0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Jan 30, 2016

Kumbe bado wanawake wanafuata asili katika kupenda…………!
Katika utafiti wa hivi karibuni, watafiti wamegundua kwamba, wanawake wanawapenda wanaume wasio waoga na mashujaa kuliko wale waoga. Ushujaa wa wanaume ni kigezo kikubwa kwa wanawake kuwapenda marafiki wa kiume wa muda mrefu na muda mfupi. Hii inamaanisha kwamba katika urafiki wa kawaida na wa kimapenzi na wa kindoa, wema au ukarimu ulionekana kwamba ni kigezo cha kawaida.

Tukirudi kwa mababu zetu wa kale walioishi mapangoni, wanawake waliwapenda wanaume shujaa ambao wangeweza kujitoa muhanga kuwalinda wao na watoto wao. Mwanaume ambaye alikuwa na uwezo wa kujitoa muhanga alionekana kuwa na uwezo wa kuwinda bila hofu na kuzama porini kutafuta chakula kwa Ajili ya familia au kutafuta dawa kwa ajili ya matibabu kwa familia yake.


Bila shaka ushujaa huo kwa wakati huo ulikuwa na maana ya mwanaume kuwa na uwezo wa kuifanya familia ijihisi salama kwa kuhakikishiwa chakula, malazi, mavazi na afya. Kwa maana hiyo, fedha ambayo ndiyo inayotamalaki hivi sasa, ndicho chombo kinachowafanya wengi kuamini kwamba kuwa na fedha inamaanisha wako salama. Kwani huduma zote hizo zinapatikana kwa urahisi pale mtu anapokuwa na fedha.
Kwa hiyo mwanaume mwenye nazo anaonekana kama ndiye anayeweza kuilinda familia. Ukikuta wanawake wanavutiwa na wanaume wenye fedha, usishangae, kwani bado wanafuata ule wito wa asili wa haja ya mwanamke kuhakikishiwa usalama wake.

Kwa maana nyingine ni kwamba kinachotafutwa na wanawake ni kuhakikishiwa usalama.............Siku hizi hatuwindi wanyama kama sehemu ya chakula, hatuchimbi miti shamba kwa ajili ya tiba bali fedha imechukua nafasi katika kujihakikishia usalama wetu........ Kila kitu siku hizi ni pesa na ndio maana wanawake kwa dhana ile ile ya kujihakikishia usalama wanavutiwa na wanaume wenye nazo........
Sio kwa sababu ya tamaa......La hasha, ni kutaka kuwa na uhakika na maisha yake na familia yake baadae, kama akikosa sifa ya fedha ataangalia mwanaume mwenye ujasiri wa kuthubutu na mchakarikaji, hapo anajua kwamba kwa kushirikiana mbeleni maisha yatakuwa mazuri na salama................
Ikitokea kwa mfano kaolewa na mwanaume mzigo au siku hizi tunawaita "Dead alive" Jukumu la kutafuta hulishika mwenyewe kwa sababu hamna jinsi na mara nyingi hufanikiwa kuzikamata kwa sababu anafanya hivyo kwa nia na dhamira ya kujihakikishia usalama.
Kama vile wanaume wanavyokosea kuoa kwa kutopiga hesabu zao vizuri katika kuoa vivo hivyo wanawake nao hukosea kwa kudanganyika na zile sifa za mwanaume za muda mfupi bila kuchunguza vizuri zaidi. Wapo ambao wakigundua kwamba mwanaume aliyeolewa naye ni mvivu na asiyejali familia anafungasha na kuondoka, lakini wapo ambao wanatafuta suluhu na kuamua kushika hatamu za kuendesha nyumba hawa ni wale wanaoogopa kufanya makosa kwa mara ya pili yaani kuondoka na kuangukia kwa mwanaume mwingine mwenye sifa zisizopendeza. Hawa wanakubali matokeo na kuamua kusimama kama wao, hawayumbishwi na huwakubali wenzi wao kama walivyo.

Wanawake wa aina hii mara nyingi kufanikiwa sana tofauti na wale wanaojipweteka na kubaki wakilalamika. Lakini naomba niseme kuwa wanawake kwa kisia kikubwa ni mashujaa hawawezi kukaa na kuangalia familia ikianguka kwa sababu mwanaume hawajibiki. Wengi sana tena kiasi cha kutosha husimama na kushika nyumba kwani wanajua kwamba nyumba ikianguka mara nyingi lawama huwaendea wao.

Kwa mfano wapo wanaume wengi hali zinapokuwa ngumu huzikimbia familia zao na kuzitelekeza hata kwa miaka kadhaa, lakini wakirudi wanakuta familia ipo mbali kimandeleo na watoto wana hali nzuri. Hao ndiyo huitwa wanawake wa shoka.
Kwa hiyo swala la uelewa katika maisha siyo sifa inayotazamwa na wanaume pekee, hata wanawake pia hicho ni kigezo kikubwa kwao linapokuja swala la kutafuta mwenza. 

1 comment:
Andika Maoni Maoni
  1. mwandishi umetisha, hongera sana mada nime ielewa sana

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi