0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Nov 17, 2008

HIVI NI NANI KATI YETU ANAYEIJUA KESHO?


Mimi naishi leo, siishi kesho, je wewe?


Watu wengi siku hizi wanaishi katika hofu kubwa, Wanahofu kuhusu familia , majirani, kazi, na matarajio ya maisha yao ya baadae.
Hofu imekuwa ni dubwana kubwa linalotisha katika maisha ya watu wengi hivi sasa, kwa sababu ya ushindani wa kutaka kuuridhisha mwili.

Tunaweza kuondoa hofu iwapo tutabadili mfumo wetu wa kufikiri kwa kuanza kufikiri vizuri. Kwa kawaida hofu huwa zinatuletea matokeo hasi, kwa sababu kwa kutawaliwa kwetu na hofu, tunajenga woga kwa kuiogopa kesho, na hiyo ndio sababu ya watu wengi kuanguka katika maisha.

Woga kuhusu kesho hauna maana, kwani kesho huwa haiji kwa namna unavyotarajia.
Sisi huwa hatuishi kesho bali tunaishi leo. Wakati unawaza nini kitakachokutokea kesho, mwezi ujao, au mwaka ujao, unakuwa unajiwekea vikwazo katika kufikia malengo yako kwa kuvuruga mfumo wako wa kufikiri.

Kwa hiyo si vyema kutumia hata sekunde yako moja kuhofu kuhusu kesho, ishi leo.
Kimsingi huwezi kufanikiwa na kufikia matarajio yako iwapo maisha yako yatakuwa yametawaliwa na hofu za kesho, na kama maisha yako yatakuwa yametawaliwa na hofu za kesho basi utakuwa unapoteza muda wako bure, na matokeo yake unakufa ukiwa hujayafikia malengo yako ya kuwepo hapa duniani.

Lakini hata hivyo ni vyema ukumbuke kuwa katika kufikia malengo yako, ukubaliane na changamoto za maisha, kamwe zisikutie hofu, cha kufanya ni wewe kuyaona matarajio yako kwa taswira ya jicho lako, jiamini na lione kabisa kwamba lengo lako limefanikiwa.
Ishi kila siku kwa nanma inavyokuja, Kwani kesho ni jina tu la siku inayofuata, kuihofia na kuiogopa ni Ujinga tu.
Kwa nini nasema ni ujinga? Ni kwa sababu hakuna hata mmoja wetu anayeijua kesho.





3 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. Bwana Bwaya ahsante kwa swali lako,
    Makala itayozungumzia mada hiyo iko jikoni lakini kwa kifupi jana imeshapita, kwa nini ikusumbue ndugu yangu?
    kama ukikaa na kuangalia mambo yaliyokutokea jana ni lazima utayakumbuka yale tu yatakayokuletea maumivu kihisi, kwa sababu hatukufundishwa kufikiri vizuri.
    Mkuu nipe muda nitakuletea mada hiyo siku si nyingi.

    ReplyDelete
  2. Bwana Bwaya ahsante kwa swali lako,
    Makala itayozungumzia mada hiyo iko jikoni lakini kwa kifupi jana imeshapita, kwa nini ikusumbue ndugu yangu?
    kama ukikaa na kuangalia mambo yaliyokutokea jana ni lazima utayakumbuka yale tu yatakayokuletea maumivu kihisi, kwa sababu hatukufundishwa kufikiri vizuri.
    Mkuu nipe muda nitakuletea mada hiyo siku si nyingi.

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi