Tafiti nyingi zilizofanywa kwa muda mrefu zinaonyesha kwamba wanawake hutofautiana kabisa kimaumbile na wanaume kiasi kwamba inakuwa kama vile ni viumbe wawili tofauti. Mtaalamu mmoja wa mahusiano ya watu John Gray anamuelezea mwanaume kuwa anatoka sayari ya Mars na mwanamke anatoka kwenye sayari ya Venus, akiwa na maana kwamba hawa ni viumbe wawili tofauti kabisa kimaumbile.
Kimaumbile
mwanamke na mwanaume hutofautiana katika kufikiri, hisia, kuyatazama mambo,
kupokea taarifa, upendo, utashi na shukurani. Mwanamke hujali sana upendo,
yaani kupendwa kuliko ilivyo kwa wanaume. Mwanamke huridhika na yuko tayari kuvumilia
‘yasiyovumilika’ kama anahisi kwamba
anapendwa na mwanaume. Ni jambo la kushangaza sana kwamba, mwanamke
anapoambaiwa ‘nakupenda’ huwa amepewa
zawadi kubwa sana na kujisikia kuwa mshindi katika mahusiano.
Wanawake
huwa wanaamini katika kusikilizwa zaidi kuliko kupewa ufumbuzi. Ndio maana
wanawake wanapokuwa pamoja wakipeana ushauri na kupeana moyo kuhusu matatizo ya
kimahusiano yanayowakabili, hawatafuti ufumbuzi bali kutaka wenzao wawasikilize
na kuwa pamoja nao katika madhila yao.
Mwanamke
anaposema jambo ambalo linamkera kumwambia mumewe au mpenzi wake, sio kwamba
anataka apatiwe suluhisho, la hasha. Anaposema jambo hilo anategemea kusikia
mume au rafiki akionesha kusikiliza au kujali na sio ufumbuzi. Kwa bahati mbaya
wanaume huwa wanadhani wanawake hao wanatafuta ufumbuzi kwa yale wanayoyaeleza.
Kwa
mfano:
Mwanamke
anapomwambia mumewe au rafiki yake, “siku
hizi naona kazi zimenizidi sana” hategemei kupewa ufumbuzi wa hilo, badala
yake anataka kusikia mwanaume aua rafiki yake akichangia katika hisia (Kumbuka
mwanamke hujali zaidi hisia). Katika hili kwa bahati mbaya mwanaume atasema, “punguza baadhi ya kazi” au “labda utafute msichana wa kazi” au “na wewe unajiumiza bure, kazi nyingine
hazina hata maana…..”
Kwa
kuwa mwanaume ni mtu wa ufumbuzi tu atadhani ndicho mkewe anachohitaji, wakati
ukweli ni kwamba, mkewe anahitaji kusikilizwa tu- anahitaji mawasiliano. Mwanamke
hapa angefurahi kusikia, “pole sana mke
wangu, hebu njoo nikukumbatie kidogo….” Angefurahi kwa sababu anachotaka ni
kusikilizwa ambapo kwake ndio thamani yake.
Wakati
mwanamke anapozungumzia matatizo yenye kumtanza, mwanaume kwa bahati mbaya
hudhani kwamba mwanamke huyo anamlaumu yeye au anatafuta ufumbuzi wa matatizo
hayo kutoka kwake. Kwa hiyo kwa kadiri mwanamke anavyokuwa na matatizo zaidi
ndivyo ambavyo mwanaume anajihisi kulaumiwa. Mwanaume hajui kwamba kimaumbile
mwanamke anapozungumzia matatizo au hofu zinazomkabili huwa anataka kusikilizwa
zaidi kuliko kutafuta ufumbuzi.
Mwanaume
hajui kwamba mwanamke hujisikia ahueni kubwa kusikia tu jibu la ‘ahaa’ au ‘oh, kumbe’ kutoka kwa mwanaume, linatosha kabisa kumpa ahueni mwanamke.
NIMEIPENDA HII MADA..NI KWELI MWANAMKE ANAPENDA SANA KUSIKILIZWA...Ningefurahi kama wengi Wake kwa waume wangesoma hii...
ReplyDelete