Eti hujitongozesha kwa mabosi!!!
Kuna dhana kwamba wanawake walioajiriwa wanakabiliwa na mazingira ambayo yanawalazimisha kuingia kwenye vitendo vya kutoka nje ya ndoa zao, ukilinganisha na wanawake ambao hawajaajiriwa hususani mama wa nyumbani jambo ambalo katika maisha ya kawaida bila utafiti linaonekana kama vile ni kinyume yaani akina mama walio majumbani ndio ambao hutoka nje zaidi.
Niliwahi kuwahoji wanawake kadhaa jijini Dar, mwanamke mmoja kati ya watano alikiri kwamba yuko tayari kujitongozesha kwa bosi ili kujaribu kulinda nafasi yake kazini au kupandishwa cheo. Nilifanya mahojiano hayo ili kujua idadi wanaume wanaotumia nafasi zao kazini kuwadhalilisha wanawake kijinsia.
Lakini bila shaka suala la mapenzi kwa wanawake walioajiriwa lina nguvu na kwa hiyo limekuwa likifanyiwa tafiti katika sehemu mbalimbali duniani. Tofauti na tafiti ambazo zimefanywa hivi karibuni zinaonyesha kwamba mwanamke mmoja kati ya kumi walioajiriwa huwa anaonyesha tabia za kimapenzi au kujitongozesha kwa bosi wake.
Tafiti hizi zinaonyesha kuwa yule mmoja kati ya kumi ambaye hujitongozesha kwa bosi huishia kutembea naye au hata kuolewa naye kama hana mume na pengine kuvunja ndoa yake. Inaelezwa pia kuwa mmoja kati ya wanawake kumi wanaojitongozesha kwa mabosi huwa anapandishwa cheo. Hii ina maana kwamba wanawake wanaopandishwa vyeo kwenye maeneo ya kazi huenda mmoja kati ya kila kumi hupandishwa kwa sababu za kimapenzi hata hivyo siyo lazima iwe hivyo.
Katika mahojiano na jarida moja nchini Marekani mwanamke mmoja kati ya watano alikiri kwamba yuko tayari kujitongozesha kwa bosi ili kujaribu kulinda nafasi yake kazini au kupandishwa cheo. Jarida hilo halikufanya mahojiani ili kujua idadi wanaume wanaotumia nafasi zao kazini kuwadhalilisha wanawake kijinsia.
Wanawake wenye watoto ambao walihojiwa kwenye tafiti hizo walisema kwamba ajira zinawasumbua na wamefikiria kuwa ni ngumu kujigawa kazini na nyumbani kishughuli.
Tafiti hizo hata hivyo hazikulenga katika kuonyesha kwamba wanawake ni dhaifu bali huenda zimelenga katika kuonyesha kwamba idadi ya wanawake wanaojitongozesha kwa mabosi ni ndogo kuliko inavyotazamwa au kuaminika na pia kuonyesha kwamba bado wanawake walioajiriwa wako kwenye nafasi kubwa zaidi kushiriki mapenzi kuliko wale walioko majumbani. Ni juu ya wanawake ambao wanadhani ni halali kuuza thamani zao kwa ajili ya kazi kubadili mwenendo huo..

Kaka Kaluse, ni tafiti nzuri. Nami pia katika maisha ya kazini huku na kule nimeyaona mambo kama hayo.
ReplyDeleteHii mada ni nzuri sana na ni ya kufundisha/kuelimisha. Ningependa wengi wasome. Inasikitisha sana kuona watu wanachukua njia ya mkato, badala ya kuongeza elimu na kupandishwa cheo. Pia hii inawezekana ni kutokana na kupata mishahara midogo na maisha sasa yapo juu. Au labda wote mabosi na wanawake hawatosheki na ndoa zao mume/mke wake. Na inawezekana mabosi wanataka tu kuwadharau wanawake kuonyesha kuwa yeye anaweza kufanya kama atakavyo. Na wanawake kwa kuogopa wanakubili tu.
ReplyDeleteDUH!
ReplyDeleteLabda sitoki nje sana ya TOPIC!:-(
Nilisoma sehemu kuwa wanawake watambuliwao na jamii kuwa ni wazuri, kwa kawaida hupandishwa cheo haraka na hata kulipwa mshahara mkubwa kirahisi kuliko wale jamii ifikiriao wanalia wakati wanacheka.
Na hii ilidaiwa WAZURI hupendelewa hata na wenye uhakika hawataonjeshwa!:-(
Na katika jarida hilohilo lililofanyiwa uchunguzi katika nchi za Scandinavia lilidai pia kuwa mara nyingi wanawake makazini huwalalamikia wanaume ambao wanawake wanaamini sio MAHENDISAMU makazini . Ina maana makazini kama kuna jamaa MADEMU waaminio ni hendisamu, linaweza hata kumshika tako mwanadada likachekewa,
WAKATI weye mwenzangu na mimi unaweza shitakiwa kwa sexual harrasment kisa unamchekeachekea Kigoli tu na anachukia umkenuliavyo meno.
Lakini mie sijui sana mitazamo ya WANAWAKE kwa kuwa hawa VIUMBE wananipa sana taabu kuwaelewa.
NIKIJIONGELEA BINAFSI...
..... tokea sekondari mpaka makazini miye binafsi NSHA tamani kuanzia Mwalimu wa kike mpaka bosi wa kike na bila kufikiria maswala YA kupasishwa Mtihani au Kuongezwa mshahara.Hapa naongelea PURE kutamani tu kwa kuwa Kibosile na Mwalimu Mhusika alikuwa amejaliwa vikorombwezo vinitiavyo majaribuni kwa TAMANIO.:-(
DUH!:-(