0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Jan 5, 2009

PABAYA LAKINI UNANG'ANG'ANIA!

Huwa najiuliza inakuwaje mtu analalamika kuhusu kazi yake, lakini bado anaendelea kuifanya. Unaweza kukuta mtu mwenye ujuzi na ambaye angepata kazi mahali pengine, lakini haondoki ila kulalamika ni kila siku akilaani kazi yake.

Unaweza kukuta mtu akiwa kwenye ndoa yenye kumuumiza, inayomzuia kufanya yale anayoyataka kwenye maisha yake, lakini badala ya kutoka kwenye ndoa hiyo yenye kumuumiza, anang’ang’ania huku akilalamikia ugumu na ubaya wa ndoa yake kila wakati. Nabaki najiuliza hivi ni kwa nini haondoki?

Unakuta mtu ana tabia fulani mbaya ambayo inamgharimu na anajua.
Ni tabia ambayo akiiacha anaweza lakini haiachi, na kila tabia hiyo ikimuumiza analalamika sana, lakini hayuko tayari kujitoa kwenye tabia hiyo. Hata akipewa msaada wa namna ya kujitoa, haufuati, hataki kuiacha ingawa inamuumiza.

Kwa mujibu wa wanasaikolojia, wanabainisha kwamba kwenye ubongo wa binadamu kuna sehemu iitwayo eneo la liwazo. Kupitia eneo hilo binadamu anajisikia ana usalama akiwa mahali au kwenye hali fulani aliyoizoea, na nje ya mahali au hali hiyo, binadamu anajihisi hayuko salama na wala hana amani.

Kwa binadamu walio wengi hata kama hawana amani moyoni wanonelea ni vyema kubaki mahali au katika hali fulani kwa sababu ya mazoea tu na kwa kuwa kwa kufanya hivyo wanajiona wako salama.
Ndio maana utakuta mtu ananyanyasika kazini au katika ndoa wakati umuhimu wa mambo hayo kwake haupo tena. Anachokiogopa hakijulikani!

Ukweli ni kwamba usalama wetu hautokani na msaada kutoka nje; usalama wetu unatakiwa utokane na sisi wenyewe.
Lakini kama nilivyosema mazoea yanamfanya mtu kuamini kwamba ni afadhali mateso ya mahali na hali aliyoizoea kuliko kuondoka wakati hajui ataangukia wapi.
Kwa bahati mabaya kama utang’ang’ania kubaki katika eneo lako la liwazo tu, kamwe hutaweza kuujua uwezo wako halisi uliojaaliwa nao au kukijua kipaji chako na kile uwezacho kukifanikisha kwa ufanisi mkubwa.

Ukiamua kwa makusudi kusogea mbele nje ya jamaa unaofahamiana nao; nje ya mazingira uliyoyazoea; na nje ya uzoefu wako, utakuwa umejiondoa katika eneo la liwazo kuelekea njia ya kukua.
Hii ni njia ya kupanua upeo wako. Mtu yeyote anayeanza kujifunza somo jipya shuleni; ajifunzaye lugha mpya; ajifunzaye mchezo mpya; au anayeanza kazi mpya anakuwa amejisogeza nje ya eneo la liwazo.

Hebu kaa utafakari kwa makini na ujiulize kama kuna haja kweli ya kuendelea na kazi hii, tabia hii au uhusiano huu.
Kama ukiona kuna haja ya kubadilika basi fanya uamuzi ulio sahihi,
maana hatima ya maisha yako iko mikononi mwako.

7 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. Nikikunukuu...''Unakuta mtu ana tabia fulani mbaya ambayo inamgharimu na anajua.
    Ni tabia ambayo akiiacha anaweza lakini haiachi,''----Hapo umenisema mimi :-)


    Niliwahi kukutana na mwanamke mmoja aliye wahi kuolewa mara nane. Nilimuuliza kwanini ameolewa mara nyingi hivyo , kwanini asiwe tu rafiki kidume tu akiite akihitaji bila kuolewa nacho? Akaniambia baada ya kuachana mara mbili , amezoea tu na sheria anajua. Kwa hiyo kazoea kuolewa na anapenda harusi halafu akikuchoka anaachika. Anadai ni mazoea.

    Inawezekana pia mtu akazoea kuacha kazi!

    ReplyDelete
  2. Nikikunukuu...''Unakuta mtu ana tabia fulani mbaya ambayo inamgharimu na anajua.
    Ni tabia ambayo akiiacha anaweza lakini haiachi,''----Hapo umenisema mimi :-)


    Niliwahi kukutana na mwanamke mmoja aliye wahi kuolewa mara nane. Nilimuuliza kwanini ameolewa mara nyingi hivyo , kwanini asiwe tu rafiki kidume tu akiite akihitaji bila kuolewa nacho? Akaniambia baada ya kuachana mara mbili , amezoea tu na sheria anajua. Kwa hiyo kazoea kuolewa na anapenda harusi halafu akikuchoka anaachika. Anadai ni mazoea.

    Inawezekana pia mtu akazoea kuacha kazi!

    ReplyDelete
  3. Hapa iko kazi!,

    Hayo ya Kitururu sitayaingilia.

    Lakini kaka Shabani hebu nisaidie, kama ninae boy friend au mume ambaye mkiwa nje ya nyumbani anakuonyesha upendo wa hali ya juu hasa ukiwa na marafiki zako,unakuta anakukumbatia, mara anakubusu na mashamsham chungu mzima, lakini mkiwa ndani ya nyumba ni ghubu lisiloisha, hakusaidii kazi, mlalamishi, anataka kila kitu afanyiwe, kama vile mtoto.
    Rafiki zako wakikuona wanakusifia kuwa una mume mzuri sana, yaani kwa sura na tabia.
    Sasa je uhusiano au ndoa ya namna hiyo, niendelee nayo au nitoke.
    Sio mimi nimeyaona kwa mwenzangu na kanitaka ushauri.

    ReplyDelete
  4. Hivi Ambiere Kitururu nimekusema wapi?
    Labda inawezekana kuna mahali mawazo yangu yamegongana, lakini haikuwa ni kusudio langu kukusema kwa sababu hata hivyo sijui tabia zako.
    Kama hivyo ndivyo basi naomba unisamehe.

    Dada Koero nimekupata vizuri, lakini nisingependa kuweka ushauri wangu hapa hadharani kwa sababu ninayo maswali kadhaa ya kukuuliza.
    Nitawasiliana na wewe kupitia email yako.

    ReplyDelete
  5. @ambiere: Hukunielewa!Ninamaanisha kuwa jambo ulilogusia kama ''Unakuta mtu ana tabia fulani mbaya ambayo inamgharimu na anajua.
    Ni tabia ambayo akiiacha anaweza lakini haiachi,'' limenigusa mimi kwa sababu mimi nazijua baadhi ya tabia zangu mbaya ambazo najikuta nazirudiarudia na zinanigharimu ingawa siachi. Sikumaanisha wakati unaandika ulikuwa unanifikiria mimi. Hii inaonyesha jinsi gani uyaandikayo yafanyavyo watu KUJITAMBUA katika swala.
    Kazi nzuri Ambiere!

    ReplyDelete
  6. Ambiere Kitururu
    Ahsante, kwa kuniweka sawa.

    hata hivyo nazipenda kazi zako.

    ReplyDelete
  7. mmenipiga ngwara kama siyo mtama, maana mmmm topiki kali. kuhusu dada koero kweli kuna maswali lukuki hapo haya kazi njema

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi