Mke
anapomjali na kumkubali mume humuongezea kujiamini…
Mahusiano
kati ya mume na mke nyumbani huweza kumfanya mume afanikiwe kwenye shughuli
zake au aanguke.
Kwa
nini?
Ni
kwamba, mtu ambaye anakataliwa na mtu au watu wanaomhusu huwa anakosa
kujiamini, huwa anafikia mahali ambapo hujichukia hata yeye mwenyewe.
Mke
anapomkosoa mume, anapomlalamikia kila mara na kuwa na ghubu, bila kujali kama
mume huyo amekosa au hapana, mume hufikia mahali huanza kujitilia mashaka kama kweli ana uwezo wa kufanya mambo, kama
kweli ana thamani anayodhani kuwa anayo.
Kujiuliza
huku mara nyingi kuna maana ya mwanaume kuanza kupoteza kujiamini na hata
kuanza kuwa na uhusiano mbaya na watu anaohusiana nao mahali pengine kama
kazini.
Unaweza
kumgundua mtu ambaye ana mke mlalamikaji, mkosoaji na mwenye ghubu kwa
kuangalia jinsi anavyojitathmini. Kama mke ni mkosoaji na mwenye ghubu kwa
mumewe ni lazima mume atakosa kujiamini
katika kufanya mambo yake mengi, ni lazima ataanza kuwa na uhusiano mmbaya na
watu wengine kutokana na hukohuko kutojiamini kwake ambako kumesababishwa na
ghubu na kukosoa kwengi kwa mkewe.
Mwanaume
ambaye ana mke mkosoaji na mwenye ghubu hutokea kutowapenda watu wengine na
kukosoa wengine inatokea kuwa sehemu muhimu kwa maisha yake, anatokea kuwa na
hasira za nkaribukaribu na ni vigumu sana kwa mtu wa aina hii kuelewana na
watu.
Baadhi
ya makampuni huko Marekani, kabla hayajampandisha mtumishi wake cheo,
humchunguza mke wa mtumishi. Hawachunguzi kama ni mzuri wa sura au kama anajua
mapenzi au kupika vizuri. Mara zote huchunguza kama mwanamke huwa anampa mumewe
moyo, kama hamkosoi na kumlalamikia na kama hana ghubu. Wanapogundua kwamba mke
wa mtumishi siyo mkosoaji wala mwenye kulalamika-lalamika humpa cheo mtumshi
kwa imani kwamba atakuwa ni mtu mwenye kujiamini.
Lakini
wanapogundua kwamba mke ni mwenye kukosoa, mwenye ghubu na mlalamikaji, kamwe
hawampi mtumishi cheo, kwa sababu wanaamini kwamba, mtumishi huyo hawezi kuwa
makini, atakuwa hajiamini.
No comments:
Andika Maoni Maoni