0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Jul 28, 2014

Watafiti sasa wabaini: Kuoana kunaelekea ukingoni...!http://cdn.madamenoire.com/wp-content/uploads/2013/05/wedding1-pf.jpg

Hivi karibuni baadhi ya watafiti wa masuala ya mapenzi na uhusiano wamebainisha kwamba bado kitambo kidogo, japokuwa ni polepole ndoa zitaanza kuonekana kama fasheni ya kale na isiyo na umuhimu kwa watu hususani wa kizazi hiki kinachokuja kwa kasi.

Licha ya jamii kushuhudia ndoa zikifungwa kila uchao tena kwa mbwembwe za kila aina, lakini jambo ambalo wengi wetu hatulijui ni kwamba hivi sasa hata hao wanaooana hawajui ni kwa nini wanaoana, na ndiyo maana hata kiwango cha talaka nacho kimepanda sana ukilinganisha na miaka ya zamani.

Kwa nini watafiti hawa wanaamini kwamba kuna siku tena siyo nyingi ndoa zitaonekana kama fasheni ya kale na isiyo na mashiko kwa kizazi hiki?Najua wengi wetu hatujui, lakini kinachotufanya tusijue ni kwa sababu tunaamini kwamba ndoa au kuoana ni suala la kimaumbile, yaani sisi binadamu hatuwezi kuishi au kuzaana bila kuoana.

Na ndiyo maana hata wale watoto na kwa bahati mbaya ni wengi sana siku hizi, wanaozaliwa nje ya utaratibu huo wa kuoana wanaitwa ni watoto haramu.

Lakini wengi wetu tusichokijua ni kwamba ndoa ilipangwa na binadamu kwa sababu ya choyo chake, na ndiyo maana zinaporomoka kila uchao!


Kama huamini,fuatana na mimi ili nikueleze usichokijua…

http://cdn.madamenoire.com/wp-content/uploads/2012/09/black-couple-in-bed.jpg

Katika kipindi chamiaka 50 iliyopita dunia imeshuhudia kubadilika kwa mitazamo mingi kuhusiana namapenzi na ndoa. Mapenzi na ndoa yalivyokuwa yakitazamwa miaka ya 1970, sivyoyanavyotazamwa leo kabisa. Siyo hapa nchini kwetu tu, bali karibu duniani kote.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba hadi kufikia miaka ya 1980 ndipo tulipoanza kusoma aukusikia na pengine kuona habari za uchumba na uhusiano zikigusa zaidi tendo la kujamiiana kuliko mapenzi, zikizungumzia tendo la kujamiaana kama kwamba zinazungumzia kupendana.

Hali hiyo ilisababisha jamii kuanza kuchukulia uchumba au uhusiano kuwa ni wa kukutana kimwili halafu basi.
Ndiyo maana ni aghalabu vijana wa siku hizi kuoana bila kukutana kimwili au kuonjana kwanza.


Kuanzia hapo kuoana kukaonekana kama siyo lengo kuu kwamba watu wamependana bali lengo lililopinda na kushindwa kueleweka.

Ndipo hapo watu wengi wakaanza kutumbukia kwenye mapenzi ya leo leo, bila kujali mila za kale zilizokuwa zikisisitiza mabinti kulinda bikra zao kwa heshima yafamilia. Mila hizo zikawa zimepigwa kumbo na kufa kifo cha mende.

http://i2.cdn.turner.com/cnn/dam/assets/130718174349-amref-childbirth-african-women-horizontal-gallery.jpg

Hebu kumbukeni vizuri, mimba za utotoni zilianza miaka gani. Ukweli ni kwamba mimba za utotoni zilianza kuonekana kitu cha kawaida kabisa kuanzia miaka ya 1990, kwani kablaya hapo, mimba za utotoni ilikuwa ni kashfa ya mtaa.

Kuanzia miaka hiyo ya 1990, kufanya mapenzi kukawa kumepewa kipaumbele na kuoana ikaonekana siyo lengo kuu.


Vitabu vya hadithi, vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya jamii kutokana na utandawazi vikagongelea msumari wa mwisho katika jambo hilo, kwani vimekuwa vikielezea suala la kujamiiana hadi jamii ikaamini kwamba kujamiiana ndiyo mapenzi yenyewe.

Sasa kama kujamiiana ndiyo mapenzi yenyewe, kuoana kuna nafasi gani? Naamini kabisa kwamba, thamani ya ndoa itakuwa ni ndogo sana, kwa sababu hata bila kuoana watu wanapata wanachohitaji na kukata kiu zao za matamanio ya kimwili.

Lakini ina maana pia kwamba thamani ya ndoa ilishushwa sana na mabadiliko haya, na ndiyo maanahaishangazi siku hizi hata wanawake wenyewe hawasitiri tupu zao na wamekuwa wakiziweka sokoni wazi wazi.

Wao wanauza na wanaume wananunua, sasa ya nini kufuga ng’ombe wakati maziwa yapo mitaani kedekede, tena kila sampuli.

Lakini pia tamthilia tunazozishuhudia kwenye runinga zetu nazo zikaja na uongo mwingine, mabinti zetu wakaanza kutamani aina ya maisha ya ndoa wanayoyaona kwenye tamthilia hizo jambo ambalo siyo halisi na hakuna kijana wa leo atakayeweza kuigiza mapenzi ya namna ile, labda anawezakufanya hivyo kwa muda mfupi na akishapata anachotaka anashindwa kuendeleakuigiza na hapo ndipo mapenzi yanapokufa kibudu.

Kama hamjui, labda niwakumbushe tu kwamba kupanda kwa kiwango cha talaka kwa jamii kama yetu kulianza kwenye miaka ya 1980 na kiwango hiki kimekuwa kikiendelea kupanda hadi leo.


http://cdn.madamenoire.com/wp-content/uploads/2012/09/high-maintenance.jpg

Haya mapenzi yaholela yamesababisha kushuka kwa thamani ya ndoa, kwani yametufundisha kwamba, kama hatuwezi kupata bashasha na furaha kutoka kwa mtu mmoja, basi tunawezakupata kwa watu wengine.

Sasa kama ni hivyo, ndoa ina maana gani? Ndiyo maana tafiti nyingi hivi sasa zinaonyesha kwamba, ndoa sita kati ya kumi, kwa wakati fulani kwa maisha ya ndoa hizo, hukabiliwa na kusalitiana kwa mwanandoa mmoja au wote kutoka nje ya ndoa zao.


Kwa hiyo siku za karibuni watu watakuwa wakioana na ikajulikana kabisa ni lini wataachana. Hivi sasa ndoa nyingi zinadumu kati ya miaka 7 na 13. Lakini tunapoelekea hali halisi inaonyesha kabisa kwamba, ndoa zitafikia mahali ambapo zitadumu kwa kati ya miaka miwili hadi minne. Katika hali hiyo itakuwa ni kujidanganya kusema kwamba kuna ndoa.

Siku hizi wasichana wa kati ya miaka 25 hadi 30 ukiwaambia wewe uko kwenye ndoa kwa miaka20 hadi 30, wanashangaa kiasi cha hata wewe mwenyewe kuwashangaa.

Hawaamini kwamba, mtu anaweza kudumu kwenye ndoa kwa miaka 20 hadi 30 akiwa na mtuhuyo huyo kwa miaka yote hiyo. Sasa hapo utasema kweli kwamba kizazi hiki kinandoa tena!

1 comment:
Andika Maoni Maoni

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi