0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Jul 4, 2013

KUNA WANAWAKE WANAOWAFUNGASHIA WAUME ZAO NA KUWAPELEKA KWENYE NYUMBA NDOGO...!Hebu fikiria mwanaume anatoka kazini na anapofika nyumbani tu anakutana na ‘kiama’ cha maneno na lawama au kero. Baada ya madhila ya kazi ya kutwa nzima ya kutafuta riziki kwa ajili ya familia, mwanaume hupenda kuona akirudi nyumbani anapata fursa ya kupumua na kusahau adha za kazini.

Lakini anaporejea na kukutana na adha nyingine, kimaumbile hukereka. Kimaumbile binadamu awaye yeyote anapokereka au kutishika atafanya jambo moja kati ya haya mawili. Ama atapambana au kukimbia. Ukiona Simba na kutishika kwa mfano, utaamua kupambana naye au kukimbia.


Kama mwanaume ataamua kupambana na hali hiyo, ni afadhali kwa sababu inaweza kuwa ni kubishana au kupigana (mara nyingi mwanamke kupigwa) Lakini mwanaume anapoamua njia ya pili ya kukimbia maana yake ni kutafuta mahali ambapo akitoka kazini ataachwa apumzike kabla hajaanza kuzogomwa na mahali hapo si pengine bali kutafuta nyumba ndogo itakayompa nafasi ya kupumzika baada ya madhila ya kazini.


Kuna wanawake ambao wanaamini kwamba, wakisema au kulalamikia jambo mara nyingi, yaani kila dakika, basi jambo hilo litatafutiwa ufumbuzi. Huu ni uongo na imani ya hatari sana. Wanawake wengi ni wazungumzaji sana, yaani wanapenda kulikuza jambo tena na tena na tena. Ni kama vile wanajaribu kuingiza maaarifa fulani kwenye kichwa cha mtoto asiyeelewa kirahisi.


Badala ya kuzungumza jambo kwa kifupi na upendo, hata kama ni la kukera, mwanamke ataanza hotuba na kuhubiri kusikoisha. Badala ya kuangalia upande mzuri wa jambo hilo na kuzungumzia upande huo ili taaarifa ifike vizuri zaidi, mwanamke atatafuta udhaifu na kung’ang’ania kuzungumzia upande huohuo.


Wasichojua wanawake hawa ni kwamba, miongoni mwa mambo ambayo wanaume huyachukia ni kuhubiriwa kama vile wamekuwa wasiojua kitu na wasioelewa kitu. Lakini pia kuambiwa jambo mara nyingi kama kwamba wao ni mbumbumbu huwakera sana wanaume kuliko wanawake wanavyofikiria. Tabia hiyo humfanya mwanaume amwone mkewe kama kisirani na kuanza kumkwepa au kumdharau. 


Mwanamke anaposema jambo anatakiwa kusema ni jambo gani hasa analenga, siyo kuzunguka. Anachotakiwa ni kuzungumzia jambo hilo na kutoa nafasi kwa mume kutafakari na kulitolea ufafanuzi au kutekeleza, siyo kukumbushia na ya mwaka juzi. Pia si vyema kukebehi au kumkejeli mume wakati wa kukumbushia jambo. Hii ni kwa sababu wanaume hawataki kukumbushwa ya juzi na wala hawako tayari kuvumilia kukejeliwa……….

 

No comments:
Andika Maoni Maoni

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi