Hizi ni miongoni mwa sababu ambazo wanaume wengi
huchomoa mapema kwa wapenzi wao wapya kabla uhusiano haujashika kasi. Kuna
wakati wanawake hukosea na kuvuka mipaka mwanzoni tu mwa uhusiano. Anamganda
mwanaume haraka sana au anaonesha dalili zote za kujipendekeza kupita kiasi.
Lakini jambo ambalo wanawake wengi hawalijui ni kwamba, wanaume wako makini sana
kuwakwepa wanawake ving’ang’anizi……..
Nitadadavua baadhi ya vijitabia vya wanawake vinavyowafanya wanaume wawaone kama ni ving’ang’anizi…..
1. Unataka kuwa naye muda mwingi kuliko kawaida…
Ni vizuri kwa wapenzi wapya kupata fursa ya kuwa
pamoja peke yao, lakini kama unakataa kuwa na mtoko, kuhudhuria sherehe au
kukutana na marafiki na kulazimisha kuwa pamoja peke yenu mahali fulani pa
faragha, basi hapo ni lazima mwanaume atadhani kwamba unataka akupe umuhimu wa
pekee muda wote. Unaweza kukuta mwanamke anakuwa king’ang’anizi kiasi kwamba
hana muda na marafiki zake au watu wengine isipokuwa mpenzi wake. Anakuwa kama
mzigo, muda wote yuko nyuma ya mwanaume kila anapokwenda…. Hapa ni lazima
mwanaume atatemana na wewe kungali mapema. Hakuna mwanaume anayeweza kujenga
mahusiano na mwanamke wa aina hii, watakukimbia kila siku.
2. Unampangia mwanaume kila kitu… Unampangia aina ya mavazi ya kuvaa, unaanza kuboresha mazingira ya nyumbani kwake haraka sana kwa kununua vitu mbalimbali vya nyumbani kwake bila kushauriana naye. Hiyo ni dalili kwamba una matarajio makubwa kwake, jambo ambalo kwake yeye bado halijamuingia akilini. Hapa mwanaume ambaye huyachukulia mambo kwa tahadhari, hukuona kuwa wewe ni king’ang’anizi na unataka kukita mizizi kwake wakati bado anachunguza uhusiano wenu ili kujua iwapo utakuwa kama vile anavyotarajia yeye… Kumbuka kwamba kila mtu ana sifa azitakazo pale anapochagua mwenza, na ni vigumu kumjua mtu kwa muda mfupi. Kunahitajika muda wa kutosha mtu kumjua mwenzake vizuri linapokuja swala la mahusianao.
2. Unampangia mwanaume kila kitu… Unampangia aina ya mavazi ya kuvaa, unaanza kuboresha mazingira ya nyumbani kwake haraka sana kwa kununua vitu mbalimbali vya nyumbani kwake bila kushauriana naye. Hiyo ni dalili kwamba una matarajio makubwa kwake, jambo ambalo kwake yeye bado halijamuingia akilini. Hapa mwanaume ambaye huyachukulia mambo kwa tahadhari, hukuona kuwa wewe ni king’ang’anizi na unataka kukita mizizi kwake wakati bado anachunguza uhusiano wenu ili kujua iwapo utakuwa kama vile anavyotarajia yeye… Kumbuka kwamba kila mtu ana sifa azitakazo pale anapochagua mwenza, na ni vigumu kumjua mtu kwa muda mfupi. Kunahitajika muda wa kutosha mtu kumjua mwenzake vizuri linapokuja swala la mahusianao.
3. Unatumia muda mwingi zaidi kukaa kwake…. Unalala kwa mpenzi wako, na
asubuhi mwanaume huyo anaondoka kwenda kwenye shughuli zake, na wewe unabaki
labda ukidai unamsaidia usafi kidogo. Lakini anaporudi jioni anakukuta bado uko
hapo nyumbani kwake ukiwa umejipumzisha. Inawezekana ukawa umeandaa chakula cha
usiku tayari na pia huenda ukawa umebeba nguo za kubadilisha kwenye mkoba wako
pamoja na vipodozi ukiwa umejiandaa kulala tena hapo kwake. Huonyeshi dalili za
kuondoka hapo kwake zaidi ya kwenda kwako au kwenu na kubadilisha nguo na
kuchukua viti vichache utakavyovihitaji utakapokuwa hapo kwake, lakini unapanga
hayo yote bila kumshirikisha zaidi ya kukuona tu ukimganda kama luba. Huonyeshi
kuwa na maisha yako kama wewe, zaidi ya kujipachika kwake……
4. Unajenga urafiki na mama yake haraka sana…… Baada ya kukutambulisha kwa
mama yake na kubadilishana namba za simu au labda na email, unaanza kujenga
ukaribu na mama yake kupita kiasi. Wanawake wengi hudhani kwamba, iwapo
watajenga urafiki na mama wakwe watarajiwa, basi itakuwa rahisi kwao kumnasa
mwanaume huyo, maana huamini kwamba watoto wa kiume hawawezi kwenda kinyume na
mama zao linapokuja swala la kuchagua mwenza. Kwa kawaida wanaume humuona
mwanamke anayejipendekeza kwa mama yake kama vile anataka kulazimisha uhusiano
au ndoa, hivyo humchukulia kama ni king’ang’anizi.
5. Unampigia simu na kumuuliza kama yuko wapi….. Unapompigia simu badala ya kumjulia hali unakuwa na maswali ya kipolisi.. ‘Uko wapi?’ ‘Unafanya nini? Maswali ya aina hiyo mwanaume huyachukulia kama ya kimtego na hawafurahishwi nayo. Wanawake wengi huamini kwamba wanaume huwa hawasemi ukweli kuhusu mahali walipo pale wanapoulizwa na wenzi wao. Jambo hilo linaweza kuwa kweli au lisiwe kweli. Inawezekana kuwa kweli kwa sababu labda ya wanaume kukwepa maswali mengi. Mara nyingi wanawake hawaridhiki na jibu moja. Mfano ni jioni ndio ametoka kazini, lakini nakapitia mahali fulani kukutana na rafiki yake, inawezekana ikawa ni kwenye mghahawa au kwenye baa. Kama mwanamke akipiga simu na mwanaume akamwambai yuko kwenye baa na rafiki yake, yatafuata maswali lukuki. Hakuna mwanaume anayependa kuulizwa maswali mengi kama vile anatuhumiwa. Na ndio sababu wanaume wengi wanakwepe kusema mahali walipo. Kwa hiyo ili kuepuka maswali anaweza kujibu kwa kifupi tu kwamba yuko kwenye kikao kazini na hatakuwa hewani, ili apate nafasi ya kuzima simu japo kwa muda. Mwanaume humuona mwanamke mwenye udadisi wa aina hiyo kama king’ang’anizi.
6. Unakuwa na chuki na wanawake wenzako… Pale ambapo mwenzi wako anapomtaja mwanamke fulani, inaweza kuwa ni mfanyakazi mwenzake, mke wa kaka yake au mtu wanayeshirikiana kibiashara, unaonyesha kisirani cha waziwazi kwamba unakerwa na ukaribu wake na wanawake wengine. Tabia hii inaashiria kwamba wewe unapenda kumiliki na wanaume wengi huwa hawapendi wanawake wenye vijitabia vya kupenda kumiliki. Hapo ni lazima utaonekana kuwa wewe ni king’ang’anizi na uhusiano wenu utavunjika mapema…..
7. Unakubali kila analosema au kila anachokifanya….Kuna kitu kinaitwa ‘uhusiano wa kinyonga.’ Hapa mwanamke anajibadili kupita kiasi ili afanane na mwenzi wake. Unakuta mwanamke anakubali kila kitu anachokiamini mwenzi wake bila kuhoji. Anapoteza utambulisho wake na kujipachika utambulisho wa mwenzi wake. Mwanaume akikuona uko hivyo, atakukimbia, atajua wewe ni king’ang’anizi
8.
Unawazungumzia mabwana ulioachana nao kila wakati…Kama
una kawaida ya kumzungumzia mwanaume uliyeachana naye mara kwa mara uwapo na
mpenzi wako mpya, ina maana kwamba bado hujaachana na jakamoyo la kuachwa.
Hakuna mwanaume anayependa kusikia kuhusu mahusiano yako ya nyuma, kwa sababu
hayamuhusu. Kama ukiwa unapenda kumzungumzia mpenzi wako wa zamani kila uwapo
na mpenzi wako mpya, jua kwamba na yeye pia utampoteza kwa sababu atakuona kuwa
wewe ni dhaifu na king’ang’anizi na ndio maana umeshindwa kusimama kama wewe,
na badala yake unawaza kuhusu mtu uliyeachana naye pamoja na kwamba uko naye.
Sio kwamba ni vibaya kumzungumzia mpenzi mliyeachana, lakini ni vyema kama
utamzungumzia pale ambapo kuna ulazima sana wa kufanya hivyo, labda kuna jambo
ambalo limamhusu ambalo mnajadili, na ikakulazimu kumtaja…..
No comments:
Andika Maoni Maoni