Inawezekana ukawa ni mke wa mtu au una mpenzi wako ambaye mna
matarajio ya kufunga ndoa na kuishi pamoja. Kuna wakati unaweza kujaribiwa na
kujikuta ukikabiliwa na hatari ya kumsaliti mpenzi wako. Kujaribiwa huko
kunaweza kukutokea katika mazingira mbalimbali kutegemea na maeneo yako ya kazi
au mahali unapofanyia shughuli zako za kila siku. Kwa mfano inaweza ikatokea
umefahamiana na mwanaume mahali pako pa kazi, anaweza kuwa ni mteja au
mfanyakazi mwenzio. Inatokea siku moja anakualika kwa ajili ya chakula cha
mchana, baada ya mtoko huo, unajisikia kutoka naye kwa mara nyingine…………………
Kutoka kwenu mara kwa mara kwenda kupata chakula cha mchana,
unagundua kwamba huyu bwana ni mtu mwenye kiwango cha juu ya usikivu, katika
mazungumzo yenu anaonekana sana kwamba ni mwelewa na mwenye subira. Hana papara
katika kuzungumza na mara nyingi huwa ni msikilizaji. Huyu unaweza kumwita
rafiki ingawa ni wa jinsia tofauti, (Sidhani kama ni dhambi kuwa na rafiki wa jinsia tofauti……!)
Kuna kitu wenzetu wazungu wanakiita Emotional infidelity, kwa
tafsiri yangu naweza kusema ni hisia za usaliti katika mapenzi. Maana yake ni
kwamba unaruhusu mtu mwingine wa jinsi tofauti azibe pengo la hisia ambalo
lingetakiwa lizibwe na mpenzi wako au mume wako.
Kama inavyofahamika kwamba wanawake ni viumbe wa hisia,
wanapenda sana kusikilizwa, na wanapenda kuona wapenzi wao au waume wao
wanawasikiliza. Inapotokea hitaji hilo halitekelezwi na mpenzi au mume wake,
basi ni rahisi sana atakapotokea mtu mwingine ambaye bila kujua akamudu kuziba
pengo hilo kuvutiwa naye na kuhitaji kuwa naye karibu mara kwa mara.
Hapa chini nitazitaja dalili ambazo zitakuonyesha kwamba
ukaribu wako na huyo rafiki utakupelekea kuisaliti ndoa yako:
1. Unatamani sana kumuona ukiwa na shauku kubwa ya kuwa naye karibu na kutumia muda mwingi kuwa naye
2. Unajikuta ukichagua mavazi na kujikagua sana ukijiuliza
jinsi atakavyo vutiwa na mavazi yako pale atakapokuona
3. Unapokuwa naye unajikuta ukimweleza matatizo ya mahusiano
yako na mpenzi wako au mumeo
4. Unajikuta ukimgusa gusa wakati mkiongea au kufanya naye
utani unaoweza kupeleka ujumbe tofauti kwake kwamba labda umevutiwa naye
kimapenzi
5. Unawsiliana naye kwanza kabla ya kuwasiliana na mpenzi
wako au mumeo pale unapokabiliwa na jambo lolote lenye kutatiza na linalohitaji
msaada wa haraka au ushauri
6. Unajikuta ukiwaza jinsi gani ungekuwa na amani iwapo
ungekuwa na uhusiano naye wa kimapenzi au ndoa
7. Inawezekana ukawa unamzuingumzia sana kwa mwenzi wako au
kwa marafiki zako, au inawezekana ukawa humzungumzii kabisaaa na kuficha
urafiki wenu.
8. Unajitahidi sana kuficha urafiki wenu na kutomzunguimzia
rafiki huyo kwa mwenzi wako kwa sababu unajua kwamba jambo hilo linaweza
kukuletea balaa.
Kwa ujumla unapojikuta umempata rafiki wa jinsia tofauti na
yako halafu ukahisi kulipukwa na moyo juu yake zikiwemo dalili nilizozitaja
hapo juu, basi ujue uhusiano wako na mume au mpenzi wako uko mashakani. Usipokuwa
makini utamsaliti.
Ni kwel kwamba wanaume ukisha kaa na mwanamke yeyote kwa cku kazaa unakuta unatamani uwe na mahusiano nae
ReplyDelete