa baadhi ya wasomaji.

Jana usiku nimepokea sms kutoka kwa msomaji mmoja akituhumu kuwa watu wa utambuzi huwa tunazungusha maneno.

Akilenga kwamba kesho ipo kwa hiyo ni lazima watu wahofu kuhusu hiyo kesho.

Nilijitahidi sana kuielezea mada hii kwa lugha nyepesi sana lakini inaonekana kwamba wapo baadhi ya wasomaji hawakunielewa.

Kwa kuwa nimeamua kufundisha kuhusu haya maarifa, sina budi kuweka sawa pale ambapo wasomaji hawanielewi.

Kimsingi sisi tangu tulipozaliwa tulifundishwa kufikiri vibaya, kamwe hatukufunndishwa kufikiri vizuri, ndio sababu watu wengi wanaishi katika maumivu makubwa kihisia na majuto.

Wapo watu ambao wanaamini kwamba kwa kuwa wazazi wao ni masikini, ambao kimsingi walitaka wenyewe, basi na wao watakufa masikini,

kwa nini? Kwa sababu wamefundishwa kwamba fedha huenda kwa wenye fedha na umasikini huenda kwa masikini.

Tumefundishwa kuwa, biashara kubwa kubwa ni kwa ajili ya wahindi na waarabu, biashara ya maduka ni ya wachaga na wakinga.

Tumeaminishwa hivyo ndio sabau tunashindwa hata kuthubutu, kwa sababu kila ukisema ujaribu zile sauti za kukatisha tamaa, kutoka kwa wazazi, ndugu, na jamii kwa ujumla zinakwambia, “huwezi acha kabisa, kamwe hutafanikiwa, hizo biashara zina wenyewe” Hata ukijaribu, ukipata changamoto kidogo, zile sauti zinarejea, na kukwambia, “ si tulikwambia bwana hizo biashara zina wenyewe”

Wakati fulani rafiki yangu mmoja alikuja kutaka kunikopa kodi ya kulipia fremu ya duka lake, kwa bahati mbaya sikuwa na hela. Rafiki yangu huyo alikuwa na wasiwasi sana, nilipomuuliza sababu, akaniambia kuwa mwenye hizo fremu ni mama mkorofi sana akicheleweshewa kodi hata siku moja anamfukuza mpangaji, nikamuuliza kwani alitakiwa kulipia lini hiyo kodi, akanijibu kuwa kesho ndio mwisho anatakiwa apeleke kodi ya watu.

Nikamshauri angoje hiyo kesho halafu aende kwa huyo mama mwenye nyumba na kumwambia ukweli kwamba amekwama kupata kodi kwa kuwa biashara sio nzuri, asikie mama atasemaje? Alikubali lakini bado alikuwa na mashaka kidogo.

Nilipokutana nae wiki mbili baadae aliniambia kuwa yule mama alikubali bila kinyongo kusubiri angalau kwa wiki mbili, na hakuonesha kukasirika, na alimwambia kuwa katika wapangaji wake wote yeye ndiye mpangaji muaminifu kuliko wote kwa sababu huwa anapeleka kodi kwa wakati.

Si unaona jinsi hofu zetu zinavyotuambia uongo. Wataalamu wa nguvu za mawazo wanasema, kwamba kwa kawaida hofu zetu zina asilimia 1 tu ya ukweli, asilimia 99 ni uongo.

Kama mtu unafikiri vizuri sidhani kama utaihofia kesho, kwani kesho ni nini?

Ipo kanuni moja inayosimamia namna ya kufikiri kwetu, huwezi kufikiri jambo hili ukavuna jambo lingine, ukifikiri kuhusu mafanikio utavuna mafanikio, kwani kile ambacho mawazo ya kawaida yanafikiri na kuamaini, mawazo ya kina yanakichukuwa na kukizalisha kama kilivyo.

Kanuni hii ilifundishwa na Yesu miaka 2000 ilioyopita kama Budha alivyofundisha kanuni hiyo miaka 500 kabla ya hapo, kwamba kile unachowaza na kuamini ndio mavuno ya kile ulichonacho leo.

Kwa kuhofia kwetu kuhusu kesho, ndio sababu wengi wetu tumekuwa watumwa wa waganga wa kienyeji.

Waganga wengi wamenufaika sana na ujimga huu, ndio sababu wanavuna kila siku, kwa sababu kila mtu anataka kujua kesho itakuwaje, iache ije, unahofu nini?

Unapoenda kwa mganga anaweza kukwambia, “naona yule jirani yako anataka kukumaliza kwa sababu anakuonea wivu na maendeleo yako”

Kwa kuwa unamuamini mganga, unaanza kujenga hofu na chuki dhidi ya jirani yako, kosa kubwa linaanzia hapo, kwani katika mawazo yako ya kawaida huwezi kufikiri kitu kingine zaidi ya chuki, hicho ndicho kitajkachoelekea kwenye mawazo yako ya kina.

Sasa hapo unafikiria utavuna nini? Ni lazima utavuna maanguko.

Ni sawa na kujenga daraja kuelekea katika maanguko yako.

Ili kuondokana na hali hiyo, kinachotakiwa ni kuanza kufikiri vizuri, kufikiri vizuri kwa maana kwamba tufikiri, malengo na mafaniko yetu na yale mambo yanayotupa faraja, na kutufurahisha.

Naona kwa leo niishie hapo, nikipata wasaa nitaandika makala inayofundisha namna ya kufikiri vizuri.

Hadi wakati mwingine, naomba kuwasilisha.

10 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. great article. nadhani umejieleza na kueleweka vizuri. nitaikopi kwangu ili wengine waisome pia. thanx

    ReplyDelete
  2. Kamal, Ahsante kwa Compliment.

    Naamini together tunawakilisha. uwe huru kuchukuwa article yoyoye kwa ajili ya blog yako.
    Natarajia mpaka 2010 maarifa haya yatasambaa nchi nzima kwa asilimia 75.

    ReplyDelete
  3. Kamal, Ahsante kwa Compliment.

    Naamini together tunawakilisha. uwe huru kuchukuwa article yoyoye kwa ajili ya blog yako.
    Natarajia mpaka 2010 maarifa haya yatasambaa nchi nzima kwa asilimia 75.

    ReplyDelete
  4. Kaka Kaluse,
    Umefundisha siri kubwa sana na mafanikio na ukiangalia kwa ndani sana jamii zetu ni masikini hasa kutokana na jinsi tunavyowaza. "Your by what u think" Ukweli nimejifunza kutumia nguvu ya kuwaza positive na kufukuza hofu kwa nguvu zote ni ukweli mafanikio huja. Hata kama umezaliwa katika umaskini wa namna gani ukiwa na mawazo positive unaweza kuwa vyovyote unataka hapa duniani. Ni kweli nakubaliana na wewe asilimia kubwa ya maskini wengi vijijini mwetu ni mtazamo (mawazo) na si rasilimali zinazotuzunguka.
    Pia ndoa nyingi zipo katika migogoro kwa sababu ya jinsi wanandoa wenyewe wanavyoamini na kukiri yale mawazo na mitazamo yao na wengine ndoa zimekufa ukiangalia kwa undani ni jinsi wananavyowaza na kutawaliwa na hofu.
    Biblia inaongelea sana ukombozi wa jinsi unavyofikiria ndiyo chanzo cha mafanikio.

    Asante sana
    Asante sana

    ReplyDelete
  5. Nashukuru sana kaka Mbilinyi kwa mchango wako.
    bado tunayo safari ndefu sana ya kuielimisha jamii juu ya mambo haya.
    Umezungumzia ndoa, kwa kweli umenigusa sana kwani mada hiyo nitakuja kuijadili hapo baadae.
    Ukweli ni kwamba ndoa nyingi ziko katika hati hati kwa sababu ya namna tunavyofikiri.
    Wanandoa tulio wengi tumekuwa sio wakweli kwa nafsi zetu,
    tunasema hivi, tukimaanisha kitu kingine.
    mawasiliano yamekuwa ni magumu sana miongoni mwetu, kiasi kwamb kila mmoja amuhofia mwenzake, hatutabiriki na maamuzi yetu mengi yamejaa utata mkubwa.
    kwa nini?
    kwa sababu tunaishi kimazoea, kila jambo tunalotaka kufanya, hatuamui kama sisi bali tunaangalia matakwa ya jamii.
    Je tutafika?
    Hili linahitaji makala inayojitegemea.

    ReplyDelete
  6. kaluse naomba uandike mada juu ya kuishi kwa mazoea

    ReplyDelete
  7. Nianze na nukuu ambayo umeielezea hapo kuwa "your mental picture will determine your actual future" ama niseme nyingine isemayo "your body achieves what your mind believes". Yaani ukipanga kuvuna magunia 10 mwaka huu ukapata 10.5 utaona umevuka malengo hata kama ardhi uliyotumia inastahili kukupa magunia 100. Na yule aliyepanga kuvuna magunia 100 katika sehemu hiyohiyo akapata 99 atajiona kama ameshindwa kutimiza malengo. Kwa hakika tunawaza saana kuhusu kesho ila tunaiwazia kama "isiyowezekana". Tunapenda kuishi siku kwa siku na hilo hutufanya tushindwe kujipanga. Ukienda mbali Kaka Shabani utagundua kuwa hata mfumo wetu wa elimu na kazi unaathirika kwa hili. Yaani unasomea uandishi wa habari mpaka unapomaliza ndio unasema eti una wito wa siasa ama kuingia kwenye ufundi kisha miaka kadhaa baadae wajikuta unataka kuwa mwanahabari.Ukiuliza kwanini hakuchagua wito tangu awali atasema Mama alisema hayo si ya ukoo wetu ama si watu kama sisi na mambo kama hayo. Umeeleza mengi na yamefunzwa mengi na sasa CHANGAMOTO YETU ni kuanza kutambua kuwa hatutakiwi kuihofia kesho maana tukiamua twaweza kubadili hisia kuwa HOFU ZA KESHO BADO NI DUBWANA LA KUTISHA.
    Thx and Blessings
    See y'all "next ijayo"

    ReplyDelete
  8. Mzee wa changamoto umenikuna na kunigusa sana na point zako, umenikumbusha mbali sana kuhusiana watu tunavyofikiri, kuna watu kazi ya wiki moja au siku 7 anafanya kwamwezi mzima au siku 30 why? kwa sababu ndiyo amefikiri na kuamua. Kwani muda hu-expand na ku-contract kutokana na wewe unavyo allocate wakati unajipangia kazi kwenye mawazo yako. Kwa kazi ya miezi 6 ufanye kwa miaka 6? unatokana na wewe unavyopanga kichwani mwako na mwili hupokea.

    Asante sana

    ReplyDelete
  9. Naona mada hii imeibua chanagamoto ambazo sikuzitarajia, ukweli ni kwamba leo nilipanga niweke mada mpya lakini nikaona si busara kuwa over feed wasomaji wa blog hii. Jana usiku nilitafakari nikaona ni vyema niwaache wasomaji nao watafakari na kuchangia, na wakati huo huo nikawa naandaa makala nyingine ya namna ya kufikiri vizuri.
    Kwa kuwa maoni ya bwana mbilinyi na ya mzee wa changamoto yamenigusa, nimeona si vibaya nikiweka makala ya Hayati mwalimu wangu Munga Tehenan katika blog yangu, ambayo inazungunzia mada hii hii, lakini kwa namna tofauti, halafu kesho mchana nitaweka ile ya namna ya kufikiri vizuri.
    Nadhani tuko pamoja.
    Kama kuna mawazo mapya bado nakaribisha maoni kuhusiana na mada hii.

    ReplyDelete
  10. Nashukuru saana kwa Mada na uchambuzi kisha uchangizi. Hili ndilo jema. Kuiinua jamii na kuiwezesha kifikra. Tukumbuke wenye fikra kama kina Bob Marley waliosema "emancipate yourselves from mental slavery, none but ourselves can free our minds". Ni vema sana tunapojiunga katika blogs namna hii na kuikomboa jamii kwa namna hii. Hili ama haya tusomayo yataigusa jamii kubwa kwa kuwa kila mmoja anaweza kuwaelimisha wengi ambao watawaelimisha wengi pia.
    Blessings

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi