Leo tuzungumzie madhara sita ya kutoa mimba na madhara yake kama tutakavyoona hapa leo.
UNAWEZA KUPOTEZA UHAI
Ukitoa mimba unaweza kupoteza maisha kutokana na ukweli kwamba mara
nyingi ndani ya wiki moja baada ya kutoa mimba mwanamke anaweza kuvuja
damu sana, au kupata madhara ya dawa za usingizi, mabonge ya damu kwenye
mishipa ya damu na mimba iliyotunga nje ya uzazi.
WATOTO KULEMAA UBONGO
Utoaji wa mimba huaribu mlango wa mfuko wa uzazi kushindwa kushika
vizuri na matokeo yake mwanamke huyu hujikuta akizaa kabla ya muda
(njiti). Lakini pia watoto hawa wanaozaliwa kabla ya muda maalumu na
viungo ambavyo havijakomaa hupata shida ya ubongo na kujikuta wakipata
ulemavu wa ubongo maisha yao yote.
MIMBA NJE YA KIZAZI
Mfuko wa uzazi una utando maalumu ambao hufanya mimba iliyotungwa kwenye
mirija iitwayo Fallopian kuwezesha yai kushuka hadi kwenye mfuko wa
uzazi. Lakini utoaji wa mimba huathiri mirija hiyo na kupoteza utando
huo na kusababisha mimba kukua nje ya mfuko wa uzazi.
KANSA YA KIZAZI
Wanawake wengi waliowahi kutoa mimba wanapoteza uwezo wa kuzaa, hivyo
kuwa wagumba. Hii inatokana na madhara makubwa waliyoyapata kwenye mfuko
wa uzazi baada ya mimba kutoka kwani mfuko huwa na kovu.
KUATHIRIKA KISAIKOLOJIA
Baadhi ya wanawake waliowahi kutoa mimba, hujutia kitendo hicho, hivyo
kuathirika kisaikolojia. Wengine huweza kusikia sauti ya mtoto akilia
wakati hakuna mtoto huyo jambo linalowaweka katika mazingira magumu.
Kufautia hali hiyo, hujikuta wakishindwa kuwa na ufanisi mzuri wa kazi na masuala mengine ya kijamii.
Jan 27, 2016
Madhara sita ya kutoa mimba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Andika Maoni Maoni