0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Nov 23, 2008

MAONI YA MUBELWA BANDIO.

Haya ni maoni ya msomaji na mwanablog Mubelwa Bandio.
Hebu soma maoni yake hapa chini.

Hii mara zote ni hatua ya kwanza ya mtu kuelekea aelekeako. Yaani wafanikiwao, wajiuao, wajikwamishao na kotekote yategemea na maamuzi yatokanayo na kujitambua. Lakini pia kuitambua sasa kwa kuwa kama ulikosea ama kukoseshwa katika maisha yaliyopita, bado una nafasi ya kutambua kuwa ulikuwa ukitenda ama kuamua visivyo na sasa unajitambua na kuanza upya.Unajua tuna usukani wa maisha yetu na pasina kujitambua hatutajua tuendako hata kidogo.`Wale wasiojitambua na wenye kuwatambua ama niseme kutambua baadhi ya wengine na wao kutamani kuwa kama wao, huishia kuiga maisha ya kina fulani katika harakati za kujitambua na matokeo yao hujipoteza wao. Kama ambavyo tunaona watu wakifanya ukatili kutaka kudhihirisha kuwa wao ni wababe. Watu wanafanya ubakaji na kuua kutafuta mafanikio ndani mwao. Ndio hayahaya aliyouliza Ziggy Marley kwenye wimbo wake Into the Groove kuwa "why wo loose ourselves just to find who we are?" Ni utambuzi mwema na kila asomaye na ajitambue, atambue aendako kisha kwa pamoja tutaitambua na kuikomboa jamii. Hii ni CHANGAMOTO YETU sote

1 comment:
Andika Maoni Maoni
  1. ni maelezo mazuri na mimi sidhani kama wanaofanya yale uliyoyasema wanatafuta kujitambua ndani mwao, bali wanataka kujitambu nje yao. wanataka tuwakome na kuwatambua kwamba ni wauaji nk badala ya waowenyewe kuchagua wanavyopenda/paswa kuwa.

    wanashindwa kujua kwamba wao wamekamilika na ukamilifu wa kwamnza upo ndani mwao na sio nje yao.
    mdada asipoambiwa kapendeza, basi hujisikia vibaya wakti mtu wa kwanza wa kujua na kusema kama kapendeza ni yeye mwenyewe na mengine ni nyongeza ambayo haiongezi wala kubadili chochote. kimsingi tumekamilika sisi kama sisi

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi