0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Jan 6, 2009

KWA NINI WATU WAKUCHUKIE WEWE TU?

Kila mtu ni mbaya kwako, kila mtu anakuchukia, wewe tu, kila mtu hakutendei haki, kila mtu ana kasoro?
Je wewe ndivyo unavyoishi hivi? Kama jibu ni ndiyo au kama una mtu wako wa karibu ambaye anaishi katika mtindo huu wa maisha, unapaswa kujua kwamba, una mtu ambaye ana matatizo makubwa.
Mtu yeyota ambaye anapenda kusema kwamba, kila mtu anamchukia au kila mtu hamwelewi, basi jua kwamba huyo ni mtu ambaye kimsingi ana matatizo makubwa sana.
Kwa nini?
Haiwezekani kila mtu akawa kama mwingine, yaani akikuchukia huyu na yule ni lazima atakuchukia, ni lazima hatakutendea haki na mengine ya aina hiyo.
Kwa nini sasa wote wawe na tabia za aina moja, yaani wafikie kukuchukia?
Kwa kuwa watu hawafanani kitabia, kimwenendo na kimtazamo, ni wazi ukiona wote wanakuchukia wewe, tatizo haliko kwao, kwa sababu hawawezi wote kuwa na mkabala wa aina moja. Ina maana kwamba wewe ndiye ambaye hujipendi na kutojipenda kwakokunaonekana kwa watu hao.

Tuanposhindwa kujipenda, hasira dhidi yetu huwa tunazitolea kwa watu waliotuzunguka.
Kwa hiyo kama unahisi kwamba watu wanakuchukia, jitahidi kujiuliza kuhusu jambo hilo. Ni wazi haliwezi kuwa jambo la kweli hata kidogo.
Kama ni kuchukiwa, hivi inawezekana ukachukiwa na kila mtu kweli?
Ukichunguza ni wazi utagundua kwamba wenye tatizo sio hao watu.
Mwenye tatizo ni wewe na watu hao ni kioo chako kwa tabia yako.

Kama kila unakopita, iwe ni kazini au popote unajikuta ukiondoka umeacha watu wengi wakiwa wanakuchukia badala ya kukupenda, ujue kwamba wewe ndie mwenye tatizo, wewe ndio mwenye kasoro. Haiwezekani watu wakae kikao cha kukuchukia, bali watu wanaweza kukerwa na kutojiamini kwako au vitendo vyakohadi ikaonekana kama wamekula njama kukuchukia.

Kwa tabia zako, wanajikuta wakikujadili na kuambiana ‘humjui, ndivyo alivyo huyo’ Basi wanakuwa wameunda aina ya timu ya kukuchukia.
Kumbuka tu kwamba kila binadamu anapenda kuona anapendwa na kuheshimiwa, ingawa ni vitu visivyo na maana sana kwake.
Na kama unashindwa kumfanyia hivyo, anaingia mahali ambapo anaona huenda kuwa karibu na wewe ni hatari au haipendezi.
Kama hii ndio tabia yako, utamfanya kila mmoja ahisi kukereka kuwa karibu na wewe.

Hapondipo kuchukiwa kunapoanza.
Naomba nikwambie ukweli kwamba usije ukasema unachukiwa na watu fulani au kwamba watu fulani hawakupendi.
Ukisema hivyo, watu wanaojua tabia za binadamu, watajua kwamba wewe ni mkorofi sana. Ukiona mtu anasema jirani zake, watumishi wenzake, wanafunzi wenzake, ndugu zake, wanaye, wazazi wake au kundi fulani la watu wanamchukia, basi kwa kiwango kikubwa mtu huyo ni mkorofi.
Tafadhali kama imetokea ukahisi kwamba watu fulani wanakuchukia, au hawakupendi inabidi uanze kujiuliza bila kujipendelea kama wewe sio chanzo cha chuki hizo.
Acha kujipenda sana kwa hasara yako, kuwa wewe katika kiwango chako cha juu.11 comments:
Andika Maoni Maoni
 1. duu wananichukia sababu najivunia elimu, pengine maisha yangu ya aghali, au labda baba yangu yupo USA au pengine bitozi au majivuno yangu yamewachosha.
  mmmmm somo kali kaka Nitarudi tena nangojea mambo ya kaka Simon na wengine

  ReplyDelete
 2. smahani OMBI, kaka tuwekee aggregator/kikusanya habari za blogu zingine au unaonaje? kwaheriiiiii kwa leo

  ReplyDelete
 3. Ahsante kwa kunitembelea kaka Mpangala.
  Kuhusu hiyo Aggregator, nimejaribu nimeshindwa naomba anyefahami zaidi anielekeze namna ya kuweka, anweza kutoa darasa lake hapa hapa.

  hata wewe Mpangala kama unaweza kunisaidia karibu, nakaribisha mchango wako.

  ReplyDelete
 4. "...Tafadhali kama imetokea ukahisi kwamba watu fulani wanakuchukia, au hawakupendi inabidi uanze kujiuliza bila kujipendelea kama wewe sio chanzo cha chuki hizo..." Hapa ni mwake kabisa.

  Sasa Kaluse, naomba msaada kwa wadau, namna tunavyoweza kujua ikiwa chanzo cha matatizo ni sisi ama hao wasiotupenda.

  Napenda kazi kama hizi. Nikisoma huwa siwezi kukaa vizuri kwenye kiti. Safi sana kaka.

  ReplyDelete
 5. kwani wewe unajipenda na unajua jinsi ya kujipenda? kama hujui lazima uchukiwe tu na utachukiwa sana mwaka huu.

  jifunze kujipenda ili nawewe upendwe ndugu. vinginevyo unajichukia na unachokiona kwa wenzio sio chuki zao bali zako, wao ni kioooooooo mirror

  ReplyDelete
 6. Kuwa wewe acha wengine wawe wao pia hutahisi kuchukiwa!

  ReplyDelete
 7. Ninae shangazi yangu, alishindwa kuendelea na masomo kwa sababu alibeba ujauzito akiwa kidato cha pili, sheria ya mfumo dume ikamtupanje.

  Sasa hivi kaolewa na anishi na mumewe kwa kubangaiza.

  Shangazi yangu huyu ni mlalamishi kweli kila nikienda kwake analalamika eti ndugu zake wanmchulia yeye na mumewe kwa kuwa hawakusoma na ni masikini.
  baba amejitahidi kumpa misaada ya kila aina lakini haishi kulalamika.

  Kila siku analalamika ndugu hawampendi, majirani wanamchukia, yaani kila mtu hampendi.

  Sasa sijui ni printi hii makala nimpelekee au nitazua ugomvi.

  hebu nipeni ushauri.

  ReplyDelete
 8. Sehemu nyingine ya maisha ni kujua mipaka yako juu ya nini unaweza kufanya na nini huwezi. Pia kujua ni nani yuko kama wewe na nani yuko tofauti. Kujua unayeweza kumridhisha na ambaye hutaweza kwa namna yoyote ile. Kwa ujumla tunaweza kuhisi tunachukiwa kwa kuwa ama tunataka wote watupende au tupende na kuridhisha wote. Lakini pia lazima tutambue (kama ulivyosema) kuwa watu wako tofauti na kuna walio kama wewe na walio tofauti. Kwa hiyo kung'ang'ania kutaka kumridhisha na aa kuridhishwa na kila mtu kutakufanya ujipoteze wewe mwenyewe na kisha ujihisi uko tofauti na hatimaye kudhani wachukiwa na hapo utajichukia. Siamini kama kuna anayeweza kupendwa na watu wote na NAJUA FIKA KUWA HAKUNA ANAYEWEZA KUCHUKIWA NA WATU WOTE, kwa hiyo ukweli ndio huo mliousema wadau, kuwa ukijihisi kuchukiwa na kila mtu, basi pengine wataka ambavyo hawawezi kufanya na hapo tayari tatizo litakuwa ni wewe na si wao.
  Blessings

  ReplyDelete
 9. koero, tatizo la huyo ant yako ni kwamba anajichukia yeye kwa kudhani kwamba kwakuwa hajasoma basi ni mbaya na wala sio ndugu zake.

  we mpende tu

  ReplyDelete
 10. Kuchukiwa kupo na hakutaisha kama kupendwa tu!

  Mpaka mshikaji Yesu akauawa kwa kuchukiwa wakati yajulikana alikuwa ni mchizi ahusuduye na aenezaye amani tu.

  Ukijijua , kujielewa na kuchukua muda kujaribu kumuelewa ´jirani yako ni rahisi kuepusha baadhi ya maswala yasiyo ya lazima yawezeshayo kuchukiwa bila sababu.

  Na mara nyingine ni tafsiri tu ya upendo ni nini. Kuna hata ujuao kuwa wanakupenda lakini wakasema hawakupendi kihivyo ndiomaana wanakunyima uroda, Kijeba unaweza kutafsiri unachukiwa.

  ReplyDelete
 11. Waungwana nawashukuru sana kwa maoni yenu.

  Mada za utambuzi zinaendelea kamakawaida.

  Dada Koero nadhani Mzee mwenzangu wa Utambuzi Kamala Luta amenisaidia kujibu swali lako.

  kama unayo maswali zaidi niwekee humu nitakujibu au wadau wengine watanisaidia kujibu.

  ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi