0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Jul 4, 2013

MWANAUME ANAPOKOSA 'CHAKULA' NYUMBANI, HUWEZA KULA CHOCHOTE MTAANI...!Kwa kawaida kadiri mwanaume anavyokosa tendo la ndoa kutoka kwa mwenzi wake ndivyo ambavyo anazidi kujishinikiza kihisia. Kama atakosa tendo kwa wiki nzima mambo huwa magumu zaidi, kwa sababu bila kujijua mwanaume hubadilika na kuwa kama simba au chui mwenye njaa aliye tayari kumvamia na kumjeruhi yeyote.

Nataka niwaambie wanawake kwamba, kama hujitahidi kuhakikisha kwamba, mumeo anamaliza kiu yake, hasa kama ana kiu sana, unachofanya ni kutengeneza mzimu ndani mwako. Mume anayekandamiza hasira za kunyimwa tendo la ndoa na mwenzi wake anakuwa kama mzimu.


Labda niwape siri moja kuhusu athari za njaa ya tendo la ndoa kwa wanandoa. Mkisikia au kusoma katika vyombo vya habari kwamba, mume amemuuwa mke wake kwa sababu ya wivu wa kimapenzi, jaribuni kuchunguza. Inawezekana kabisa, mke huyo kabla hajauawa alikuwa hampi mumewe unyumba, hivyo kumfanya mumewe akusanye maumivu ya kihisia ya kunyimwa unyumba na mkewe yaliyomfikisha mahali pa kugeuka kuwa mzimu uliommaliza mkewe. 


Tafiti nyingi zinakubaliana na jambo hili kwamba, kwa sababu ya uzalishwaji wa mbegu za kiume, homoni ya sili ya testosterone na sababu nyingine, mwanaume huhitaji kufanya tendo la kujamiiana angalau mara tatu kwa wiki ili aweze kuhisi ahueni. Labda tu pale ambapo mwanaume anaumwa, ana matatizo ya kusongeka kiakili au muda mdogo sana, ndipo ambapo anaweza kukaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa. Lakini hata mkewe anapokuwa na matatizo ambayo yanamfanya asiweze kushiriki tendo la ndoa na mwanaume anampenda mkewe, anaweza kabisa kuratibu hisia zake na kumudu kuvumilia. 


Lakini kama inatokana na mwanamke kutojisikia kufanya na kama mawasiliano kuhusu jambo hilo hayajawa wazi, mwanaume hugeuka kuwa mzimu kweli. Kumbuka kuna migogoro mingi sana ndani ya ndoa ambayo chanzo chake ni tendo la ndoa, ingawa wanandoa wanakuwa hawaoni. Wanaume wanahitaji tendo la ndoa zaidi kuliko wanawake na hiyo haina maana kwamba, ni wahuni au wazinzi, hapana. Kama mwanamke atajitahidi kuwa kiongozi wa jambo hili na hasa kufungua milango ya mwasiliano, yeye ndiye atakayenufaika zaidi.


Mwanamke anapaswa kukumbuka kwamba, hamu ya mwanaume kwenye tendo la ndoa ni kama mwito wa kimwili kama ilivyo njaa. Je, mtu akikosa chakula akipendacho hawezi kula chochote ili kuuwa makali ya njaa? Hiyo hufanyika sana………..! 

No comments:
Andika Maoni Maoni

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi