UJAUZITO ni safari ndefu inayomchukua
mwanamke miezi tisa au majuma arobaini hadi kujifungua. Ni safari yenye
mikikimikiki na hatari nyingi kwa mama na mtoto. Tusichukulie suala la ujauzito
kama jambo la kawaida ingawa pia ni wajibu kwa mwanamke.
Ujauzito siyo hali ya hatari au
kutisha endapo mambo ya msingi yatazingatiwa kabla ya kuwa mjamzito na kipindi
cha ujauzito hadi baada kujifungua.
Katika kipindi cha ujauzito kuna
mambo mengi ambayo ni mabadiliko humtokea mama na mtoto aliye tumboni.
Katika makala haya tutazungumzia
mambo ya kuzingatia kabla ya kuamua kubeba mimba, siyo kila mwanamke anaweza
kubeba mimba kwa sababu wengine huwa na matatizo katika mfumo wao wa uzazi,
aidha homoni zao hazifanyi kazi vizuri na mayai hayazalishwi au hayapevuki.
Huenda pia mirija ya uzazi imeziba au
ana matatizo ndani ya kizazi.
NINI CHA KUFANYA?
Ni vyema upange sasa unataka kuwa
mjamzito au mwezi fulani unataka kushika mimba, uwe na mpango. Hata hivyo,
hakikisha umri wako upo zaidi ya miaka 20 kwa usalama zaidi wa afya yako.
Mshirikishe mwenzi wako na mwambie ungependa upate ujauzito, siyo vizuri
kushtukiza kwani inaweza kukupa ‘stress’ wewe mwenyewe au mwenzako endapo mmoja
wenu hajajiandaa kisaikolojia.
CHEKI AFYA YAKO
Hakikisha una afya njema, huna
magonjwa sugu kama kisukari, shinikizo la damu, magonjwa mengine ya moyo,
kansa, HIV, kifafa, pumu, siko seli au grupu lako la damu ni RH Negative.
Endapo una matatizo haya hapo juu,
basi haraka wasiliana na daktari wako wa masuala ya uzazi akupe ushauri kwani
magonjwa mengine yatakusumbua wakati wa ujauzito, au magonjwa yenyewe
yatamwathiri mtoto.
Hakikisha huna magonjwa au matatizo
katika viungo vya uzazi, mfano kutokwa na uchafu ukeni wenye muwasho na harufu
mbaya, vipele au vidonda sehemu za siri, maumivu wakati wa tendo la ndoa,
kutokwa na damu au usaha ukeni. Vile vile mfumo wako wa uzazi uwe vizuri,
matatizo katika mfumo wa uzazi ni kama vile maumivu ya tumbo chini ya kitovu,
kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi, kutopevusha mayai na kukosa hamu ya tendo la
ndoa.
VILEVI ACHA
Epuka unywaji wa pombe na uvutaji wa
sigara, hili hata kwa mwanaume anayetaka mtoto. Mwanamke kabla ya kuwa mjamzito
hakikisha unakula sana mboga za majani ili upate kiwango kizuri cha vitamin ya
Folic Acid, ni vema ule sana mboga za majani au upate virutubisho vya Folic
Acid. Endapo hutakuwa na kiwango kizuri cha Folic Acid, kuna hatari ya kuzaa
watoto wenye matatizo.
MAZOEZI
Fanya mazoezi mepesi mara kwa mara
ili kuimarisha nyonga na viungo vyako vingine na usipate matatizo wakati wa
kujifungua. Pata ushauri wa daktari kipindi muafaka.
Tibu magonjwa yanayoathiri mfumo wa
uzazi, mfano maumivu ya korodani, maumivu ya njia ya mkojo, upungufu au ukosefu
wa nguvu za kiume. Kutoa manii mepesi sana kiasi kwamba baada ya tendo la ndoa
manii zote zinatoka ukeni.
Udah punya Asuransi belum? Pasti belum, iya kan. Yuk baca artikel berikut Asuransi Kendaraan MSIG, Berkendara Tanpa Cemas kali aja setelah baca artikel berikut langsung kepincut beli asuransi. Asuransi itu penting loh.
ReplyDelete??
ReplyDeletelink text
ReplyDelete