Katika utafiti uliofanywa na akina Kruger na wenzake kwa
wanyama jamii ya Sokwe, ilibainika kwamba kulikuwa na vifo vingi vya Sokwe
madume wenye umri wa miaka 13. Hali hii ilitokana na sababu kwamba, kwa kawaida
katika umri huo, Sokwe madume huwa
wamefikia umri wa kupanda na kufanya mapenzi na hivyo huanza kushindana
wenyewe kwa wenyewe wakigombea majike na hata kwa lengo la kudumisha hadhi yao
miongoni mwa Sokwe wengine.
Katika hatua hii Sokwe hao hufikia mahali pa kupigana na hata
kuuana kwa lengo la kujipatia wapenzi na kudumisha hadhi zao. Hali hii haiko
kwa sokwe peke yao, bali hata kwa wanyama wengine pamoja na ndege wa aina
mbalimbali.
Hata hivyo, pamoja na ukweli huo binadamu naye hajanusurika
hata kidogo na purukushani za aina hiyo. Labda kinachomtofautisha binadamu na
wanyama hao ni namna wanavyokabiliana na mashindano hayo. Lakini ukweli unabaki
palepale kwamba, hata akichagua njia ya aina gani ili kushindana na binadamu
wenzake, bado matokeo ya mwisho yatafanana na yale ya wanyama, yaani kifo.
Imeonekana wazi kwamba binadamu wa kiume ndiye mwenye
mwelekeo mkubwa wa kupenda purukushani na kuhatarisha maisha yake. Ingawa
binadamu huyu wa kiume au mwanaume hahitaji kupigana mweleka na mwanaume
mwenzake ili kumpata mwanamke, lakini harakati zake ni zaidi ya kupigana
mweleka.
Hata hivyo katika mazingira mengine, mieleka hupiganwa sana
katika sura ya mieleka halisi au katika sura nyingine za ushindani wa kutafuta
ushindi katika kumpata mwanamke. Wengi tunajua kuhusu habari za kuuawa kwa
wanaume kutokana na vurugu za kugombea wanawake.
Tabia hii ya wanaume ya kuhatarisha maisha si ya leo, bali ni
ya tangu kale. Huenda huko nyuma baadhi ya wanaume walitumia silaha kwa lengo
la kuwadhulumu ama kuwauwa wanaume wenzao ili hatimaye waweze kuwamiliki
wanawake wanaowapenda.
Kwa kawaida, wanaume hushindana wao kwa wao kwa lengo la
kumiliki rasilimali na kuhifadhi au kudumisha hadhi na heshima yao ndani ya
jamii wanamoishi.
Huu ndio ukweli wenyewe ambao hautofautiani hata chembe na
ule wa Sokwe. Ukweli ni kwamba mwanaume anapokuwa na uwezo wa kumiliki
rasilimali adimu kama vile fedha na anapoweza kusimika kwa uhakika heshima na
hadhi yake, ndani ya jamii iliyomzunguka, mambo hayo humpatia thamani kubwa na
kumrahisishia kazi ya kumpata mwanamke anayemtaka.
Ama kweli kaaaazi kwelikweli..kila kitu hakipatikanai tu kwa kutaka mpaka vita...
ReplyDelete@Da' Yasinta Ni matumaini yangu kuwa umzima wewe na familia yako.......
ReplyDeletenautambua uwepo wako katika Blog hii ya Utambuzi na Kujitambua....
kaluse kaka yangu habari za siku tele umepotea sana ndugu yangu kama u busy ni sawa tu bora uzima mimi ni fan wako mkubwa sana huwa napende sana kutembelea blog yako so nimeona kimya muda mrefu sana kama umerudi utuwekea mambo mazuri tuanze kusoma huwa najifunza mengi sana ktk blog yako ubarikiwe kaka
ReplyDeleteNi jamaa alisema kuhangaika kote kwa mwanaume ni kwa ajili ya mwanamke...sijui alikua na maana gani!
ReplyDeleteAnnony, hapo juu, nimesharejea na sasa utakuwa unanisoma kila siku
ReplyDeleteemu-three... Nimekusoma mkuu
ReplyDelete