0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Jan 9, 2009

JE KUKONDEANA NI DALILI YA KUWA NA ROHO MBAYA?

Ni jambo ambalo watu hulisema bila kujua maana yake. Unaweza kukuta mtu akisema
“Ndio maana amekondeana, ana roho mbaya sana”
Ukimuuliza ni kwa nini anahusisha kukondeana au afya mbaya na roho mbaya au kukosa upendo alikonako mtu, hataweza kukupa jibu sahihi. Lakini anajua kwamba kukondeana huwapata wenye roho mbaya.

Kauli hiyo ina ukweli mkubwa wa kutosha. Watu ambao wanatengeneza nguvu hasi nyingi, hatimaye nguvu hizo huwarudia na kuwadhuru. Kwa sehemu kubwa madhara ya nguvu hizo huja kujitokeza kwenye miili yao.

Mtu ambaye anaumwa mara kwa mara anaweza kuwa anaumwa tu kwa sababu nyingine, lakini pia anaweza kuwa anaumwa kutokana na nguvu hasi anazotengeneza.
Nikisema nguvu hasi nina maana ya kufikiri na matendo ambayo yanamuumiza mwenye mawazo na matendo hayo, pia wale wanaomzunguka.

Kwa mfano mtu asiyeweza kusamehe, mwenye visasi, mwenye kijicho, mpenda makuu, mshindani na mengine ya aina hiyo.
Kuna watu ambao hutengeneza sana nguvu hasi kwa kufikiri kwao na tabia zao.

Kwa kawaida nguvu hasi zinadhuru hisia na mwili wa mhusika.

Kwa vipi?

Hebu tutazame kushindwa kusamehe na kijicho.

Mtu ambaye hawezikusamehe anajiweka mahali ambapo muda wote anakuwa kwenye hasira, hisia chungu na mikakati ya kulipa kisasi..
Hii ni sawa na mtu ambaye ana kijicho, kwa mfano. Huyu naye, muda mwingi wa maisha yake atakuwa akiumia kwani kila wengine wakifanikiwa kwa chochote, atahisi vibaya.
Kwa hiyo hisia zake zitakuwa zinachokozeka karibu muda wote.

Kwa kawaida hisia zetu zinapochokozeka tunaiingiza miili yetu kwenye kuzalisha kemikali au homoni ambazo wakati huo hazihitajiwi.
Kwa uzalishwaji huo wa kemikali zisizohitajika mwilini, tunaiumiza miili yetu kwa njia mbalimbali.
Kemikali hizo hatimaye huanza kutuumiza na kutuletea maradhi mbalimbali miilini mwetu.
Hili ni jambo ambalo limethibitishwa kitaalamu.

Kuna maradhi zaidi ya kumi ambayo chanzo chake ni mihemko yetu, maradhi ambayo kitaalamu hufahamika kama Emotionally Induced Diseases.
Haya ni pamoja na maumivu ya mwili, tumbo, kufunga choo, na mengine .
Ndio maana wale watu wote wanaokwenda hospitalini wakiwa wanaumwa, ambao wanaambiwa vipimo havioneshi maradhi yoyote, ukiwachunguza utagundua kwamba wanakabiliwa na hofu, mashaka, visasi na matatizo mengine ya kihisia.

Sisemi kwamba wote wanopimwa na kuonekana hawana maradhi ndivyo walivyo, la hasha.Lakini wengi kati yao ndivyo walivyo.
Hata wale wanaodaiwa kuwa na mapepo pia, utakuta ni wale wenye hisia chungu.

Kwa sababu ya maumivu ya kimwili na yale ya kiakili unakuta watu hawa wakiwa dhaifu.
Kama walivyo wagonjwa wengine, suala la udhaifu wa mwili hujitokeza sana kwa watu hawa, kwani pamoja na maradhi yanayoletwa na hisia chafu, kinga ya mwili hushuka sana pale miili inapohemkwa mara kwa mara.
Ni rahisi kwa hali hiyo watu wenye roho mbaya kukondeana na kukosa afya imara.

Hata hivyo sio kweli kwamba watu wote wenye afya mbovu inatokana na roho mbaya, hapana. Lakini kwa wale walio na roho mbaya, yaani kufikiri na tabia zenye kuzalisha nguvu hasi, nirahisi zaidi kwao kukosa afya bora, kama tulivyoona.



2 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. mapenzi yako waapii........


    nikifa usiweke msiba,
    ila sherekea kwa sababu
    una roho mbayaa
    WEMBAAAAAAAYAAAAAAA!

    ReplyDelete
  2. Naona kama hii habari ina ukweli!
    Unajua kaka Kaluse baada ya kusoma hii habari nilianza kuwakumbuka baadhi ya watu wembamba waliokondeana ninaowafahamu, katita watu kumi niliowakumbuka, sita wanazo tabia ulizozisema.

    Maana sijui niseme kuwa wana wivu, sijui ni roho mbaya, kwani hawaishi kulalamika lalamika hovyo.
    Nadhani hili jambo linaweza kuwa na ukweli japo kidogo.

    Ngoja niwapishe wengine nao wachangie kwani bado naendelea na utafiti wangu.

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi