0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Jun 25, 2009

FEDHA ZINAPOGEUZWA MHIMILI MKUU KATIKA MAISHA

Hata uwe na fedha kiasi gani haziwezi kukupa furaha

Kuna imani zisizo sahihi zilizoenea kuhusu pesa ambazo miongoni mwa imani hizo ni zile zinazodai kwamba utajiri hutuongoza kwenye amani ndani ya nafsi zetu, na kutupatia furaha, faraja, heshima na thamani ya nafsi zetu.

Katika tamaduni zinazo abudu majivuno na si maadili, na zinazoheshimu vitu vyenye thamani isiyo ya kudumu, yaani thamani ya nje, ni rahisi kudhani yule mwenye vitu vingi vya kuchezea anaishi vizuri zaidi ya yule mwenye kutafuta maisha ya msingi na ya furaha zaidi.

Bila kujua tunachagua fedha, hiki kifaa cha kuchezea tunachokiona muhimu sana kwa maisha yetu, kuliko maisha ya kiroho, kwa kuamini kwamba fedha ni tiba na ni jibu kwa matatizo yetu yote. Kumbuka, nikisema maisha ya kiroho, sina maana maisha ya kidini. Nina maanisha maisha ya kutambua jambo kubwa kuliko wewe mwenyewe.

Haishangazi kuona harakati za kutafuta vitu visivyo muhimu vya thamani, huwa ndilo jambo tunalolipa umuhimu zaidi. Tunakua tayari kujitoa mhanga katika mengi ili kutafuta fedha (tunakua tayari hata kuhatarisha ama kupoteza roho zetu za thamani kubwa katika kutafuta vitu vya thamani ambavyo tunadhani ni vya muhimu na vyenye thamani hata kushinda roho zetu), lakini badae tunagundua kwamba haikupaswa iwe hivyo.

Tunapogundua kwamba tunafika huko hatupati furaha tunayotarajia, hutufanya tutambue kwamba cha muhimu ni furaha na si fedha kama tulivyodhani.

Imani nyingine siyo sahihi, inatokana na baadhi ya vitabu vya dini, kwamba fedha ndio msingi wa maovu yote duniani (kama vile hakuna kitu chochote cha thamani zaidi ya kuwa maskini wenye kushindwa kujisaidia hata katika matatizo madogo na ya familia yake, acha ya jamii yako).

Kutokana na imani hiyo, baadhi ya watu hujijengea tabia ya kuchukia fedha na kutoa shutuma kubwa kwa fedha.

Hata hivyo tatizo la kweli si fedha, bali ni choyo, ubinafsi na uroho wa fedha (uroho wa fedha unaowafanya watu kutumia njia zozote hata za hatari katika kuipata), ndicho kiini cha maovu yote duniani.

Fedha huandamana na malengo ili iweze kuwa na nguvu kuleta mabadiliko katika maisha ya watu. Wakati kile tunachofanya nacho kinahisia za malengo yaliyopandikizwa na kupewa uhusiano wa lazima na fedha, ndio sababu inayozusha mchakato wa hatari wa kutafuta fedha kiasi kwamba hivi sasa hatua hizo zinaonekana kama malengo yenye sababu na ya muhimu ingawa yanaumiza.

Fedha ambayo kwa kweli ni kitu kilicho huru, haina haja ya kuabudiwa, wala kupotezwa hovyo. Tunachotakiwa ni kuifurahia na kuitumia kwa busara na ni bora ikiwa itatumika kwa malengo muhimu. Ni ukweli ulio wazi kwamba, huwezi kuondoka duniani na fedha uliyoichuma kwenda nayo kwenye maisha baada ya kifo, na kwa ukweli fedha hukupatia uhakika wa usalama usio na ukweli.

Maisha yanaweza kwa kuonekana magumu, na ukweli kwamba kwa jinsi unavyokua kwenye kiwango cha juu ya fedha, ndiyo inavyokua na uwezekano mkubwa kuzama kwenye mambo machafu, yanayokuondolea furaha.

Ni vema tukaepuka kuweka uzito mkubwa kwa fedha, iwezayo kuja na kuondoka, na tukatoa umuhimu katika makuzi ya kiroho, jambo ambalo haliwezi kubadilishwa wala kuchukuliwa na watu wa nje na inakupa ushindi bila kujali kule maisha yanapokupeleka.

Inatakiwa kuwepo sababu Ni wazi hakuna mtu anayeishi huku akifikiria kwamba lengo lake la maisha ni kufikiria ni ace cream au ni peremende ama keki ngapi atakula kabla ya kufikiri. Hivyo ndivyo kuna ulazima wa mtu kukaa chini na kufikiria ni kitu gani kilicho muhimu kwa maisha yake.

Jiulize ikiwa kile unacho kifanya kinakuelekeza kwenye kutimiza lengo la kuwepo kwako duniani au kinakupeleka njia iayo sahihi.

Kumbuka duniani unapoishi hakuna nafasi ya kufanya majaribio ya kuishi kabla hujaingia kwenye maisha halisi ya dunia bali hapa ndio nafasi yako pekee na ya mwisho ya kuishi duniani.

Pengine kitu kinachoweza kukupa uwazi zaidi ni kujiuliza kila siku kabla ya kufumba macho yako na kulala. ‘Ninaishi ili nifanye kazi ama ninafanya kazi ili niweze kuendelea kuishi?’.

Njia nyingine ni kutambua kile unachokiona cha thamani zaidi katika maisha yako na hili unaliweza kwa kujiuliza . ‘Nini ningefanya kama ningepewa taarifa kwamba nina miezi sita tu iliyobakiya kuishi?’ Hii itakusaidia kuepuka makosa yaliyofanywa na watu wenye fedha, watu wa kundi la walionacho walioamini ni lazima wawe wanachama wa vilabu vya walio na fedha ili waweze kuishi.

Kwa vile kitu chochote kikizidi sana hugeuka laana, kuweka usawa ni jambo muhimu. Toa nafasi sawa katika mambo yako ya kidunia na kutafuta fedha na ya kiroho. Narudia tena nikisema kiroho sizungumzii dini, ingawa inaweza kuhusika. Nazungumzia kujua lengo lako maishani na kuifanya dunia kua mahali bora pa kuishi, kwako na wengine wote.

Tunapo weza kuweka uwiano wa utafutaji wetu wa dunia na kiroho, maisha yanakua ya furaha ya kweli na yanakua na udhoefu wa kuridhika tutakaofurahia kuishi ndani yake.

Kwa kufanya hivyo tunajipatia zawadi kubwa kushinda zote ambayo ni amani na utulivu akilini na furaha ya kweli inatotokana na kujua kwamba sababu ya maisha ni kitu fulani hata ikiwa tutamsaidia mtu na kufanya maisha yetu yabadilike bila kujali mchango huo ni wa kinyenyekevu kiasi gani.

Wazo hili hueleweka zaidi kwa kutumia maneno ya Ralph Waldo Emerson aliyewahi kusema ‘maisha ya mtu huwa mazuri zaidi unapojua mwingine ameweza kupumua kwa urahisi zaidi kwa vile yeye anaishi huku ni kufanikiwa.

Nani aliyesema huwezi kuwa na vyote? Ni wazi unaweza. Ukweli ni kwamba, hali asilia ya roho zetu ni ya matumaini kamili, ikiwa imetawaliwa na maana halisi ya furaha ya kweli na kuridhika.

Cha muhimu ni kuweka uwiano mzuri kati ya utafutaji wako wa utajiri wa kidunia na dunia ya kiroho. Kumbuka ya fedha ni huduma na ipo kwa ajili ya kuhudumia na si vinginevyo.

Wakati fedha inapopatikana katika njia za kizamani, (kwa njia za uaminifu na haki) kutumika kama chombo muhimu cha kuondoa tofauti, maisha yanakua ni uzoefu wa kusisimua badala ya kua tatizo linalohitaji kutatuliwa. Na hiyo ndiyo siri kubwa iliyofichwa yakutafuta heshima na matumaini.

3 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. Kaka, ahsante sana kwa mada nzuri sana. Huwa najiuliza mara nyingi kama kweli pesa inaleta furaha.
    Maswali yamezidi kunichanganya tangia mwezi Agosi 2006, nikiwa ndani ya daladala nikakutana na kijana aliyevaa tshirt yenye maneno haya, "whoever said money can't buy happiness; doesn't know where to buy."
    Mi hadi leo I don't know where to buy.

    ReplyDelete
  2. Umesema kweli kaka Shaban watu wengi sana wanafikiri ukiwa na pesa basi huna matatizo tena.Hawajua kama mtu unaweza kuwa na kila kitu pia pesa lakini bado hutakuwa na raha kama hapa hapo juu alivyosema kaka Fadhy nanukuu "whoever said money can't buy happiness; doesn't know where to buy."

    ReplyDelete
  3. Asante kwa kutukumbusha hili Mkuu!

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi