Hivi huyu nishamuona wapi?
Kuna wakati unakuwa mahali, halafu unahisi kwamba ulishakuwa mahali hapo kabla, na pengine ukiwa na watu wale wale. Lakini, kwa unavjojua, hujawahi kuwepo hapo, wala kuwa na kuwa na watu hao.
Hali ya uzoefu huu kufahamika kitaalamu kama Déjà vu. Kama nilivyosema awali kwamba, unakuwa katika sehemu ngeni unashangaa kuona kama kwamba, ulishawahi kwenda sehemu hiyo huko nyuma.
Unaona na mtu kwa mara ya kwanza lakini unapata mawazo kama uliwahi kuonana naye huko nyuma. Hiyo ndiyo Déjà vu.
Neno Déjà vu, asili yake ni lugha ya kifaransa ikiwa na maana kwamba, Tayari nilishawahi kumuona au mahali hapa niliwahi kupaona kabla, ikiwa na maana kwamba mtu anakutana na kitu kipya katika mazingira mapya na anagundua kwamba aliwahi kukumbana na hicho kitu kabla, pengine katika mazingira hayo hayo.
Inasemekana kwamba, mambo haya ya Déjà vu ni ya kawaida. Kila watu saba katika kial kumi wanasema kwamba waliwahi kuukumbana nayo angalau mara moja katika maisha yao.
Neno hili Déjà vu lilitumiwa kwa mara ya kwanza na Emile Boirac (1851-1917), ambaye alikuwa mtafiti wa Kifaransa wa mambo ya akili za ziada za watu. Kuna maelezo mengi ya uzoefu huu, kama ifuatavyo: Unakutana napicha kwa mara ya kwanza lakini unagundua kwamba uliwahi kuiona zamani.
Unafika mahali pageni na unagundua kwamba, mahali pale si pageni bali uliwahi kufika kabla. Lakini, kwa akili ya kawaida, unakumbuka kwamba hujwahi kufika hapo. Unaiona sinema mpya lakini unahisi kwamba uliwahi kuiona kabla. Na cha kushangaza ni kwamba unaweza hata kutabiri kitendo kitakachofuata na ikawa kweli, lakini hukumbuki na pengine hujawahi kuiona, kwani ni sinema mpya.
Unakumbana na hali fulani au unafika mahali fulani pageni lakini unagundua kwamba hali ile au mahali pale uliwahi kupaona katika ndoto zako huko nyuma.
Déjà vu pia inaweza ikaonekana katika unusaji, ladha ya chakula, mchanganyiko wa rangi, sauti ya juu au ya chini, kelele au kitu chochote ambacho kinafukua kumbukumbu ya mambo ya zamani.
Mtu mgeni aliye mmbele yako uvaaji wake na namna anavyoongea anaweza kukukumbusha mtu uliyekuwa umekutana naye kabla. Baadhi ya watu wanasema kwamba hali hii ya kufanana inaweza kusababishwa na hali ya ubongo kwa wakati huo.
Watu wanaamini kwamba binadamu baada ya kufa roho yake inaingia katika mwili wa mwingine, wanasema kwamba kwa mujibu wa Déjà vu waliwahi kukumbana na hali kama hiyo zamani. Kunaweza kukawa na sababu na maelezo chungu nzima kuhusu Déjà vu.

Mtambuzi nakubaliana na wewe. Unajua nimesoma makala hii nikijilinganishia na matukio yaliyowahi kunipata mwenyewe nikajikuta najisemea 'lakini kweli'.
ReplyDeleteBwana Shabani, kwangu huwa ajabu kidogo. Mara nyingine napoenda mahali pageni au kukutana tukio fulani huwa inakuwa kama nakumbukia movi flani ambayo kimsingi nilipaota! Inakuwa kama kile nilichoota kinakuwa halisi. Sijui.
Siijui nadharia hii na hitamisho lake, lakini observation iliyofanyika ina ukweli.
Bila shaka tutapata elimu zaidi kuhusu hili. Asante sana.
Kwanza habari za siku nyingi kaka Bwaya, nashukuru umerudi maana tulikukosa sana mtandaoni.
ReplyDeleteKuhusu mada hii ni kweli kabisa uliyoyasema kwani hata wakati naiandika nilikuwa najua itawafikirisha wasomaji na ukweli utaonekana, mimi sio mtaalamu wa kuchunguza mambo ya kale lakini kuna wakati huwa napambana na chanagamoto nyingi ambazo zinanipeleka katika kuzifanyia utafiti, na hili lilikuwa ni mojawapo...Bado naendelea na utafiti huu.
Tuko pamoja kaka....
Kusema ukweli kaka Shabani, mambo mengine sijui nisema ni kama miujiza au nini..... yaani jambo hili huwa linanitokea sana lakini nilikuwa naogopa kulisema kwa kuhofia kuitwa mshirikina, kuna wakati niliwahi kumsimulia mama yangu akaniambia eti hayo ni mambo ya kishetani.....
ReplyDeleteKama kaka Bwaya na mimi nasubiri matokeo ya utafiti huo ili nijifunze zaidi
Mmmh Jambo hili huwa linanitokea mara nyingi sana. Nami nasubiri utafiti huo.
ReplyDeleteMmhhhh!! Sasa mbona hiyo idadi ya 7 kati ya 10 yaweza kuwa ndogo? Maana hakika yanawakumba wengi na wengine wanayatumia haya kujipanga na kufanya mambo yanayowafanikisha na wengine yanayowarudisha nyuma. Kwa ujumla wenye kufuata hali hizi ni miongoni mwa watu wanaoaminika kuwa wana-take risks na wenye kufanikiwa wanaonekana kuwa na visions za mbali na wanaoshindwa wanaonekana kama walikuwa na nightmares.
ReplyDeleteSina hakika kama litapatikana suluhisho la hili maana ni imaginary zaidi ya reality.
Blessings Kaka