0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Apr 13, 2011

MWANANGU SHEYLA KALUSE ATIMIZA MIAKA 7 LEO

Sheyla miaka 7 sasa Rankim miaka 9 sasa

Sheyla akininong'oneza jambo!


Hapa akisubiri nimjibu


(Picha hizi zimepigwa na Fadhy Mtanga)


Tarehe kama ya leo, ndio siku ambayo binti huyu alizaliwa, ilikuwa ni furaha kwangu na kwa mzazi mwenzangu kuzaliwa kwa binti huyu ambaye alitanguliwa na kaka yake Rankim aliyezaliwa miaka miwili iliyopita kabla yake. Mwenetu Rankim alitimiza miaka 9 hapo mnamo tarehe 28/02/2011.


Kwa niaba ya sisi wazazi wa watoto hawa tunapenda kutoa pongezi kwa wenetu hawa wawili kwa kutimiza miaka. Mungu awajaalie wakue kwa umri na kimo ili wapate kutimiza ndoto zao.

11 comments:
Andika Maoni Maoni
 1. Nachukua nafasi hii na kuwapongeza sana watoto/shangazi zangu Rankim na Shyla kwa kutimiza miaka. Ingawa miezi kadhaa imepita kwako Rankim si kitu HONGERA SANA. Nawe dada Shyla miaka saba leo HONGERA SANA nawatakieni na kuwaombea kwa Mungu ndoto zenu zitimie na muwe watoto wasikivu ,watii na wenye upendo kwa kila mtu. Hongera pia wazazi kwa kuwalea watoto hawa. Uwe na siku njema Sheyla.....usininyime keki hiyoooo...lol

  ReplyDelete
 2. nachukua fursa hii kukupa pongezi wewe kama mzazi...nampa pongezi mzazi mwenzako....

  Nampa pongezi Sheyla kwa kutimiza miaka 9.

  Naikumbuka siku ya Jumamosi asubuhi niliwapigeni picha. Jioni nikawa nawe Movenpick...lakini ilipofika Jumapili, mwenyezi Mungu akaninusuru kifo mbele ya mdomo wa bastola.

  Ninamshukuru sana Mungu kwa kuwa na rafiki kama ninyi wanablog wenzangu.

  Happy birthday Sheyla

  ReplyDelete
 3. nimekosea. Hongera Sheyla kwa kutimiza miaja 7 siyo tisa kama nilivyoandika awali

  ReplyDelete
 4. Hongera Sheyla,hongera wazazi kwa kumzaa na kumkuza Sheyla hata leo ametimiza miaka saba

  ReplyDelete
 5. Happy birthday Sheyla na Rankim..... Jamani watota wazuri kama baba yao.

  Swali la kizushi: Kaka Shaban hapo Sheyla alikuwa akikunong'oneza nini?

  ReplyDelete
 6. Koero! kama mama nadhani hapo shangazi yetu Sheyla anamnongóneza babake kuwa, baba, je? utaninunulia keki?

  ReplyDelete
 7. Hongera wazazi kwa malezi na Mungu awaongezee hekima na maarifa ya malezi.

  Hongera binti kaluse na Mungu akuongoze katika maisha yako!!!!

  ReplyDelete
 8. ha ha ha ha haaaaaaaa hapo hata mie mpiga picha nilisahau kuuliza Sheyla alimnong'oneza nini baba yake. Shaban tuambie tafadhali.

  ReplyDelete
 9. Mi naona alimwambia hivi:
  Baba nimekubakshia biscuit.

  ReplyDelete
 10. Namii sijachelewa kukupa hongera ndugu yangu. HONGERA MKUU. na HAPPY BIRTHDAY KWA WATOTO WETU.
  Jukumu kubwa kwa mzazi ni kuwajibika kwa watoto hasa ELIMU...Na hivi sasa hapa bongo mwamko ni mkubwa, ila GHARAMA...WALISEMA KAMA UNAONA ELIMU NI GHARAMA JARIBI UJINGA. Haya ni mawazo tu mkuu! Nakupa pongezi kwa majukumu hayo makubwa
  Hongera kwa familia nzima, kwa siku hiyo muhimu!

  ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi