Wanawake
wengi hukabiliwa na matatizo yanayohusiana na mihemko, ukilinganisha na
wanaume. Maradhi kama shinikizo la juu au la chini la moyo, kiarusi, kupoteza
mwelekeo katika hedhi na sasa kansa. Nasema na sasa Kansa kwa sababu, huko
nyuma hakuna aliyekuwa akijua kwamba, kansa kwa sehemu kubwa huchochewa na
sononi za kimaisha. Hivi sasa kuna ongezeko kubwa sana la wanawake wanaougua
kansa ya matiti na kizazi. Msisistizo mkubwa unawekwa kwenye kupima ili mtu
aweze kuwahi kutibiwa. Lakini, hakuna anayejua chanzo kinachopelekea matatizo
haya ya kansa.
Wataalamu
hivi sasa wanakiri kwamba, kansa kama ile ya kizazi, uvimbe wake hukua haraka
zaidi kwa wanawake ambao wanakabiliwa na sononi za kimaisha. Ugunduzi huu
unamaanisha kwamba, kuna uhusiano wa karibu wa kibailojia kati ya sononi au huzuni kali na kansa. Kuna ukweli mkubwa kuhusu jambo hili hasa mtu anapopitia tafiti kadhaa zenye kuzungumzia jambo hili. Kwa mfano kuna wanaosema au kuamini kwamba, misukosuko ya kimaisha kama vile talaka au kutelekezwa kunaweza kuwasababaishia wanawake kansa.
Kansa inayotokana na misukosuko hii ya maisha, hujitokeza baadae sana kwenye maisha ya mtu, kwani hukua polepole. Hii ina maana kwamba, misukosuko ya maisha inapomtia mtu katika huzuni kali husababisha kansa, lakini pia huichochea kama ipo tayari. Dr. Anil Sood ambaye amekuwa kifanya utafiti kuhusu maradhi haya, anasema imebainika kwamba, huzuni kali husababisha kansa ya kizazi kukua na kusambaa haraka mwilini kuliko inavyofikiriwa.
Hebu
tujiulize wote linapokuja suala la mateso ya wanawake kwenye ndoa. Je kuna haja
ya kuwasaidia wanawake hao kwa kuwaambia tu kwamba, wana haki sawa na wanaume
au tuna haja ya kuwaambia pia kwamba, kukubali kwao kuishi kwenye ndoa za mateso
kuna maana ya vifo vyao kabla ya muda? Leo hii kuna idadi kubwa ya wanawake
wenye kansa na inaonyesha wazi kwamba, idadi inaongezeka kila siku. Ni nani anajua
ni kwa kiasi gani kansa zinasababishwa na kero na misukosuko ya ndoa?
Kuna
magonjwa mengi ya moyo na kisukari kwa wanawake wengi leo hii. Ukifanya utafiti
mdogo tu utabaini kwamba, akina mama wenye maradhi ya moyo, kisukari, shinikizo
la damu na hata kansa, ndoa zao zina au zilikuwa na misukosuko mingi. Nadhani
sasa imefika muda ambapo wanawake wanapaswa kuujua ukweli mkubwa zaidi kuhusu maisha
yao ya ndoa na afya zao, lakini na uhai wao kwa ujumla. Pengine wanawake wengi
hawajui kwamba, kwa kuendelea kuishi kwenye ndoa zenye huzuni na sononeko, wapo
hatarini kupata matatizo makubwa ya kimaradhi kama vile kansa. Hii ina maana
kwamba, idadi ya wanawake wanaokufa kwa mwaka kutokana na mateso ya ndoa ni
wengi sana kuliko inavyofikiriwa……
No comments:
Andika Maoni Maoni