Mimba kutoka mara kwa mara ni tatizo linalotokea kwa wajawazito ambao mimba zao hutoka zikiwa na umri wa chini ya wiki 20.
Utokaji huo wa mimba kitaalamu huitwa
recurrent miscarriage au Recurrent Pregnancy Loss. Karibu asilimia moja
ya wanawake wenye uzazi hukumbwa na tatizo hili na kwa wanawake wote
tatizo hili huongezeka kadiri umri wake unavyoongezeka.
Zipo sababu mbalimbali za mimba kutoka
mara kwa mara, baadhi yake ni kuwa na matatizo ya mji wa mimba ya
kuzaliwa nayo kitaalamu huitwa Congenital Malformation.
Hii ni kwa sababu kizazi huwa hakina umbo au nafasi ya kutosha kuruhusu mtoto akue mpaka kuzaliwa. Vivimbe vya mji wa uzazi pia husababisha mimba kuchoropoka.
Hii ni kwa sababu kizazi huwa hakina umbo au nafasi ya kutosha kuruhusu mtoto akue mpaka kuzaliwa. Vivimbe vya mji wa uzazi pia husababisha mimba kuchoropoka.
Wanawake wengine mimba zao hutoka
kutokana na kuwa na tatizo kwenye Shingo ya Uzazi ambayo hulegea na
kitaalamu kujulikana kama Cervical Incompetence. Kadiri mimba inavyokua,
shingo ya uzazi hushindwa kuhimili na hivyo mimba kuchoropoka.
Wengine mimba zao hutoka kutokana na kushikana kwenye kuta za mji wa mimba hali ambayo huitwa kitaalamu Asherman’s Syndrome.
Wengine mimba zao hutoka kutokana na
kuwa na ugonjwa wa kisukari, ugonjwa wa vivimbe vya ovari (Polycystic
Ovarian Syndrome), upungufu wa homoni ya tezi shingo (Hypothyirodism),
vichochezi kutokaa vizuri yaani Hormonal Imbalance n.k.
DALILI ZA MIMBA KUTOKA
Dalili za mimba kutoka zipo nyingi lakini leo nitazitaja zile kubwa ambazo ni kutokwa na damu ukeni, maumivu ya tumbo hasa chini ya kitovu na kiunoni, kutoa uchafu au sehemu ya mimba iliyoharibika na siyo ajabu mwanamke akisikia homa na kutapika .

Unapopata dalili hizo nenda kamuone
daktari haraka akakufanyie uchunguzi ili kugundua chanzo cha tatizo
hili. Ingawa mara nyingine inakuwa ni ngumu kujua chanzo halisi cha
tatizo.
Daktari akifanya uchunguzi wake kwa
vipimo na chanzo cha tatizo kujulikana, mgonjwa anaweza kutibiwa kwa
kutumia dawa au kwa kufanyiwa upasuaji na mgonjwa kupona kabisa kwa
sababu ni ugonjwa unaotibika.
Mimba zenye hatari ya kuharibika nizile
ambazo mjamzito hutoka damu ukeni wakati wa wiki za mwanzo za ujauzito,
yaachi chini ya wiki ya 20.
Hali hii huashiria dalili ya mimba
kutaka kuharibika au kutoka, ingawa ujauzito unaweza kuendelea mpaka
kujifungua, hiyo hali kitaalamu huitwa Threatened Abortion.
Baadhi ya mambo ambayo huleta hatari ya mimba kuharibika ni kuumia tumboni, matumizi ya kahawa kwa wingi, maambukizi ya magonjwa mbalimbali, umri wa zaidi ya miaka 35 wa mjamzito.
Baadhi ya mambo ambayo huleta hatari ya mimba kuharibika ni kuumia tumboni, matumizi ya kahawa kwa wingi, maambukizi ya magonjwa mbalimbali, umri wa zaidi ya miaka 35 wa mjamzito.
Upatapo dalili hizo kamuone daktari
ambaye atakufanyia vipimo vya Ultrasound ya tumbo, kipimo cha ujauzito,
mkojo ili kuona kama mimba haina madhara kwa dalili hizo na akiona
tatizo atatoa tiba husika.
Ataweza kumshauri mjamazito kupumzika bila kufanya shughuli yoyote na inasaidia kupunguza hatari ya mimba kuharibika. Mjamzito akipatwa na dalili hizo anashauriwa kusitisha kufanya mapenzi na mwenzi wake, kujisafisha sehemu za siri mara kwa mara, punguza au kuacha unywaji wa vinywaji vyenye caffeine kama kahawa au chai, kuacha kufanya mazoezi mazito na asikose kwenda kliniki ya ujauzito na kufanyiwa vipimo.

No comments:
Andika Maoni Maoni